Wafanyakazi wa Idhaa ya Kiswahili ya CRI
China Radio International
China
Dunia
(GMT+08:00) 2007-06-04 14:54:40    
Michezo ya sanaa ya China inavutia zaidi katika Tamasha la "Kukutana Mjini Beijing"

cri

Tokea mwisho wa mwezi Aprili Tamasha la "Kukutana Mjini Beijing" lianzishwe, vikundi vya sanaa zaidi ya 40 kutoka nchi 20 vimeshiriki kwenye tamasha hilo. Michezo ya sanaa ya China ni sehemu muhimu katika tamasha hilo.

Muziki uliopigwa katika ufunguzi wa tamasha hilo unaeleza jinsi kabila la wafugaji la Wamongolia nchini China lilivyoanza na kuimarika katika historia yake ndefu kwa kuonesha sherehe ya tambiko, vita vikali, maisha ya wafugaji na mandhari nzuri ya malisho.

China ni nchi yenye historia ya kuandikwa kwa miaka elfu tano, Wachina wamevumbua aina za nyimbo na ngoma kwa kueleza mambo, na katika Enzi ya Han, miaka 200 iliyopita, nyimbo na ngoma za kueleza mambo zilifikia ngazi ya juu, na zimeweka msingi wa maendeleo ya dansi ya kale ya Kichina. Katika tamasha la "Kukutana Mjini Beijing" mchezo wa nyimbo na ngoma uitwao "Dhuruba" umetungwa kwa mujibu wa nyimbo na ngoma za kale za China, ukionesha vurugu za mabadiliko ya enzi katika historia ya China.

Mchezo wa dansi na muziki unaonesha jinsi mfalme wa Enzi ya Han alivyokumbwa na hali ngumu katika miaka yake ya kuiunganisha China na kuanzisha enzi yake. Muziki mara unahuzunisha mara unashupaza ukieleza hisia za furaha na huzuni za mfalme huyo. Muziki ulipigwa kwa ala za jadi za China, ambao watazamaji wanajikuta wako katika mazingira ya utamaduni wa kale wa China. Mwongozaji wa mchezo huo Bw. Xu Rui alisema,

"Tulifanya juhudi nyingi kuandaa mchezo huo, kuhusu vitendo vya ngoma tulifanya utafiti kwa miaka karibu 50 kutoka katika vitabu mbalimbali vya zamani. Mchezo huo licha ya kuonesha utamaduni mkubwa wa kale wa China unawakumbusha Wachina shina la utamaduni wao na kuwafanya wathamini utamaduni huo, kwa hiyo licha ya kuvutia unafundisha."

Muziki wa piano pia ni moja ya michezo ya sanaa katika tamasha hilo, mpigaji mashuhuri wa piano wa China Bw. Li Ang alifanya maonesho ya muziki peke yake. Miaka ya karibuni wapigaji vijana wa piano wa China wameibuka wengi na wanasifiwa sana katika maonesho ya kimataifa, Bw. Li Ang ni mmojawao. Bw. Li Ang aliona furaha ya kuweza kufanya maonesho yake ya muziki wa piano katika tamasha hilo. Piano ni ala ya muziki ya nchi za magharibi, lakini alipokaribishwa kupiga tena muziki wake, kwa makusudi alipiga muziki uliohaririwa kutoka nyimbo za China. Alisema,

"Nilikaribishwa kupiga tena muziki, kwa makusudi nilipiga muziki uliohaririwa kutoka nyimbo za China. Muziki huo wa nyimbo mbili niliupiga mara nyingi katika nchi za nje. Mwishoni mwa mwezi Aprili nilipiga muziki huo katika maonesho yangu ya muziki nchini Marekani, wasikilizaji waliufurahia sana."

Katika siku za tamasha la "Kukutana Mjini Beijing", michezo ya sanaa ya kienyeji nchini China pia ilivutia sana. Mwimbaji wa mkoa wa Xinjiang aitwaye Maila ana mikataba ya kushiriki maonesho ya opera na majumba kadhaa ya michezo ya sanaa ya nchi za nje, kwa hiyo mara nyingi aliimba katika opera maarufu iitwayo "the Lady of the Camellias". Katika siku za tamasha la "Kukutana Mjini Beijing" aliimba wimbo mmoja ambao jina la wimbo huo ni sawa na jina lake mwenyewe, Maila. Alisema,

"Wimbo huu unasema, 'Mimi naitwa Maila, watu wanasema mimi ni mwimbaji Maila na mshairi Maila, meno yangu meupe pepepe na sauti yangu tamu kama asali'. Nilipokuwa mtoto niliimba wimbo huo mara kwa mara. Mama yangu pia ni mwimbaji, na katika maonesho ya muziki wake kila mara aliimba wimbo huo, kwa hiyo nimekua kwa kusikiliza wimbo huo, baada ya mimi kuwa mkubwa, naimba wimbo huo vile vile kama mama yangu."