Baraza la mashauriano ya kisiasa la China ni baraza muhimu la kufanya ushirikiano wa vyama vingi na mashauriano ya kisiasa chini ya uongozi wa Chama cha kikomunisti cha China, ambapo wajumbe wa baraza hilo wanaweza kuenzi demokrasia ya ujamaa katika maisha ya kisiasa nchini China. Kutetea mshikamano na demokrasia ni nia na kanuni za baraza hilo. Nchini China mbali na Chama cha kikomunnisti cha China, pia kuna vyama vinane vya kidemokrasia, chama cha wasomi cha Jiusan ni moja kati ya vyama hivyo. Wanachama wake ni wasomi wa kiwango cha juu na wastani wanaoshughulikia mambo ya sayansi na teknolojia, utamaduni na elimu pamoja na afya. Leo tunawaelezea kuhusu wajumbe watatu wanawake wa chama hicho.
Mjumbe wa baraza la mashauriano ya kisiasa la China Bibi. Xie Lijuan ni naibu mwenyekiti wa baraza la mashauriano ya kisiasa la Shanghai. Tangu miaka 80 hadi miaka 90 ya karne iliyopita, Bibi Xie Lijuan aliwahi kuwa naibu meya wa mji wa Shanghai. Katika kipindi cha kushika madaraka hayo, Bibi. Xie Lijuan siku zote alitoa kipamubele kwa mambo yanayohusu maisha ya wakazi. Mwanzoni mwa miaka ya 90 ya karne iliyopita, kutokana na juhudi zake, Shanghai ilitoa hatua za bima ya matibabu kwa wanafunzi. Baada ya kuanza kutekelezwa kwa hatua hizo, wanafunzi kati ya 50,000 na 60,000 wananufaika kila mwaka.
Sasa Bibi Xie Lijuan siyo tena naibu meya wa Shanghai, lakini akiwa mjumbe wa baraza la mashauriano ya kisiasa la China, bado anaendelea kutoa maoni na mapendekezo kwa ajili ya ujenzi wa jamii yenye masikilizano. Alisema:
"Miaka kumi iliyopita, nilitoa pendekezo kuhusu kutowafanya watoto wa wakulima wanaofanya kazi za vibarua mijini wasijue kusoma na kuandika katika karne mpya, baadaye nilipata jibu kutoka kwa wizara ya elimu, ilisema itafanya utafiti kuhusu suala hilo halafu itatoa mpango wa kulitatua. Mwanzoni mwa mwaka 2004, serikali ya China ilitoa uamuzi mpya kuhusu kuhakikisha watoto wa wakulima wanaofanya kazi za vibarua mijini wanapata elimu ya lazima kote nchini, wajumbe wote wa baraza la mashauriano ya kisiasa la China pia wanahimiza utekelezaji wa uamuzi huo.
Bibi Xie anafurahia kuwa, katika miaka ya hivi karibuni kutokana na uungaji mkono wa sera husika zilizotolewa na serikali ya China na kushiriki kwa sekta mbalimbali za jamii, suala la elimu ya watoto wa wakulima wanaofanya kazi za vibarua mijini limetatuliwa hatua kwa hatua. Katika ufunguzi wa mkutano wa mwaka wa bunge la umma la China wa tarehe 5 mwezi Machi mwaka huu, waziri mkuu wa China Bw. Wen Jiabao alisema China itatenga fedha zaidi kwa elimu ya lazima vijijini ili kuwawezesha watoto wote wapate nafasi ya kwenda shule.
Mjumbe wa baraza la mashauriano ya kisiasa la China Bibi Li Huizhen ni naibu mwenyekiti wa baraza la mashauriano ya kisiasa mkoani Jilin, yeye ni mtaalamu wa utengenezaji wa mashine, hivyo anatilia maanani fedha za kununua mashine na utumiaji wa mashine. Katika miaka ya karibuni China ilinunua mashine mengi lakini mashine kadhaa hazikutumika vizuri na hata zilipata kutu. Bibi Li ana wasiwasi sana, alisema: "
"Mwaka 2005 nilijulisha suala hilo katika mkutano wa wajumbe wa kudumu wa baraza la mashauriano ya kisiasa la China, naibu katibu mkuu wa baraza la serikali ya China Bw. Wang Yang aliitisha mkutano kuhusu suala hilo ili kushughulikia maslahi ya pande mbalimbali, baada ya nusu mwaka kampuni ya usambazaji wa bidhaa ya Hua Liang ikaanzishwa na mashine hizo zilianza kufanya kazi.
Bibi Lu Guangxiu ni naibu mwenyekiti wa baraza la mashauriano ya kisiasa mkoani Hunan ambaye ni mtaalamu katika sekta ya kinga na tiba ya magonjwa nchini China. Katika miaka 90 karne iliyopita, Bibi Lu Guangxiu alitoa mchango mkubwa katika kueneza matumizi ya chumvi yenye madini ya joto katika bara la China. Tangu mwaka 1989 hadi mwaka 1993, Bibi Lu Guangxiu aliongoza kikundi cha matibabu kufanya uchunguzi kwenye kijiji chenye watu wasio na akili timamu magharibi mwa mkoa wa Hunan, baada ya uchunguzi wa miaka kadhaa, aligundua kuwa upungufu wa madini ya joto kwenye sehemu za China bara ulisababisha watu kwenye kijiji hicho kutokuwa na akili timamu. Ripoti hiyo ilitiliwa maanani baada ya kuwasilishwa kwa serikali, na baadaye matumizi ya chumvi yenye madini ya joto yalianza kuenezwa.
Mwaka huu Bibi Lu alitoa pendekezo kuhusu kuongeza nguvu ya kukinga na kutibu magonjwa yanayoweza kutokea kazini, alisema: "
"Ndani ya migodi, magonjwa yaliyotokea wakati wa kazi hayatiliwi maanani, wafanyakazi wanaochimba madini wanapata ugonjwa wa kifua kikuu baada ya kufanya kazi kwa miaka miwili au mitatu migodini. Lakini wakuu wa makampuni hayo walizingatia maslahi yao tu, hawakutekeleza wajibu wao kwa jamii. Wengi wa wafanyakazi wa migodini ni watu wenye matatizo ya kiuchumi, na hawakujua namna ya kulinda maslahi yao. Suala hilo linapaswa kufuatiliwa zaidi.
Wajumbe wanawake ni wachache miongoni mwa wajumbe wa baraza la mashauriano ya kisiasa la China, lakini sura yao inawavutia watu zaidi. Naibu mwenyekiti wa baraza la mashauriano ya kisasa mkoani Jilin Bibi Li Huizhen alipozungumzia umaalum wa wajumbe hao wanawake alisema: "
"Naona wanawake wako makini zaidi na wana huruma zaidi, na wanatilia maanani zaidi watu wadhaifu.
Wajumbe hao wanawake walisema katika miaka kadhaa iliyopita baada ya kuchaguliwa kuwa wajumbe wa baraza la mashauriano ya kisiasa la China, walifanya kazi chache tu nyumbani kwao lakini walipanua upeo wao, kuongeza uwezo wa kuzingatia masuala na kuelewa wananchi zaidi. Walimwambia mwandishi wa habari kuwa, familia zao zinawaunga mkono, hivyo wanaweza kufanya kazi zao bila kuwa na wasiwasi na familia zao.
|