Mahitaji:
Samaki mmoja, nyama ya kondoo gramu 600, mboga gramu 50, mchuzi wa soya gramu 60, sukari gramu 40, chembechembe za kukoleza ladha gramu 2, chumvi gramu 2, vitunguu maji gramu 10, tangawizi gramu 10, kiasi kidogo cha pilipili manga
njia:
1. osha samaki, ondoa kichwa na mkia wake, halafu kata awe vipande, kata nyama ya kondoo iwe vipande.
2. washa moto mimina mafuta kwenye sufuria, tia vipande vya vitunguu maji na tangawizi korogakoroga, uviweke vipande vya samaki kwenye sufuria vikaange, halafu tia vipande vya nyama ya kondoo, mimina mchuzi wa soya, mvinyo wa kupikia, tia chumvi na mimina maji, korogakoroga baada ya kuchemka, punguza moto endelea kuchemsha kwa muda, tia sukari na ongeza moto, tia pilipili manga, korogakoroga, pakua vipande vya samaki kwenye sahani, halafu weka vipande vya nyama ya kondoo kwenye samaki, mimina mchuzi wa samaki uliochemka. Mpaka hapo kitoweo hiki kiko tayari kuliwa.
|