Mahitaji
Vipande vya nyama ya kuku gramu 200, karoti moja, figili gramu 50, chembechembe za kukoleza ladha kijiko kimoja, mvinyo wa kupikia vijiko viwili, chumvi vijiko viwili, wanga bakuli moja, pilipili hoho gramu 2, vipande vya vitunguu maji gramu 5, wanga wa pilipili manga vijiko viwili
Njia
1. kata karoti na figili ziwe vipande vipande, halafu washa moto na mimina maji kwenye sufuria baada ya kuchemka, tia vipande vya karoti ndani ya sufuria, korogakoroga halafu vipakue, baada ya hapo tia vipande vya figili kwenye sufuria korogakoroga halafu vipakue.
2. koroga vipande vya nyama ya kuku pamoja na mvinyo wa kupikia, wanga wa pilipili manga, chumvi na chembechembe za kukoleza ladha.
3.mimina maji kidogo pamoja na nyama ya kuku, halafu weka vipande vya nyama ya kuku ndani ya wanga, kasha washa moto tena, na mimina mafuta kwenye sufuria, baada ya hapo tia vipande vya nyama ya kuku kwenye sufuria na vikaange, mpaka viwe rangi ya hudhurungi kasha vipakue.
4. washa moto tena, mimina mafuta kidogo kwenye sufuria, halafu tia pilipili hoho, korogakoroga, halafu tia vipande vya karoti, figili na vipande vya nyama ya kuku, korogakoroga, kasha tia chumvi, chembechembe za kukoleza ladha, wanga wa pilipili manga, vipande vya vitunguu maji, korogakoroga na ipakue. Mpaka hapo kitoweo hiki kiko tayari kuliwa.
|