Mkutano wa Baraza la Mashauriano ya Kisiasa la China ulifanyika hapa Beijing. Miongoni mwa wajumbe walioshiriki katika mkutano huo wako wajumbe zaidi ya 150 kutoka nyanja ya fasihi na sanaa, ambao kama wajumbe wengine walijitahidi kutoa maoni na mapendekezo yao kutokana na uchunguzi wao.
Bi. Li Guyi ni mwimbaji anayejulikana kwa Wachina wote, kila mwaka katika sherehe ya sikukuu ya mwaka mpya wa Kichina inayotangazwa kote nchini China kupitia televisheni anaimba wimbo wake wa "usiku usiosahaulika" wakati sherehe inapomalizika. Kuanzia mwaka 1983 Bi. Li Guyi amekuwa mjumbe wa Baraza la Mashauriano ya Kisiasa la China.
Utaratibu wa ushirikiano wa vyama vyingi na mashauriano ya kisiasa chini ya uongozi wa Chama cha Kikomunisti cha China ni utaratibu wa kimsingi wa kisiasa nchini China, wajumbe wa Baraza hilo wote ni wataalamu wa sekta mbalimbali, na kutokana na ukaguzi na uchunguzi wao waliwasilisha maoni na mapendekezo serikalini kwa niaba ya umma kuhusu hali na masuala ya jamii.
Bi. Li Guyi alipozungumza na waandishi wa habari alisema, miaka miwili ya mwanzo baada ya kuwa mjumbe aliona fahari tu bila kuona majukumu yake, kwa hiyo hakutoa pendekezo lolote. Baadaye katika muda wa miaka 25 hivi alitoa mapendekezo yasiyopungua 40 kuhusu mawasiliano, afya na matibabu. Jambo linalomfurahisha ni kuwa pendekezo alilotoa pamoja na wajumbe wengine la kujenga jumba la taifa la opera limemalizika kujengwa Beijing. Mwaka huu ametoa mapendekezo sita na yote yanahusu hifadhi ya mazingira na kupunguza ufadhirifu wa nishati. Alisema, kutokana na kasi ya maendeleo ya uchumi watu wanazidi kukimbilia mambo ya anasa. Kwa mfano bidhaa za kawaida hufungwa kwa maridadi na anasa, huu ni ubadhirifu wa maliasili na kuleta uchafuzi wa mazingira baada ya kutupwa. Hali hiyo alichunguza kwa muda mrefu. Alipokuwa katika nchi za nje aliona kwamba vitu ndani ya mabafu katika hoteli vyote havifungwi. Alichukua vitu hivi kwenye mkutano kama ni ushahidi. Baada ya kuwa mjumbe Bi. Li Guyi amekuwa mtu wa makini sana katika uchunguzi wa hali ya jamii na mazingira, na mara kwa mara kuna watu wanaokuja kwake kueleza maoni na matatizo yao. Alisema,
"Kuisaidia serikali kuboresha utawala ni majukumu ya wajumbe, kwa sababu wanaishi miongoni mwa umma, wanaelewa zaidi matatizo yao. Watu wanasema, wewe ni mjumbe tusaidie kusilisha maoni yetu Barazani."
Kama Bi. Li Guyi alivyo, mjumbe ambaye ni mkuu wa Kundi la Opera ya Kibeijing Bw. Wu Jiang alisema,
"Sisi wajumbe ni lazima tufahamu majukumu yetu. Kuhusu matatizo yanayozungumzwa sana katika jamii sio matatizo ambayo wajumbe wanapaswa kuyafuatilia sana kwa sababu matatizo hayo serikali ishafahamu na kuzingatia. Majukumu yetu ni kugundua matatizo yatakayotokea baadaye, ambayo kwa sasa serikali haijawahi kugundua na kuzingatia. Baraza la Mashauri ya Kisiasa limekusanya wataalamu wengi wa sekta mbalimbali, ni majukumu yao kugundua matatizo yatakayotokea hapo baadaye ili serikali iwe tayari kwa sasa."
Kundi la Opera ya Kibeijing linawakilisha kiwango cha juu cha sanaa ya opera hiyo nchini China. Mwaka huu Bw. Wu Jiang alitoa pendekezo moja tu, nalo ni kufanya utafiti nadharia ya maonesho ya opera ya Kibeijing. Alisema katika zama ambazo aina za michezo ya sanaa zimekuwa nyingi, shughuli za kuhifadhi na kurithisha sanaa ya opera ya Kibeijing yenye historia ndefu ni lazima zianza mapema.
Bw. Zhang Xianliang ni mwandishi wa vitabu. Alisema, tokea mwaka 1983 alipokuwa mjumbe alikuwa anafuatilia sana matatizo yanayotokea jinsi mageuzi yanavyoendelea. Hapo kabla mapendekezo yake yalikuwa yanahusu uandishi wa vitabu tu, lakini tokea karne hii mapendekezo yake yamehusu sekta nyingine. Aliwaambia waandishi wa habari,
"Pendekezo langu mwaka huu ni kuwa katika 'Sheria ya Watumishi wa Serikali' ni lazima iongezwe kipengele cha kuwataka watumishi wa serikali wenye ngazi fulani lazima watangaze mali zao kila baada ya muda fulani. Hii ni hatua muhimu dhidi ya ufisadi."
Mwigizaji mashuhuri wa tamthilia ya kuchekesha Bw. Huaang Hong kwenye mkutano huo alitoa pendekezo lake kuhusu matatizo ya wakulima wanaofanya kazi za vibarua mijini yakiwa ni pamoja na utaratibu wa kuongeza mishahara yao, uhakikisho wa kupata huduma za jamii na kuwainulia utamaduni. Utungaji wake wa tamthlia karibu wote unaeleza maisha ya wakulima wanaofanya kazi za vibarua mijini aliingilia sana maisha ya vibarua hao. Alisema,
"Kabla ya kuwa mjumbe nilikuwa naandika tu mambo yao kwenye vitabu vyangu lakini baada ya kuwa mjumbe nimekuwa na majukumu ya kuzingatia matatizo yanayowakabili wate."
Miongoni mwa wajumbe wako wengi kutoka fasihi na sanaa, kwa kufanya uchunguzi, ufafanuzi na tafakuri walitoa mapendekezo yao kusaidia serikali kuboredha utawala.
Idhaa ya kiswahili 2007-03-19
|