Kutokana na maendeleo ya teknolojia ya upashanaji wa habari, bidhaa mbalimbali za upashanaji wa habari kama vile kompyuta na simu za mkononi zinatumiwa na watu wengi, na zimekuwa vyombo muhimu kwa kazi na maisha ya watu. Lakini teknolojia nyingi muhimu za bidhaa hizo, hasa teknolojia za CPU zinazoitwa "injini ya bidhaa za upashanaji wa habari", zinadhibitiwa na nchi zilizoendelea za Ulaya na Amerika. Hivi sasa nchi chache tu duniani kama vile Marekani na Japan ambazo zinaweza kutengeneza CPU.
China ilianza utafiti wa kutengeneza CPU ya Loongson mwaka 2001, na kufanikiwa kutengeneza CPU ya Loogson No.1 mwaka 2002. Tukio hilo limekomesha historia kuwa kompyuta zilizotengenezwa na China kutumia CPU zilizotengenezwa na nchi za nje tu. Baada ya hapo, China ilianza kufanya utafiti wa CPU ya Loongson No.2. Hivi sasa CUP ya Loongson No.2E imeanza kuzalishwa kwa wingi na kutolewa kwenye soko la kimataifa kwa kushirikiana na kampuni ya Micro Electronics ya ST ambayo ni kampuni maarufu sana katika sekta hiyo.
Kazi ya utafiti wa CPU za Loongson inayofanywa na taasisi ya teknolojia ya kompyuta katika taasisi ya Sayansi ya China inaungwa mkono na serikali ya China, na fedha zote za utafiti huo zilitolewa na serikali. Taasisi hiyo ilianza utafiti huo mwaka 2005, mkuu wa mradi wa CPU ya Loongson Bw. Hu Weiwu alisema:
"CPU ya Loongson No. 2E inachukua nafasi ya mbele duniani katika usanifu wake, CPU hiyo ni ya kwanza yenye uwezo mkubwa duniani isiyotengenezwa na Marekani na Japan. Kasi yake ya kuhesabu inaweza kufikia mara bilioni 4 kwa sekunde, pia inatumia nishati kidogo zaidi. Hivi sasa CPU hiyo imeanza kuzalishwa na kuuzwa sokoni."
Imefahamika kuwa, ingawa CPU ya Loongson 2E si CPU ya hali ya juu kabisa duniani, lakini imefikia kiwango cha CPU ya aina ya Pentium 4 iliyotengenezwa na Marekani. CPU ya Loongson 2E Ikilinganishwa na Pentium 4, CPU ya Loongson 2E ina bei ya chini zaidi na inatumia nishati kidogo zaidi, hivyo inapendwa na makampuni mengi yanayotengeneza software na kompyuta.
Hivi sasa bidhaa zilizotengenezwa kwa kutumia CPU ya Loongson 2E ni pamoja na kompyuta na mfumo wa kompyuta wa kwenye televisheni na gari. Katika eneo la software, makampuni mashuhuri yakiwemo Microsoft, Xinhua pia yamesaini mkataba kusanifu software husika zinazolingana na CPU hiyo.
Hivi sasa kampuni moja ya China imezalisha kompyuta zenye CPU ya Loongson 2E na kutolewa sokoni nchini China. Bei ya kompyuta ya aina hiyo ni Yuan 1599 tu, na uzito wake ni chini ya kilo moja, ambao ni asilimia 10 tu kuliko ule wa kompyuta wa kawaida, matumizi yake ya nishati pia yanachukua asilimia 20 tu ya yale ya kompyuta ya kawaida. Mkurugenzi mtendaji wa teknolojia wa kampuni ya Zhongkelongmeng ya mkoa wa Jiangsu inayotengeneza kompyuta ya aina hiyo Bw. Hu Mingchang alisema:
"Kompyuta hiyo ina uwezo mkubwa na inauzwa kwa bei nafuu, na inaweza kukidhi mahitaji ya kawaida ya kazi za ofisi na burudani, kama vile kazi ya kuhariri makala, kutuma barua pepe, kuonesha video na kusikiliza audio."
Mkuu wa taasisi ya teknolojia ya kompyuta katika taasisi ya sayansi na teknolojia ya China Bw. Li Guojie aliona kuwa, kufanikiwa kwa utafiti na kutolewa sokoni kwa CPU ya Loongson 2E kunaonesha kuwa China imepata maendeleo makubwa katika teknolojia muhimu ya sekta ya upashanaji habari. Bw. Li Guojie alisema:
"hivi sasa kompyuta ya mezani na kompyuta ya laptop zinalenga kukidhi mahitaji ya watu wenye pato la juu, tunapaswa kutengeneza na kueneza kompyuta kwa watu kwenye pato la chini. Katika siku za baadaye, CPU ya Loongson inaweza kubadilisha muundo wa soko la CPU duniani. CPU ya Loongson itatoa mchango wa kihistoria katika kupunguza gharama za upashanaji wa habari duniani."
Kwa kushirikiana na kampuni ya ST micro electronics, CPU ya Loongson yenye hakimiliki ya China itaenezwa kote duniani. Kwa mujibu wa mkataba kati ya taasisi ya sayansi na teknolojia ya China na kampuni hiyo, kampuni hiyo itawajibika na uzalishaji wa CPU ya Loongson 2E na kuieneza kwenye soko la kimataifa kupitia mtandao wa usambazaji wa kampuni hiyo. Kampuni ya ST micro electronics pia itailipa China mrahaba na sehemu ya pato linalotokana na mauzo ya CPU hiyo. Hii pia ni mara ya kwanza kwa teknolojia ya usanifu wa CPU ya China kutumika kwa kulipwa na kampuni kubwa za nje.
Kampuni ya ST micro electronics ni kampuni maarufu ya bidhaa za upashanaji wa habari duniani ambayo pato lake linaweza kufikia dola za kimarekani bilioni 10 kwa mwaka. Naibu mkuu wa kampuni hiyo Bw. Gianluca Bertino alisema, CPU ya Loongson 2E ina nguvu ya ushindani kutokana na bei nafuu na matumizi madogo ya nishati, ambayo inaweza kusaidiana na bidhaa nyingine za kampuni hiyo. Bw. Bertino alisema:
"Kampuni ya ST micro electronics inafurahi kushirikiana na taasisi ya teknolojia ya kompyuta ya China, tungependa kuzalisha CPU ya Loongson kwa kutumia vifaa na teknolojia zetu. Tunajua mahitaji ya taasisi hiyo, tutakuwa wenzi wazuri wa ushirikiano."
Baada ya Loongson 2E, China itaendelea kuendeleza CPU ya Loongson, mkuu wa mradi wa CPU ya Loongson Bw. Hu Wei alisema:
"Usanifu wa CPU ya Loongson 2F utakamilika hivi karibuni, na inatarajia kutolewa sokoni katika nusu ya pili ya mwaka 2007. Ikilinganishwa na Loongson 2E, Loongson 2F ina uwezo mkubwa zaidi, na matumizi yake ya nishati yamepunguzwa zaidi."
Aidha, China pia itaendeleza CPU ya Loongson No.3, na CPU hiyo itatumika katika server na kompyuta ya hali ya juu.
Idhaa ya kiswahili 2007-05-02
|