Mahitaji
Matango ya baharini kilo 1, vitunguu maji gramu 300, tangawizi gramu 10, mvinyo wa kupikia vijiko vitano, sukari vijiko viwili, chumvi kijiko kimoja, mchuzi wa soya kijiko kimoja, M.S.G kijiko kimoja, mafuta ya ufuta kijiko kimoja, maji ya wanga, na maji bakuli moja.
Njia
1. chemsha maji halafu tia matango ya baharini kwenye maji baada ya dakika mbili yapakue na uyakausha.
2. tia mafuta kwenye sufuria yachemshe tia vipande vya vitunguu maji kwenye sufuria vikaange mpaka viwe rangi ya hudhurungi kisha vipakue.
3. pasha moto tena, tia vipande vya vitunguu maji na tangawizi, korogakoroga, tia matango ya baharini korogakoroga, mimina mvinyo wa kupikia, mchuzi wa soya, tia M.S.G, sukari na vipande vya vitunguu maji vilivyokaangwa, korogakoroga kwa dakika mbili, mimina maji ya wanga, korogakoroga, tia mafuta ya ufuta korogakoroga, kasha ipakue. Mpaka hapo kitoweo hiki kiko tayari kuliwa.
|