Wafanyakazi wa Idhaa ya Kiswahili ya CRI
China Radio International
China
Dunia
(GMT+08:00) 2007-03-12 15:20:10    
Mwanamuziki Tan Dun

cri

Bw. Tan Dun ni mwanamuziki mashuhuri wa China. Muziki alioutunga kwa ajili ya filamu ya "Mahali Penye Watu Hodari" ulipata tuzo ya Oscar mwaka 2001, ambayo ni mwanamuziki wa kwanza wa China kupata tuzo hiyo. Bw. Tan Dun anazingatia sana kuunganisha mtindo wa Kichina na wa Kimagharibi na kuufanya muziki wake kuwa wa aina mpya, na unaopokelewa na watu wa magharibi kwa furaha.

Bw. Tan Dun alizaliwa mwaka 1957 mkoani Hunan China. Alipokuwa mtoto siku moja baba yake alimletea filimbi na kinanda cha Kichina, vitu ambavyo vilimfanya aanze safari ya kuwa mwanamuziki mkubwa. Alipokuwa mtoto aliwahi kujifunza ala nyingi za muziki ikiwa ni pamoja na ala za Kichina na fidla.

Kwenye maskani yake sherehe zote za ndoa au mazishi hufanyika pamoja na muziki wa kienyeji, hali hiyo ilimfanya awe na kipaji cha muziki.

Mliosikia ni sehemu ya muziki alioutunga kwa ajili ya filamu ya "Karamu ya Usiku". Muziki huo ulipigwa kwa ala za nyuzi za Kichina ambao unawaletea wasikilizaji mazingira ya siku za kale nchini China. Bw. Tan Dun anaona kuwa utamaduni wa maskani yake Hunan unachangia sana utungaji wake wa muziki.

Mwishoni mwa miaka 70 ya karne iliyopita Bw. Tan Dun alijiunga na Chuo Kikuu cha Muziki cha Beijing na kusomea utungaji wa muziki, baada ya kupata shahada ya pili alikwenda Marekani na kujiunga na Chuo Kikuu cha Columbia ili kuongeza elimu kuhusu muziki wa kale wa nchi za magharibi na alipata shahada ya kwanza. Kuanzia hapo hadi sasa anaishi Marekani. Alihama kutoka maskani yake mkoani Hunan hadi Beijing, na kutoka Beijing alihamia New York, uhamisho huo ulimfahamisha kwa kina utamaduni tofauti, na tofauti hizo zina athari katika utungaji wake wa muziki. Alisema,

"Maishani mwangu nilikutwa mara mbli na migongano ya utamaduni. Mara ya kwanza ilitokea nilipohamia Beijing kutoka maskani yangu mkoani Hunan, na mara ya pili ilitokea nilipohamia New York kutoka Beijing. Aina tofauti za utamaduni, makabila na mazingira zinaniathiri sana. Tofauti hizo sio rangi ya ngozi na lugha, bali hata mazoea ya chakula na mavazi."

Wakati alipokuwa anasoma New York, Tan Dun alikuwa kama wanafunzi wengine wa China, waliosumbuliwa sana na utamaduni tofauti. Katika muda mrefu wa kujirekebisha kiutamaduni, suala alilotafakari zaidi ni namna ya kuunganisha utamaduni wa China na wa Magharibi, na alipata mafanikio.

Katika eneo la muziki wa kale wa kimataifa, Bw. Tan Dun anajulikana kwa muziki wake wa kuunganisha mitindo tofauti ya muziki. Muziki wake wa filamu ya "Mahali Penye Watu Hodari" alioutunga kwa miaka minne ni mfano wa muunganisho wa mtindo ya Kichina na wa Kimagharibi. Kwa kutumia sifa tofauti za ala za Kichina na ala za Kimagharibi aliufanya muziki wake uwe wa ajabu na wa kuhuzunisha, ambao unalingana kabisa na mazingira ya hadithi za gongfu katika China ya kale.

Mliosikia ni muziki wa filamu ya "Mahali Penye Watu Hodari". Muziki huo ulipata tuzo ya muziki ya Oscar mwaka 2001.

Pamoja na mafanikio ya kuunganisha mtindo wa muziki wa Kichina na wa Kimagharibi, kumetokea maoni mengi tofauti, lakini Bw. Tan Dun anaamini kuwa muziki ni wa duniani kote, hauna mipaka. Alisema,

"Maneno makali yaliyonikosoa yalitokea kwenye magazeti ya New York, yakisema ni afadhali nitunge muziki wa Kichina tu, kwa nini nitunge muziki wa fidla? Mchina anafaa kutunga muziki wa Kichina, na muziki wa Kichina unafaa tu kwa Wachina. Naona kuwa maneno hayo ni makosa kabisa, na naona mimi ni mtungaji muziki duniani, muziki wangu unatungwa kwa ajili ya watu wote duniani."

Hivi sasa Bw. Tan Dun mwenye umri wa miaka 50 anaishi New York. Maisha yake ni ya kawaida kabisa.

Idhaa ya kiswahili 2007-03-12