Wafanyakazi wa Idhaa ya Kiswahili ya CRI
China Radio International
China
Dunia
(GMT+08:00) 2007-04-18 16:30:19    
Kituo cha Tianjin kinachowasaidia watoto wenye ugonjwa wa kukaa katika hali ya upweke wajiunge na jamii

cri

Watoto wenye ugonjwa wa kukaa katika hali ya upweke hawapendi kuwasiliana na watu wengine, wala hawasikilizi wanayoambiwa. Katika mji wa Tianjin kuna kituo maalum kinachowasaidia watoto wa namna hii kwa njia ya kisayansi waondokane na hali ya upweke na wajiunge na jamii. Mkuu wa kituo hicho Bi. Guo Jianmei si kama tu ni mwanzilishi na mkurugenzi wa kituo hicho, bali pia ni mzazi wa mtoto mwenye ugonjwa wa kukaa katika hali ya upweke. Alisema, mtoto wake Xiao An alithibitishwa kuwa mgonjwa wa kukaa katika hali ya upweke alipokuwa na umri wa miaka mitatu, na kuanzia hapo maisha ya familia yake yalibadilika kabisa. Bi. Guo Jianmei alipaswa kujiuzulu kiwandani ili kumwambatana na mtoto wake kuja Beijing kufanya mazoezi maalum katika kituo pekee cha aina hiyo nchini China. Katika muda huo Bi. Guo Jianmei aliwakuta wazazi wengi wa watoto wenye ugonjwa wa kukaa katika hali ya upweke. Na aliona kuwa upungufu wa vituo vya kuwapa wagonjwa wa namna hiyo mazoezi ili waweze kujiunga na jamii, ni suala linalowasumbua sana wazazi wa watoto wenye ugonjwa wa kukaa katika hali ya upweke. Hivyo Bibi Guo Jianmei aliamua kuanzisha kituo cha kuwasaidia watoto wa aina hiyo wajiunge na jamii mjini Tianjin. Alisema:

"Kutokana na upungufu wa vituo kama hivyo nchini China inawachukua wazazi wa watoto muda mwingi kuwapeleka watoto wao wenye ugonjwa wa kukaa katika hali ya upweke kupata mazoezi ili waweze kujiunga na jamii. Na niliona kuwa si vigumu kujifunza namna ya kuwasaidia watoto hao kufanya mazoezi."

Baada ya kufanya maandalizi kwa muda mrefu, mwezi Agosti mwaka 2003 kituo cha kuwasaidia watoto wenye ugonjwa wa kukaa katika hali ya upweke kujiunga na jamii cha Tianjin kilianzishwa rasmi. Bi. Guo Jianmei alifahamisha kuwa, hivi sasa masomo ya kituo hicho yanawekwa kwa ajili ya watoto wenye umri wa kuanzia miaka 3 hadi miaka 12. Watoto wasiozidi umri wa miaka 6 wanapewa mazoezi ya mmoja kwa mmoja, na wengine wanashiriki katika darasa kwa pamoja.

Kutokana na taabu ya kuthibitisha hali ya ugonjwa wa kukaa katika hali ya upweke, hivi sasa ugonjwa huo bado haujaweza kupatiwa matibabu maalum duniani, mazoezi ya aina mbalimbali yanaweza tu kupunguza hali yao ya kukaa kwenye upweke. Watoto wanaojifungia katika dunia yao ya upweke wanahitaji sana upendo kutoka kwa jamii. Katika miaka ya karibuni idadi ya watu wenye ugonjwa wa kukaa katika hali ya upweke nchini China imekuwa ikiongezeka, hivyo watu wengi zaidi wameanza kufahamu madhara ya ugonjwa huo, na wanajitahidi kuwakaribia watu wenye ugonjwa wa kukaa katika hali ya upweke na kutoa upendo wao.

Licha ya walimu, watu wanaojitolea pia wanaonekana kwenye kituo cha Tianjin cha kuwasaidia watoto hao, wakicheza pamoja na watoto hao. Bw. Zhang Shun mwenye umri wa miaka zaidi ya 20 kwa sasa anafanya kazi ya kuuza nguo, alipofahamu hali ya watoto wenye ugonjwa wa kukaa katika hali ya upweke kila Jumanne na Ijumaa anakwenda mahususi kwenye kituo hicho kucheza pamoja na watoto hao. Alisema:

"Napenda kucheza pamoja na watoto hao, kila ninapoona tabasamu kwenye nyuso zao, mimi mwenyewe hujisikia vizuri sana."

Licha ya watu wanaojitolea, baadhi ya mashirika ya jamii pia yanaonesha upendo wao kwa kukisaidia kituo hicho cha Tianjin zana za kimaisha na vifaa vya kutoa mafunzo kwa watoto ili kiendeshwe bila matatizo.

Idhaa ya kiswahili 2007-04-18