Mfuko wa China unaowasaidia watoto na vijana ulianzishwa mwaka 1981, ni shirika la kwanza nchini China linalowasaidia watoto na vijana kwa njia ya kuchangisha fedha kutoka kwa jamii, lengo la mfuko huo ni kushirikiana na serikali kuwatunza, kuwaandaa na kuwaelimisha watoto na vijana hasa waishio katika sehemu zilizoko nyuma kimaendeleo na sehemu za makabila madogo madogo.
Chini ya uongozi wa baraza la mfuko huo na shirikisho kuu la wanawake la China Mfuko wa China unaowasaidia watoto na vijana umefanya kazi nyingi katika kushughulikia elimu na huduma kwa watoto na vijana, umesifiwa sana na watu wa fani mbalimbali nchini China. Mfuko wa China unaowasaidia watoto na vijana ulikuwa umetenga fedha na kutoa vifaa kwa mara nyingi kuwasaidia watoto waliokumbwa na maafa ya kimaumbile kama vile tetemeko la ardhi, mafuriko ya maji na maafa ya moto, pia kuchangia ujenzi wa shule za msingi, shule za awali, nyumba za watoto yatima, kasri la watoto na vijana na vituo vya kufanya shughuli mbalimbali kwa watoto.
Mwaka 1989 Mfuko wa China unaowasaidia watoto na vijana ulianzisha shughuli za kuwasaidia watoto wa kike wa familia zenye matatizo ya kiuchumi walioacha shule warudi shuleni tena, yaani "Mradi wa Chipukizi", mradi huo ulianzisha "shule za chipukizi" na "darasa la chipukizi la watoto wa kike". Ili kuwawezesha watoto wa kike waliohitimu kutoka "shule ya chipukizi" kujiendeleza kwa ujuzi waliojifunza shuleni, mfuko huo pia ulianzisha "mfuko maalumu wa kutoa mafunzo ya kazi za ufundi kwa watoto wa kike wa mpango wa chipukizi". Ilipofika mwaka 2004 "Mradi wa Chipukizi" ulikuwa umechangisha Yuan milioni 600, fedha hizo zilitumiwa kujenga shule zaidi ya 300 za chipukizi, madarasa 4600 ya chipukizi na kuwasaidia watoto wa kike zaidi ya milioni 1.5 walioacha shule warudi shuleni tena, na kutoa mafunzo ya aina mbalimbali ya kazi za ufundi kwa wanawake na watoto zaidi ya laki 4. "Mradi wa Chipukizi" umekuwa kitu kinachojulikana kwa kila mtu nchini China.
Mwezi Mei mwaka 2000, Mfuko wa China unaowasaidia watoto na vijana ulianzisha mradi mwingine mkubwa wa kutoa huduma kwa jamii nchini China, yaani "Mradi wa Enkon", yaani mradi wa kuwasaidia watoto wakue kwa afya na kwa salama, mradi huo unalenga kuwasaidia watoto wasiache shule, wawe mbali na magonjwa, madhara na uhalifu.
"Mradi wa Enkon" ulikuwa umefanya shughuli nyingi za huduma za kijamii, kama vile kujenga shule, vituo vya afya, darasa la kutoa mafunzo kutoka mbali katika sehemu mbalimbali nchini China, shughuli hizo zimeboresha kwa kiwango kikubwa hali ya kujifunza kwa watoto wa huko. "Mradi wa Enkon" pia ulianzisha mfuko maalumu wa kuwasaidia watoto wenye uwezo hafifu wa kuona mbali, ambapo umewatibu watoto 250 hivi wenye ugonjwa huo.
"Mradi wa Chipukizi" na "Mradi wa Enkon" ni mafanikio ya maendeleo ya haki za binadamu nchini China, umeorodheshwa katika nyaraka za serikali ya China za "Hali ya watoto nchini China", "Hali ya kupunguza umaskini na kujiendeleza nchini China" na "Maendeleo ya haki za binadamu nchini China ya mwaka 2000" na "Muongozo wa maendeleo ya watoto nchini China" kuanzia mwaka 2001 hadi 2010.
Ili kuchangisha fedha nyingi zaidi kwa ajili ya kuwasaidia watoto wenye shida, Mfuko wa China unaowasaidia watoto na vijana pia ulianzisha shughuli za aina mbalimbali kama vile kuweka masanduku ya kuchangisha chenji za hisani, na kuweka "siku ya kutoa hisani kwa watoto".
Idhaa ya kiswahili 2007-05-23
|