Wafanyakazi wa Idhaa ya Kiswahili ya CRI
China Radio International
China
Dunia
(GMT+08:00) 2007-06-13 10:41:27    
China yaanzisha mpango wa taifa wa uungaji mkono wa sayansi na teknolojia

cri

Hivi karibuni, China ilianzisha mpango mpya wa taifa wa sayansi na teknolojia ili kuinua kikamilifu uungaji mkono wa sayansi na teknolojia kwa maendeleo ya uchumi na jamii ya China.

Mpango huo unaoitwa mpango wa taifa wa uungaji mkono wa sayansi na teknolojia umetekelezwa kuanzia mwezi Februari mwaka huu, na unakadiriwa kugharamu yuan bilioni 30. serikali ya China inataka kutatua hatua kwa hatua matatizo ya nishati, raslimali na mazingira yanayozuia maendeleo ya uchumi na jamii katika miaka kadhaa ijayo na kuinua kikamilifu kiwango cha sayansi na teknolojia katika sekta ya huduma za umma. Mjumbe wa taifa wa China Bi. Chen Zhili alisema:

"kuweka na kutekeleza mpango huo kunahudumia moja kwa moja shughuli za ujenzi wa uchumi na maendeleo ya jamii. China inalenga kupata maendeleo katika teknolojia muhimu zinazotumika katika sekta mbalimbali, kupata mafanikio ya teknolojia yenye hakimiliki ya ubunifu, kuandaa makampuni yenya nguvu ya ushindani duniani, na kuondoa vizuizi vya maendeleo ya uchumi na jamii."

Imefahamika kuwa, mpango huo unatokana na mpango wa zamani wa maendeleo ya sayansi na teknolojia. Tangu mpango wa maendeleo ya sayansi na teknolojia uanze kutekelezwa miaka ya 80 ya karne iliyopita, China imepata maendeleo katika teknolojia muhimu za sekta mbalimbali, zikiwemo teknolojia za mpunga chotara, mradi wa magenge matatu, na kituo cha kuzalisha umeme kwa nishati ya nyuklia cha Qinshan, mafanikio hayo yameshaleta manufaa makubwa ya kiuchumi na kijamii.

Hivi sasa China imeingia kwenye kipindi kipya cha maendeleo, sekta mbalimbali zikiwemo nishati, raslimali, mazingira, kinga na tiba ya magonjwa, nguvu ya ushindani ya viwanda na usalama wa umma, zote zinakabiliwa na changamoto kubwa, na mpango ule wa zamani hauwezi kukidhi mahitaji ya hivi sasa.

Kutokana na hali hiyo, China iliweka mpango wa uungaji mkono wa sayansi na teknolojia kwenye msingi wa mpango wa zamani, ili kukusanya raslimali za sayansi na teknolojia kote nchini China kwa ajili ya kuunga mkono maendeleo ya uchumi na jamii. Mkurugenzi wa idara ya mpango wa maendeleo katika wizara ya sayansi na teknolojia ya China Bw. Wang Xiaofang alisema, mpango huo unaohusisha sekta 11 zikiwemo kilimo na shguhuli za utengenezaji, utatoa uungaji mkono kwa miradi 350. hivi saa kundi la kwanza la miradi hiyo kimethibitishwa. Bw. Wang Xiaofang alisema:

"miradi 147 imethibitishwa na itatekelezwa kwanza, na serikali imetenga yuan bilioni 7.35 kwa ajili ya miradi hiyo. Fedha hizo zinatarajiwa kuvutia vitega uchumi zaidi ya mara mbili kutoka kwa makampuni na idara husika."

Mashine ya kitarakimu ya upimaji wa magonjwa kwa Supersonic inayosanifiwa na Kampuni ya teknolojia ya kitarakimu ya Tianhuihua ya Beijing imechukuliwa kuwa moja kati ya miradi ya mpango huo itakayotekelezwa kwanza.

Ofisa wa kampuni hiyo Bw. Shen Jianlei alisema, utafiti wa vifaa kama hiyo utagharamia zaidi ya yuan milioni 10, uwekezaji mkubwa namna hii una hatari kubwa kwa kampuni hiyo ya wastani. Lakini kutokana na mradi huo kuchukuliwa kwenye mpango wa taifa, umekuwa shughuli ya taifa wala si ya kampuni hiyo peke yake. Bw. Shen Jianlei alisema:

"mpango huo wa taifa umetenga fedha yuan milioni tatu, kampuni peke yake inatoa yuan milioni 3. kutokana na kukabidhiwa kazi ya utafiti wa mradi huo, tunaweza kuvutia vitega uchumi zaidi ya mara kumi kutoka kwa jamii. Mpango huo unaweza kuhamasisha na kuelekeza kwa ufanisi uwekezaji wa jamii."

Mpango wa uungaji mkono wa sayansi na teknolojia pia unaweka mkazo katika sekta ya raslimali. Kwa mujibu wa mpango huo, ifikapo mwaka 2010, China itagundua vituo vitatu na vinne vya akiba ya madini, asilimia 80 ya maji yanayotumika katika shughuli za viwanda yatatumiwa tena, na China pia inatazamiwa kupata maendeleo katika teknolojia ya matumizi ya maji ya bahari,

Aidha, miradi ya utafiti inayohusika na maisha ya wananchi kama vile huduma za afya na mawasiliano barabarani pia inatiliwa maanani katika mpango huo. Katika kituo cha usimamizi na uongozi wa mawasiliano ya barabarani cha Beijing, mfumo wa kisasa wa usimamizi wa mawasiliano barabarani unaotolewa na mpango huo umeshatumika. Mfumo huo unaweza kuonesha moja kwa moja hali ya mawasiliano barabarani ndani ya mzunguko wa tano wa Beijing. Takwimu husika zimeonesha, matumizi ya mfumo huo yameongeza ufanisi wa mawasiliano barabarani kwa asilimia 12.

Ofisa wa kituo hicho Bw. Wu Xianli alisema,

"baada ya kutumia mfumo huo, kwa wastani polisi wanaweza kufika mahali palipotokea ajali ndani ya dakika 3.6, lakini zamani walichukua zaidi ya dakika 10 hata 20."

Mbali na hayo, mawasiliano kwa teknolojia ya magnetic levitation pia yamethibitishwa kuwa ni mradi muhimu katika sekta ya mawasiliano na uchukuzi. China inapanga kuweza kuanzisha mfumo wa udhibiti wa mawasiliano ya kasi yanayotumia teknolojia ya magnetic levitation ndani ya miaka kadhaa ijayo, na kufanya utafiti wa treni inayotumia teknolojia hiyo yenye mwendo kasi wa kilomita 500 kwa saa.

Wachambuzi wa sekta ya sanyansi na teknolojia wanaona kuw,a kutokana na kutekelezwa hatua kwa hatua kwa mapngo wa taifa wa uungaji mkono wa sayansi na teknolojia, uwezo wa sayansi na teknolojia kuunga mkono maendeleo ya uchumi na jamii utainuka kikamilifu.