Sekta ya elimu ni moja ya sekta ambazo shughuli nyingi zaidi zimefanyika katika ushirikiano na mawasiliano kati ya China bara na Taiwan za mlango bahari wa Taiwan, na shughuli za kutembeleana kwa wasomi na kubadilishana kwa wanafunzi kutoka China bara na Taiwan zimeongezeka siku hadi siku. Kwenye baraza la tatu la uchumi, biashara na utamaduni kati ya pande mbili liliofanyika hivi karibuni hapa Beijing, wataalamu kutoka China bara na Taiwan walijadiliana maoni kuhusu kusukuma mbele mawasiliano na ushirikiano wa elimu kati ya China bara na Taiwan na kufikia maoni ya pamoja kuhusu mambo mengi ya elimu. China bara pia imetangaza kuvikaribisha vyuo vikuu vya Taiwan kuja kuandikisha wanafunzi. Ushirikiano na mawasiliano ya elimu kati ya China bara na Taiwan ndiyo ni njia mwafaka ya kufaidika kwa pamoja busara za ndugu wa pande mbili na kutimiza maendeleo ya pamoja katika siku za baadaye.
Habari kutoka vyombo vya habari vya Taiwan zinasema, takwimu mpya zimeonesha kuwa, asilimia 15 ya wanafunzi wa kidato cha tatu katika shule za sekondari ya juu kisiwani Taiwan wana nia ya kusoma vyuo vikuu katika China bara. Wanafunzi hao wanaona kuwa kusoma katika China bara kunawasaidia kupata mtizamo wa kimataifa na China bara inatoa nafasi nyingi zaidi za kujiendeleza. Wanafunzi kadhaa walipohojiwa na mwandishi wetu wa habari, walisema:
Bw. Xie An alisema: "sasa kisiwani Taiwan kama ukiwaambia wengine kuwa unasoma katika chuo kikuu cha Beijing, wataweza kukupongeza na kueleza matumaini yao ya kusoma mjini Beijing pia."
Bw. Pan Yiyuan alisema: "China bara inatoa nafasi nyingi za ajira, basi wanafunzi wengi wanachagua kubaki na kufanya kazi katika China bara baada ya kuhitimu."
Lakini katika muda mrefu uliopita, shahada zilizotolewa na vyuo vikuu vya China hazitambuliwi kisiwani Taiwan, hali hiyo imewazuia wanafunzi wa Taiwan kusoma katika China bara.
Sauti kubwa za kuzitaka idara za utawala wa Taiwan kutambua shahada zilizotolewa na vyuo vikuu vya China bara zimesikika kwenye baraza hilo.
Mkuu wa chuo kikuu cha Shijian cha Taiwan Bw. Zhang Guangzheng anaona kuwa, kama idara ya utawala ya Taiwan ikiweza kutambua shahada za vyuo vikuu vya China bara, italeta manufaa mengi kwa wanafunzi wa Taiwan. Bw. Zhang Guangzheng alisema:
"ninawaunga mkono wanafunzi wa Taiwan kusoma katika China bara, kwani inaweza kuwasaidia wanafunzi na wasomi wa Taiwan kufahamu kwa kina kuhusu hali halisi ya China bara. Hali hii inaweza kuongeza maoni ya pamoja kuhusu utamaduni wa taifa la China, na pia inaweza kuendeleza uwezo wa kufikiri na kuamua kwa kujitegemea, pia inaweza kutatua suala la elimu kwa watoto wa wafanyabiashara wa Taiwan wanaofanya shughuli katika China bara. Hali hii pia inaleta ushindani na kuhimiza maendeleo ya vyuo vikuu na idara mbalimbali za utafiti. "
Katika miaka ya hivi karibuni, serikali ya China imetoa sera mbalimbali za kuwapa urahisi wanafunzi wa Taiwan kusoma na kupata ajira katika China bara, shahada za vyuo vikuu vya Taiwan vilivyoidhinishwa na idara ya usimamizi wa elimu ya Taiwan zimetambuliwa katika China bara. Wanafunzi wa Taiwan wanapokewa sawasawa kama wanafunzi wa China bara katika masuala ya ada za shule na mabweni, wanafunzi hao pia wana fursa ya kupewa misaada ya masomo. Katika mwaka jana tu, wanafunzi zaidi ya 1700 wa Taiwan walipewa miaada ya masomo zaidi ya yuan milioni 7, kiasi hiki kinachukua robo ya kile cha wanafunzi wote wa Taiwan wanaosoma katika China bara.
Lakini pamoja na wanafunzi wengi kusoma katika vyuo vikuu vya China bara, wanafunzi wachache tu wa China bara ambao wanaweza kusoma kisiwani Taiwan. Hali hiyo inatokana na kuwa wanafunzi wa China bara wanaoenda kusoma katika vyuo vikuu vya Taiwan wanaruhusiwa kushiriki kwenye mafunzo ya muda mfupi usiozidi miezi minne tu, wala hawaruhusiwi kusoma shahada kisiwani Taiwan.
Mjumbe wa chama cha Guoming Bw. Zhou Shouxun anaona, kama idara ya utawala ya Taiwan ikifungua mlango kwa wanafunzi wa China bara, itasaidia kutatua hali ya upungufu wa wanafunzi wa vyuo vikuu kisiwani Taiwan.
Elimu na ajira siku zote ni masuala yanayoungana. Hivi sasa, wanafunzi wa vyuo vikuu vya Taiwan hawana vizuizi vyovyote vya kupata ajira katika China bara, huduma wanazipewa pia zinaongezeka, vilevile wanaweza kunufaika na bima za huduma za jamii kama walivyo pale wakazi wa China bara.
Kwenye kongamano hilo la uchumi, biashara na utamaduni kati ya China bara na Taiwan za mlango bahari wa Taiwan, idara ya usimamizi wa nguvukazi ya China bara imetangaza kuwa, mitihani ya kupata sifa ya mafundi ya taaluma15 zikiwemo uhasibu na ukalimani imeshafunguliwa rasmi kwa wakazi wa Taiwan. Imefahamika kuwa, mafundi wa Taiwan wanaotimiza masharti wanaweza kutoa maombi kwa idara husika za usimamizi za kila mkoa, sehemu inayojiendesha na mji unaotawaliwa moja kwa moja ya serikali kuu ya China.
Mkuu wa chuo kikuu cha Mingchuan cha Taiwan Bw. Li Quan anaona kuwa, China bara imekuwa soko jipya la ajira kwa wanafunzi wa Taiwan, katika hali hiyo, ushirikiano wa elimu kati ya China bara na Taiwan za mlango bahari wa Taiwan unapaswa kupanuliwa kwa kina zaidi. Bw. Li alisema:
"walimu wa China bara na Taiwan wanaweza kufundisha na kuwaelekeza wanafunzi kwa pamoja, pia wanaweza kushirikiana katika utafiti. Mbali na hayo, tunaweza kushirikiana katika kutoa mafunzo katika nchi za nje. Hali hiyo itasaidia kuinua kwa pamoja sifa za elimu katika vyuo vikuu vya China bara na Taiwan."
|