Wafanyakazi wa Idhaa ya Kiswahili ya CRI
China Radio International
China
Dunia
(GMT+08:00) 2007-03-07 20:18:39    
Chuo kikuu cha makabila cha kusini magharibi ya China

cri

China ni nchi yenye makabila mengi, mbali na kabila la waHan, pia kuna makabila 55 madogomadogo. Katika muda mrefu uliopita, kutokana na sababu mbalimbali za kihistoria na kimaumbile, kiwango cha elemu kwenye baadhi ya sehemu za makabila madogomadogo bado kiko nyuma kuliko kiwango kinachohitajika kwa ajili ya mandeleo ya kiuchumi na kijamii ya huko.Hivyo katika miaka mingi iliyopita, serikali ya China ilianzisha shule za aina mbalimbali, hasa vyuo vikuu vya makabila, kuandaa watu wenye ujuzi kutokana na hali halisi ya makabila hayo.

Chuo Kikuu cha makabila cha China kipo kusini magharibi mwa China katika mji wa Chengdu ambao ni mji mkuu wa mkoa wa Sichuan uliko kusini magharibi mwa China.Naibu mkuu wa chuo kikuu hicho Bw. Zeng Ming alisemachuo kikuu hicho kilichoanzishwa mwaka 1951, ni moja kati ya vyuo vikuu vya makabila vilivyoanzishwa mapema zaidi baada ya kuanzishwa kwa China mpya. Hivi sasa wanafunzi wanaosoma katika chuo kikuu hicho wanatoka kwenye makabila yote 56. Bwa Zeng Ming alisema:

Baadhi ya wanafunzi wanatoka kwenye kabila dogo lenye watu elfu kadhaa tu, na ni mwanafunzi mmoja wa kabila hilo ambaye aliweza kushiriki kwenye mtihani wa kujiunga na vikuu na kufanikiwa kujiunga na chuo hicho.

Aidha msichana mmoja wa kabila la Tajik wanayemwita "mgeni kutoka mlima wa barafu" alitembea kwa miguu kwa zaidi ya mwezi mmoja kutoka maskani yake hadi chuo chetu"

Imefahamika kuwa, miaka 50 tangu chuo kiazishwe kimeshaandaa watu wenye utaalam wa aina mbalimbali zaidi ya elfu 90.Miongoni mwao kunamadaktari wa kwanza wa makabila ya wa Tibeti na wa kabila la waQiang nchini China, pamoja na wataalam na wasomi wengi mashuhuri. Watu hao wametoa mchango kwa maendeleo na ujenzi wa sehemu za makabila madogomadogo nchini China.

Lakini kila kabila lina lugha na mila tofauti, ni vipi wanafunzi kutoka makabila 56 wanweza kupatana na kuhimizana katika chuo kikuu hicho?

Kwa mfano wa chuo kikuu cha waYi, mkuu wa chuo hicho Profesa Wuniduoqie alieleza kuwa, katika kutoa elimu, chuo hicho kinasisitiza umaalum wa "tofauti pamoja na masikilizano" Hivi sasa chuo hicho kimekuwa kituo muhimu cha kuandaa wataalamu wa lugha mbili za kichina na KiiYi na wataalamu wa utafiti wa kabila la wa Yi. Profesa Wuniduoqie alieleza:

"Kila kabila lina mila, desturi, na utamaduni tofauti, mila, utamaduni na dini zao zote zinaheshimiwa kikamilifu katika chuo hicho.Kutokana na hali hiyo, elimu ya makabila madogomadogo imepata maendeleo kamili na ya kudumu, shugjuli za kuandaa wataalamu wa makabila madogomadogo pia zimekuwa na umaaalumu wa kipekee.

Ili kuwasaidia wanafunzi wapya kuzoea haraka maisha ya chuoni, chuo kikuu cha makabila cha kusini magharibi ya China kilianzisha kituo cha elimu ya afya na saikolojia, ili kutoa huduma kwa wanafunzi wapya. Mwalimu mmoja wa kituo hicho alisema, kituo hicho kinaweza kutoa misaada kwa wanafunzi wakikumbwa na matatizo ya kisaikolojia, pia kinawasaidia wanafunzi kuzoea haraka maisha ya chuo kikuu.

Wanafunzi wengi walioandikishwa na chuo kikuu hicho wanatoka sehemu za mbali na zilizo nyuma kiuchumi.Kutokana na hali hiyo, idara husika za chuo hicho zimetekeleza kwa makini sera husika za nchi kuhusu utoaji wa ruzuku na mikopo ya misaada ya masomo kwa wanafunzi wenye matatizo ya kiuchumi.Aidha, chuo kikuu hicho pia kinatoa nafasi za kazi zenye kipato kwa wanafunzi ili waweze kumudu kidogo ada za masomo. Mwanafunzi wa kabila la waZhuang kutoka chuo cha uhandisi wa kompyuta ni mmoja kati ya wanafunzi waliopewa misaada. Alisema:

"Jina langu ni Luo Wen, natoka sehemu inayojiendesha ya kabila la wazhuang ya Guangxi.Kwa kuwa hali ya kiuchumi ya familia yangu si nzuri, chuo kikuu kilitoa nafasi ya kazi yenye kipato., baada ya usaili nilipewa nafasi ya msaidizi wa utoaji mikopo ya misaada ya kimasomo ya taifa na kushughulikia maombi ya mikopo hiyo.Kazi hiyo inatoa misaada ya kiuchumi kwa maisha yangu, jambo muhimu zaidi ni kwamba nimepata uzoefu katika kazi hiyo.

Shughuli mbalimbali zinazoandaliwa na chuo kikuu hicho zinasifiwa sana na wanafunzi, ambazo ni pamoja na sherehe mbalimbali, mashindano ya hotuba au mashindano ya sanaa za maandiko.Miongoni mwa shughuri hizo, tamasha la utamaduni la vyakula vya makabila mbalimbalimbali linapendwa zaidi na wanafunzi.Imefahamika kuwa, tamasha la utamaduni wa vyakula vya makabila mbalimbali linafanyika mara moja kila mwaka, wakati huo wanafunzi hupika vyakula maalum vya makabila yao kwenye uwanja wa michezo wa chuo kikuu hicho, ili waweze kuonja vyakula vya makabila mbalimbali.

Kijana He Jian anayetoka kabila la waTibet ansoma katika chuo cha luhga za kigeni. Alimwambia mwandishi wetu wa habari kuwa, anakipenda sana chuo hicho amabao ameishi kwa miaka mitatu.

Alisema:

"Baada ya kujiunga na chuo kikuu hiki, naona kuwa hali ya kiutamaduni ya chuo hiki ni nzuri sana.Nimekutana na wanafunzi kutoka makabila na sehemu mbalimbali, na hali hiyo imenisaidia kupanua uelewa wangu.Niliwahi kugombea nafasi ya mkuu wa darasa, kuandaa shughuli mbalimbali na kuwasiliana na wanafunzi wengi, hayo yote yemenifanya nijiamini zaidi."

Naibu mkuu wa chuo kikuu hicho Bw. Zeng Ming alisema, chuko kikuu hicho kiliandaa wanafunzi kutoka makabila mbalimbali kizazi baada ya kizazi.Katika siku za baadaye, chuo kikuu hicho kitaendelea kushikilia mtizamo wa elimu yenye masikilizano ili kukiendeleza chuo kikuu hicho kuwa chuo kikuu cha kisasa cha makabila nchini China.