Mahitaji
Mizizi ya yungiyungi gramu 50, figili gramu 50, njegere gramu 50, karoti gramu 50, chumvi vijiko viwili, chembechembe za kukoleza ladha kijiko kimoja, sukari kijiko kimoja, vipande vya vitunguu maji na tangawizi gramu 5
Njia
1. ondoa magamba ya mizizi ya yungiyungi, halafu ikate iwe vipande vipande.
2. katakata karoti na figili ziwe vipande vipande.
3. washa moto na mimina maji kwenye sufuria, baada ya maji kuchemka, tia vipande vya mizizi ya yungiyungi kwenye sufuria, korogakoroga kwa haraka halafu vipakue. Baada ya hapo tia vipande vya figili kwenye sufuria na kisha korogakoroga kwa haraka na vipakue.
4. washa moto tena tia mafuta kwenye sufuria, tia vipande vya vitunguu maji na tangawizi korogakoroga, kisha tia vipande vya karoti na figili korogakoroga, halafu tia vipande vya mizizi ya yungiyungi na njegere korogakoroga, baada ya hapo tia chumvi, chembechembe za kukoleza ladha na sukari, halafu korogakoroga halafu ipakue. Mpaka hapo kitoweo hiki kiko tayari kuliwa.
|