Maonesho ya viwanda ya kimataifa katika mji wa Hanover Ujerumani yalifunguliwa tarehe 16, mashirika zaidi ya 500 ya China yalishiriki kwenye maonesho hayo. Maonesho ya China yanachukua mita za mraba 5,500 ambayo ni makubwa kuliko nchi nyingine isipokuwa tu Italia.
Mada ya maonesho hayo ya kimataifa ni hifadhi ya hali ya hewa na matumizi bora ya nishati. Jumba la maonesho ya nishati katika maonesho ya Hanover ni jumba kubwa duniani na ukumbi wa 11 katika jumba hilo ulikuwa hutumiwa na mashirika ya Siemens, lakini mwaka huu Shirika la Beihaiyinhe la Sayansi na Teknolojia la China ambalo kwa mara ya kwanza lilishiriki kwenye maonesho ya mji huo mwaka jana, mwaka huu liliingia katika ukumbi huo, hii inaonesha nia ya mashirika ya China kuingia kwenye ushindani na mashirika makubwa duniani. Mkuu wa maonesho hayo Bw. Xu Jiaxue alieleza,
"Mwaka jana tulishiriki kwenye maonesho kwa mara ya kwanza, na eneo la maonesho lilikuwa mita za mraba 100, vitu tulivyoonesha vilikuwa ni swichi na vifaa vya kuhakikisha usalama wa umeme ambavyo vyote tulivibuni sisi wenyewe na kupata hakimiliki, tunaridhika na maonesho ya mwaka jana kwa kutangaza chapa ya bidhaa yetu. Mwaka huu tumepanua maeneo ya maonesho kwa lengo la kupata washirika na mawakala wengi."
Maonesho ya Hanover yameshuhudia mabadiliko makubwa ya mashirika ya China yaliyoshiriki katika maonesho hayo. Bidhaa za mashirika mengi zimetoka nje ya China na mashirika hayo yamepanua upeo wa macho na kuona hali ilivyo ya kisasa duniani. Kundi la Jianfeng la mji wa Shenzhen mwaka huu ni mwaka wa tatu kushiriki katika maonesho hayo, na maeneo ya maonesho yanaongezeka kila baada ya mwaka mmoja. Msimamizi mkuu wa teknolojia wa kundi hilo Bw. Zhan Feng alisema,
"Mawazo yangu niliyopata katika maonesho hayo ni kuwa, maonesho ya Hanover kweli ni maonesho makubwa kabisa duniani katika maonesho ya viwanda, kwa hiyo kushiriki katika maonesho hayo sio tu kunasaidia kuimarisha kundi letu na pia kunasaidia kusambaza bidhaa zetu duniani."
Maonesho ya Hanover yanachukuliwa kama ni "mita ya kuashiria hali ya viwanda duniani". Katika siku maonesho yanapofanyika, kuna shughuli mbalimbali zikiwa ni pamoja na "Baraza la Biashara Duniani", "Kutoa Tuzo ya Uvumbuzi wa Bidhaa za Viwanda" ambayo inachukuliwa kama ni tuzo ya Oscar na "Mazungumzo kuhusu Nishati Endelevu Duniani". Huu ni mwaka wa kwanza kwa kundi la bidhaa za Umeme na Elektroniki kushiriki katika maonesho hayo, lengo lake ni kufahamu hali ilivyo ya soko la kimataifa na kutafuta mawakala wa bidhaa zake na kutangaza chapa yake. Naibu meneja mkuu wa kundi hilo Bw. Wu Tianming aliwaambia waandishi wa habari kuwa,
"Kwa kushiriki kwenye maonesho hayo, tumefahamu hali ya mashirika mengi yaliyotangulia duniani ilivyo, bidhaa zao zimekusanya sayansi na teknolojia ya hali ya juu, maonesho hayo ni nadra kuonekana nchini China. Kwa hiyo naona kuwa kushiriki kwenye maonesho hayo kunatusaidia sana kuinua kiwango cha bidhaa za mashirika ya China."
Mashirika kutoka Asia na hasa mashirika ya China yanavutia sana katika maonesho hayo ya kimataifa. Idadi ya mashirika ya China yaliyoshiriki katika maonesho hayo imezidi yale ya Uturuki na kuwa yanavutia sana katika maonesho ya Hanover. Msimamizi mkuu wa teknolojia wa kundi la Jianfeng Bw. Zhan Feng alisema,
"Katika dunia ya leo utandawazi wanapoenea, mashirika mengi ya Ulaya na Marekani yamekuwa yanavutiwa na bidhaa za mashirika ya China. Tunatumai kupitia maonesho hayo kujulisha bidhaa zetu na pia tunatumai kutoa mchango kwa ajili ya kundi letu na pia kwa ajili ya bidhaa za mashirika yote ya China kwa ujumla kujulikana duniani."
Maonesho mazuri ya viwanda ya China pia yamesifiwa na mwenyeji wa kuandaa maonesho hayo. Mmoja kati ya viongozi wa maonesho hayo Bw. Hans Klaus alipodadisiwa na waandishi wa habari alisema, maonesho ya mwaka kesho yataendelea kukaribisha mashirika ya China. Alisema,
"Maendeleo ya uchumi wa China katika miaka mingi mfululizo yameonesha kuwa mwaka 2008 uchumi wa China utakuwa na hali nzuri, na hii inaashiria kwamba mashirika ya China yatashiriki zaidi kwenye maonesho ya Hanover mwaka kesho. Bila shaka sisemi yatashiriki kwenye maonesho ya viwanda tu, bali vile vile kwenye maonesho ya bidhaa za sekta nyingine."
Idhaa ya kiswahili 2007-05-01
|