Wafanyakazi wa Idhaa ya Kiswahili ya CRI
China Radio International
China
Dunia
(GMT+08:00) 2007-05-16 16:17:47    
Chuo kikuu cha Nankai chafungua mlango kwa wataalamu wa nje

cri

Chuo kikuu cha Nankai ambacho ni chuo kikuu maarufu nchini China hivi karibuni kilifanya sherehe ya kuajiri wataalamu na kuwakabidhi mwaliko wa ajira. Wataalamu hao waliochaguliwa kutoka kote duniani watashika nyadhifa za wakurugenzi wa vitivo vya udaktari, sayansi ya uhai na fizikia. Hii ni mara ya kwanza kwa chuo kikuu hicho chenye historia ya miaka 88 kuchagua wataalamu wa taaluma mbalimbali kutoka kote duniani.

Dk. Xiang Rong ni mmoja wa wataalamu tisa walioalikwa kuwa wakuu wa vitivo katika chuo kikuu hicho. Dk. Xiang Rong mwenye umri wa miaka 48 alipata shahada ya udaktari kuhusud chembechembe katika chuo kikuu cha pili cha udaktari cha Shanghai, kabla ya hapo, alikuwa profesa msaidizi wa mchepuo wa kinga ya mwili katika taasisi ya utafiti ya Scripps kwenye jimbo la California, Marekani. Dk. Xiang Rong alisema,

"nilifanya kazi katika maabara moja nchini Marekani, rafiki yangu mmoja ambaye pia ni profesa wa chuo kikuu chetu aliniambia kuwa, chuo kikuu cha Nankai kinachagua wataalamu kutoka kote duniani, hivyo nilijaza fomu za taarifa binafsi kwenye tovuti ya chuo kikuu hicho, baada ya muda mfupi tu, niliitwa kwenye usaili. Chuo kikuu cha Nankai ni moja ya vyuo maarufu nchini China, na mji wa Tianjin ni moja ya miji muhimu kwenye maendeleo ya China, naona kuwa chuo kikuu cha Nankai ni jukwaa kubwa zaidi ambalo tunaweza kujiendeleza vizuri zaidi."

Chuo kikuu cha Nankai cha Tianjin ni moja ya vyuo vikuu muhimu vya elimu ya jumla nchini China. Chuo kikuu hicho chenye historia ndefu kimeandaa wataalamu wengi akiwemo waziri mkuu wa kwanza wa China mpya marehemu Zhou Enlai, na kimetoa mchango mkubwa kwa ustawi wa taifa la China.

Kwa upande mwengine, chuo kikuu cha Nankai siku zote kinaungana na maendeleo ya mji wa Tianjin. Tianjin ukiwa ni mji mkubwa wa bandari ya kisasa kwenye sehemu ya kaskazini mwa China, utatoa mchango mkubwa zaidi katika maendeleo ya uchumi wa China katika siku za baadaye, hasa eneo jipya la pwani la Tianjin limechukuliwa kuwa moja ya maeneo yaliyowekwa kwenye mpango wa maendeleo na serikali ya China. Ili kukabiliana na fursa hizo za maendeleo, chuo kikuu cha Nankai kimeweka mkazo katika kukusanya wataalamu wa maeneo mbalimbali kutoka kote duniani.

Mkuu wa chuo kikuu hicho Bw. Rao Zihao alieleza, chuo kikuu hicho kilitangaza taarifa ya kuchagua wataalamu kote duniani mwezi Oktoba mwaka 2006 kwa kupitia vyombo vingi vya habari vya nchi za nje, na taarifa hiyo ilifuatiliwa na kuitikiwa na wataalamu wengi duniani.

