Wafanyakazi wa Idhaa ya Kiswahili ya CRI
China Radio International
China
Dunia
(GMT+08:00) 2007-02-28 16:26:05    
Wataalamu watoa mapendekezo kuhusu suala la idadi ya watu na maendeleo ya China

cri

China ikiwa ni nchi yenye idadi kubwa ya watu duniani, serikali ya China imechukua hatua nyingi na kutoa sera mbalimbali ili kuhimiza maendeleo yenye uwiano kati ya idadi ya watu,  na maendeleo ya uchumi na jamii. Wakati wa kutekeleza hatua na sera hizo, serikali ya China pia inatilia maanani maoni na mapendekezo ya wataalamu. Kwenye kongamano la idadi ya watu na maendeleo ya China lililofanyika hivi karibuni, wataalamu kumi kadhaa kutoka idara mbalimbali za utafiti za China walifanya majadiliano kuhusu masuala mengi yanayohusu idadi ya watu wa China.

China inatekeleza sera ya mpango wa uzazi kuanzia miaka ya 70 ya karne iliyopita. Kutokana na sera hiyo, katika miaka 30 iliyopita, kiasi cha uzazi kimeendelea kupungua na hali hiyo imepunguza watu milioni 400. wataalamu wanaona kuwa, hivi sasa China bado inapaswa kudumisha kiwango cha chini cha uzazi. Mtafiti wa taasisi ya idadi ya watu ya China Bw. Tian Xueyuan alisema:

"kwa nini tunasema hivi sasa China bado inapaswa kuweka mkazo katika udhibiti wa idadi ya watu? Kwa sababu tatizo la kimsingi la suala la idadi ya watu wa China ni kuwa zaidi ya nguvu ni kubwa kuliko nguvu kazi ile inayohitajika katika shughuli za uzalishaji mali nchini China."

Katika nchi nyingi zilizoendelea, suala la idadi ya watu ni upungufu wa nguvu kazi. Kwa China, suala hilo linakwenda kinyume kabisa. Kutokana na kiasi kikubwa cha uzazi wa watu kabla ya miaka 30 iliyopita, ongezeko la kasi la idadi ya watu ni moja ya changamoto kubwa zinazoikabili China.

Wataalamu wanaona kuwa, hivi sasa kiwango cha uzazi nchini China kimepungua na kufikia kiwango cha chini, na ni lazima kudumisha kiwango hicho, lakini haimaanishi kuwa kiwango hicho kikiwa chini zaidi kitakuwa bora zaidi. Kwa kuwa kiwango cha chini kupita kiasi kitafanya idadi ya wazee iongezeke zaidi, na pia kitaathiri shughuli za kuinua sifa ya wananchi, yote hayo yatatoa athari mbaya kwa maendeleo ya kiuchumi na kijamii. Mtafiti wa taasisi ya idadi ya watu katika taasisi ya sayansi ya jamii ya China Bw. Tian Xueyuan alisema:

"sidhani kuwa kiwango cha uzazi kikiwa chini zaidi, kitakuwa bora zaidi, bali kinapaswa kudhibitiwa vizuri ili kuidumisha katika kiwango kinachofaa kutokana na hali halisi ya China."

Wataalamu waliohudhuria mkutano huo wana maoni tofauti kuhusu masuala na chamgamoto zinazoikabili China. Kuhusu suala la kuongezeka kwa wazee nchini China, profesa wa taasisi ya idadi ya watu na maendeleo katika chuo kikuu cha Umma cha China Bw. Wu Cangping alisema, ifikapo mwaka 2020, idadi ya wazee wenye umri wa zaidi ya miaka 65 nchini China itafikia milioni 164, ikichukua asilimia 11.2 ya idadi ya jumla ya watu wa China. Inakadiriwa kuwa katika miaka ya 40 ya karne hiyo idadi ya wazee nchini China itafikia kilele na wakati huo kila mmoja kati ya watatu au wanne ni wazee. Suala la kuongezeka kwa wazee litaongeza shinikizo kwa mfumo wa huduma za jamii na huduma za umma.

