Baada ya kufanya kazi ngumu zilizodumu kwa miezi sita, katikati ya pili mwezi March, kikosi cha Walungu cha askari wa uhandishi wa kulinda amani wa China nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo kilikamilisha ujenzi wa uwanja wa ndege na kambi ya jeshi la Pakistan kwenye sehemu ya Walungu, mkoani Kivu ya Kusini. Huo ulikuwa mradi mkubwa wa kwanza kwa kikosi hicho tangu kiwasili nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo. Hivi sasa mradi huo umefanikiwa kupitishwa kwenye ukaguzi, na askari hao wa China walioshiriki kwenye mradi huo walisifiwa sana na maofisa wa ujumbe wa Umoja wa Mataifa kwenye nchi hiyo.
Mwezi Septemba mwaka 2006, mara kikosi hicho kilipowasili sehemu ambapo kilitekeleza jukumu, kilipokea amri na kuwatuma askari 45 kwenye kambi ya ujenzi ya Walungu. Kambi hiyo iko kwenye mlima wenye mwinuko wa mita 2,000 kutoka usawa wa bahari. Ingawa mandhari ya huko ni nzuri sana, lakini mazingira ya kazi ya huko ni ngumu sana. sehemu hiyo ina unyevunyevu mwingi, ndani ya hema kuna hali ya ukungu, hata unaota uyoga. na nguo za askari siku zote zilikuwa za unyevunyevu. Halijoto ya mchana ya huko inafikia 40?C, ilikuwa joto sana ndani ya hema. Lakini halijoto ya usiku ya huko inapungua kuwa 5?C, askari hao walikuwa wanalala na mablanketi zeneye unyevunyevu, ndani ya hema ilikuwa baridi sana.
Kutokana na hali ngumu, kikosi hicho cha Walungu kilikuwa kinapata huduma mara moja kila wiki, askari hao walikuwa wanaweza kupata mboga mbichi kwa siku tatu kila wiki. Kutokana na kukosa vitamine, askari wengi walipata vidonda midomoni. Kwa sababu ya mazingira yenye unyevunyevu na uchovu wa kazi, askari wengi walipata magonjwa madogo madogo ya aina mbalimbali. Askari hao walikuwa wanaona maumivu viunoni na miguuni mara kwa mara.
Ilikuwa majira ya mvua wakati kikosi kilipofanya ujenzi kwenye sehemu hiyo, ilikuwa kawaida kunyesha mvua mkubwa siku nzima. Askari hao walitumia nafasi zote kufanya ujenzi, hata katika kipindi cha mwaka mpya wa jadi wa China mwaka 2007, askari hao hawakupumzika.
Hali ya usalama wa sehemu hiyo pia ilikuwa na wasiwasi, watu wengi wenye silaha wasiojulikana huwasumbua wakazi wa huko. Watu hao wenye silaha pia walikuwa wanajitokeza karibu na kambi ya ujenzi. Askari waliobeba wajibu wa kulinda kambi walikuwa na macho, watu hao hawakuchukua hatua yoyote.
Ingawa waliishi katika nchi ya kigeni, na mbali sana na jamaa zao, pia mazingira ya huko ilikuwa ngumu sana, lakini askari hao wa China hawakulalamika. Askari mmoja aliwahi kuandika maneno hayo, "tunawakilisha nchi yetu na wananchi wake, tunawakilisha Jeshi la Ukombozi wa Umma la China, sisi ni balozi wa amani, heshima na wajibu wetu umeondoa hali ya upekwe miongoni mwetu."
Baada ya kukamilisha ujenzi wa mradi huo, ofisa mkuu wa sehemu ya tatu ya ujumbe wa Umoja wa Mataifa nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo aliwasifu sana askari wa China kwa ufundi wao hodari, nia ya imara, maadili yao na mchango mkubwa waliotoa.
Tangu kikosi hicho kiwasili sehemu ambapo kilitekeleza jukumu mwezi Agosti mwaka 2006, kukabiliana na mazingira mabaya na matatizo mbalimbali, kilitekeleza majukumu ya ujenzi wa uwanja wa ndege, madaraja, barabara n.k. tarehe 21 mwezi March mwaka huu, askari 218 wa kikosi cha jeshi la kulinda amani la China nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo walipewa nishani ya heshima ya kulinda amani ya Umoja wa Mataifa.
Njia ya safari ya meli ya mizigo kati ya Lianyungang na Bahari ya Sham ya Afrika yafunguliwa
Njia ya safari ya meli ya mizigo kati ya Lianyungang nchini China na bahari nyekundu ya Afrika ilifunguliwa rasmi mwishioni mwa mwezi March, njia hiyo iliendeshwa na kampuni ya uchukuzi kwenye bahari ya mbali ya Nanjing na kampuni ya bandari ya Lianyungang.
Meneja mkuu wa kampuni ya uchukuzi kwenye bahari ya mbali ya Nanjing Bw. Liu Hongliang alijulisha kuwa, katika miaka kadhaa iliyopita, ushirikiano kati ya China na Afrika ulizidi kuimarishwa, mawasiliano ya kiuchumi na kibiashara kati yao yalifanyika mara kwa mara, hasa baada ya mkutano wa wakuu wa baraza la ushirikiano kati ya China na Afrika, mahitaji ya uchukuzi wa mizigo yalizidi siku hadi siku.
Imefahamika kuwa kufunguliwa kwa njia hiyo kutahimiza kukamilishwa kwa soko la uchukuzi wa mizigo la bandari ya Lianyungang, hasa kutahimiza maendeleo ya uchumi wa sehemu ya kati na sehemu ya kaskazini mkoani Jiangsu.
Bw. Liu Hongliang alisema, kampuni ya uchukuzi kwenye bahari ya mbali ya Nanjing itatumia meli yeneye uwezo wa uchukuzi wa toni zaidi ya laki moja, ambayo itakwenda bandari muhimu za Bahari ya Sham na bahari ya Mediterranean mara mbili kila mwezi. Kampuni ya uchukuzi kwenye bahari ya mbali ya Nanjing itatuma meli nyingi zaidi na kupanua njia ya safari kwa bandari nyingi zaidi.
Kampuni ya uchukuzi kwenye bahari ya mbali ya Nanjing ina meli zaidi ya 20 za aina mbalimbali, na uwezo wao wa jumla umefikia tani laki 5. hivi sasa kampuni hiyo imeanzisha njia nyingi za usafiri hadi nchi na sehemu barani Asia, Oceania, Afrika, Ulaya na Amerika.
Idhaa ya kiswahili 2007-04-13
|