Katika uandikishaji wa miezi miwili, chuo kikuu hicho kilipata maombi zaidi ya 140 kutoka nchi 14, wataalamu wengi waliotoa maombi wana uzoefu wa kufundisha katika vyuo vikuu maarufu duniani, vikiwemo vyuo vikuu vya Harvard, Oxford, Cambridge na Yale, na wastani wa umri wao ni miaka 45. Mkuu wa chuo kikuu cha Nankai Bw. Rao Zihe alisema:

"wataalamu wengi waliotoa maombi wana uzoefu wa usimamizi na walipata mafanikio makubwa ya kitaaluma, tunaendelea na njia hiyo ya kuajiri wataalamu, hasa wataalamu mabingwa wanaoongoza katika maeneo yao ya utafiti, na wale vijana wenye mustakabali mzuri wenye umri wa chini ya miaka 35."

Maombi 34 kati ya maombi yote 73 yalitoka ng'ambo, mabapo watu wengi waligombea wadhifa wa wakuu wa vivito vya udaktari, elimu ya viumbe, upashanaji wa habari na fizikia, hata kuna nafasi moja iligombewa na watu 18. Dk. Xiang Rong ndiye aliyepata nafasi hiyo kati ya watu hao.

Wakati chuo kikuu hicho kilipochagua wakuu wa idara, baadhi ya watu walikuwa na mashaka kama wakuu walioajiriwa kwa namna hiyo wanaweza kujitolea kwa ajili ya maendeleo ya chuo kikuu. Dk. Xiang Rong alisema:

"nitafanya kilai niwezalo kuendeleza kitivo cha udaktari cha chuo kikuu cha Nankai, tunalenga kuandaa wataalamu mabingwa katika eneo la udaktari. Kwangu mimi binafsi, hili ni tukio muhimu katika maisha yangu. Nitaleta maarifa niliyopata katika nchi za nje kwa chuo kikuu hicho na kutoa mchango kwa ajili ya mambo ya udaktari nchini China."

Dk. Xiang Rong alisema, utafiti wake ni kuhusu kinga dhidi ya saratani na matibabu ya saratani kwa teknolojia ya gene, teknolojia hizo zimeanza kufanyiwa majaribio ya kimatibabu nchini Marekani. Katika muda ambapo Dk. Xiong Rong atafanya kazi katika chuo kikuu cha Naikai, atajitahidi kuunganisha mafanikio ya kitaaluma na majaribio ya kimatibabu.

Mwandishi wetu wa habari alipofanya mahojiano katika chuo kikuu cha Nankai, pia alikutana na wanasayansi wawili waliorudi kutoka Marekani, mmoja ni mkuu wa kitivo cha sayansi ya uhai ambaye alikuwa naibu profesa katika chuo kikuu cha Yale Bw. Yin Zhinan, na mwingine mkuu wa kitivo cha elimu ya dawa ambaye ni profesa wa kudumu katika chuo kikuu cha jimbo la Ohio la Marekani Bw. Wang Peng. Alipozungumzia sababu za kurudi China, profesa Yin Zhinan alisema:

"tulirudi kwa ajili ya fursa ya maendeleo ya Tianjin katika miaka mitano ijayo. China imeweka kituo cha sekta ya udaktari wa viumbe mjini Tianjin, nadhani kwamba fursa hiyo ni muhimu zaidi kwetu."

Kati ya wakuu wapya wa vitivo, mwanafizikia wa Ulaya Bw. Romano Rupp amekuwa mkuu wa kwanza wa kitivo anayetoka nchi ya nje katika chuo kikuu cha Nankai. Kabla ya hapo, Bw. Rupp aliwahi kuwa profesa wa taasisi ya utafiti wa fizikia katika chuo kikuu cha Vienna ambacho ni chuo kikuu maarufu sana nchini Austria. Bw. Rupp alisema, chuo kikuu cha Nankai ni kizuri sana, na anatumai kuwa ataweza kupata maendeleo zaidi ya kitaaluma mjini Tianjin.

Katika muda mfupi ujao, wakuu hao wapya wa vitivo mbalimbali watashika nyadhifa rasmi. Wanaona kuwa mji wa Tianjin unaoendelea kwa kasi umeweka mazingira mazuri ya kuanzisha shughuli zao, chuo kikuu cha Nankai kufungua mlango kwa nje pia kumeonesha uimara wa sekta ya elimu ya juu ya China.