Hivyo profesa Wu anapendekeza kuwa China inapaswa kujenga mara moja mfumo wa utoaji huduma kwa wazee na mfumo kamili wa huduma za jamii, na kukamilisha sheria kuhusu uhakikisho wa haki za wazee na watoto kuwalisha na kuwahudumia wazazi wao waliozeeka. China pia inapaswa kuimarisha huduma kwa ajili ya wazee kwenye maeneo ya makazi na kuendeleza zaidi sekta ya huduma kwa ajili ya wazee.

Mkurugenzi wa taasisi ya idadi ya watu na maendeleo ya China Bi. Ma Li anafuatilia hali ya kupotea kwa uwiano wa kijinsia wa watoto nchini China.

Uwiano wa kijinsia wa watoto ni kiasi cha idadi ya watoto wachanga wa kiume kwa ile ya watoto wachanga wa kike. kwa kawaida kiasi hicho kinafuata kanuni za baiolojia na kudumisha kwenye 103/100 hadi 107/100. lakini kuanzia miaka ya 80 ya karne iliyopita, kiasi hicho kimeendelea kuongezeka mwaka hadi mwaka, katika mwaka 2005, kiasi hicho kilifikia 118/100. kwenye baadhi ya mikoa, kiasi hicho hata kilizidi 130/100. Bi. Ma Li alisema:

"suala la kupotea kwa uwiano wa kijinsia wa watoto nchini China si kama tu linadumu kwa muda mrefu, bali pia linaathari eneo kubwa zaidi. Kama hali hiyo ikiendelea kuwepo, italeta matatizo makubwa ya kijamii."

Bi. Ma Li alisema, serikali ya China inapaswa kuchukua hatua za utatuzi wa jumla, kukamilisha sheria za kuhimiza usawa wa kijinsia na sheria za kulinda haki halali za wanawake na watoto. Seriakli pia inapaswa kupiga marufuku na kuadhibisha vitendo vya kutoa mimba kwa ajili ya kuchagua jinsia ya watoto.

Maofisa wanaoshughulikia mambo kuhusu idadi ya watu walisikiliza kwa makini mashauri ya wataalamu. Mkuu wa idara ya mpango na maendeleo katika kamati ya idadi ya watu na mpango wa uzazi ya China Bw. Chen Li alisema, mpaka sasa China imepita kwenye vipindi vitatu katika shughuli za udhibiti wa idadi ya watu:

"kipindi cha kwanza ni kupunguza kiwango cha uzazi; cha pili ni kudumisha kiwango cha chini cha uzazi. Hivi sasa China imeingia kwenye kipindi kitatu yaani kutatua kwa jumla suala la idadi ya watu kwenye msingi wa kudumisha kiwango cha chini cha uzazi. China inapaswa kuendelea kuinua sifa ya wananchi na kuboresha muundo wa idadi ya watu ili kuwa nchi yenye raslimali nyingi za nguvu kazi duanini."

Mkurugenzi wa kamati ya idadi ya watu na mpango wa uzazi ya China Bw. Zhang Weiqing alisema, ili kutatua suala la kupotea kwa uwiano wa kijinsia za watoto, China inapaswa kuchukua hatua za jumla, zikiwemo kuinua kwa haraka kiwango cha maisha ya wananchi, kukamilisha zaidi mfumo na utaratibu wa huduma za jamii; kuinua hadhi ya kijamii na kiuchumi ya watoto na wanawake; kupiga marufuku na kuadhibisha vikali vitendo vya kutoa mimba kwa ajili ya kuchagua jinsia ya watoto; China inapanga kutumia miaka 10 hadi 15 kutimiza kimsingi uwiano wa kijinsia wa watoto nchini humo.

Kuhusu hali ya kuongezeka kwa wazee, Bw. Zhang Weiqing alisema, hivi sasa China imeanza kuingia kwenye kipindi cha jamii yenye wazee wengi, wakati huo serikali ya China inapaswa kutilia maanani suala hilo na kuchukua hatua mwafaka, suala hilo litatatuliwa bila matatizo.

Idhaa ya kiswahili 2007-02-28