Wafanyakazi wa Idhaa ya Kiswahili ya CRI
China Radio International
China
Dunia
(GMT+08:00) 2007-06-22 11:42:49    
Wiki ya filamu za China nchini Mauritius

cri
Ili kuadhinisha miaka 35 tangu China na Mauritius zianzishe uhusiano wa kibalozi, wizara ya utamaduni na sanaa ya Mauritius na ubalozi wa China nchini Mauritius hivi karibuni huko Port Louis, mji mkuu wa nchi hiyo zilifanya shughuli za wiki ya filamu za China.

Kwenye ufunguzi wa shughuli hiyo, waziri wa utamaduni na sanaa wa Mauritius Bw. Motee Ramdass alisema, kufanikiwa kuandaa wiki ya filamu za China ni jambo muhimu katika mawasiliano na ushirikiano kati ya sekta za utamaduni na sanaa za nchi hizo mbili, na filamu za China zenye umaalumu hakika zitaimarisha maelewano ya wananchi wa Mauritius kwa wananchi wa China.

Naibu mkurugenzi wa shirika kuu la radio, televisheni na filamu la China Bw. Zhao Shi alijulisha historia ya maendeleo na hali ya sasa ya filamu za China, pia alionesha matakwa ya sekta ya utamaduni na sanaa ya China kuhusu kutaka kuimarisha mawasiliano na ushirikiano na sekta ya utamduni na sanaa ya Mauritius.

Ehiopia ni nchi kubwa inayozalisha kahawa kwa wingi kabisa barani Afrika, hivi sasa inapanga kuanzisha kituo cha biashara kwenye mtandao wa internet ili kuhimiza biashara za mazao yake muhimu ya kilimo.

Mkurugenzi wa mradi wa kituo cha biashara za bidhaa kwenye mtandao wa internet alisema, kituo hicho kitazinduliwa kuanzia mwishoni mwa mwaka huu, mazao ya biashara ni ya aina 6 yakiwemo kahawa, ufuta na mahindi.

Mkurugenzi huyo alisema, baada ya kazi zianze kama kawaida, kituo hicho huenda kitaanzisha mawasiliano na vituo vya biashara vya nchi za nje ikiwemo China. Hivi sasa China ni nchi inayoagiza ufuta kwa wingi zaidi kutoka nchini Ethiopia.

Takwimu zinaonesha kuwa, ikiwa nchi inayozalisha kahawa kwa wingi kabisa barani Afrika, kuanzia mwaka 2005 hadi 2006, Ethiopia iliuza kahawa tani laki 1.83 zenye thamani ya dola za kimarekani milioni 427 katika nchi za nje.

Maonesho ya 12 ya kimataifa ya magari na vipuri vya magari ya nchi za kiafrika na kiarabu hivi karibuni yalifunguliwa kwenye kituo cha maonesho ya kimataifa huko Cairo, mji mkuu wa Misri, magari ya aina mbalimbali yaliyotengenezwa na viwanda vya magari vya China yalioneshwa kwenye maonesho hayo.

Kwenye maonesho hayo, meneja wa uuzaji wa kampuni ya magari ya Biyadi Bw. Li Changsheng aliwaambia waandishi wa habari kuwa, katika miaka kadhaa iliyopita, magari yaliyotengenezwa na China yaliingia kwenye masoko ya mashariki ya kati na Afrika ya kaskazini, na uuzaji wa magari hayo kwenye soko uliongezeka siku hadi siku. Kampuni ya Biyadi ilileta magari ya F3, Flyer kwenye maonesho hayo.

Wakala mmoja wa uuzaji wa magari wa huko alisema, magari yaliyotengenezwa na China yanakaribishwa sana nchini Misri, kwa sababu bei ya magari ya China ina nguvu za ushindani. Kampuni anayofanya kazi ni wakala wa uuzaji wa magari ya "Cherry" ya China, bei ya gari la QQ ni pauni za Kimisri elfu 46.9 tu.

Maonesho ya kimataifa ya magari na vipuri vya magari ya Afrika na kiarabu yanafanyika kila mwezi June huko Cairo, hivi sasa yamekuwa maonesho muhimu ya kimataifa ya magari kwenye sehemu ya mashariki ya kati na Afrika ya kaskazini.

Mfumo wa mobile wa kwanza uliotumia tekenolojia ya 3G nchini Zimbabwe mwezi June ulianza kutumika rasmi, mfumo huo ulijengwa na kampuni ya Huawei ya China na kampuni ya Telone ya Zimbabwe.

Waziri wa mawasiliano ya habari na telekom wa Zimbabwe Bw. Moshowi kwenye sherehe ya kuzinduliwa kwa mfumo huo alisema, kampuni ya Telone ni mojawapo ya kampuni kubwa zinazoshughulikia mfumo wa telekom barani Afrika. Mfumo huo mpya uliowekezwa dola za kimarekani milioni 456 utapunguza zaidi pengo kati ya miji na vijiji, na kukidhi mahitaji ya wakazi wa huko ya kuwasiliana na mtandano wa Internet na mtandao wa mobile.

Balozi wa China nchini Zimbabwe Bw. Yuan Nansheng alisema, hivi sasa ujenzi wa miundo mbinu nchini Zimbabwe unakabiliwa na shinikizo kubwa, tekenolojia hiyo mpya itawafanya wazimbabwe wengi zaidi waweze kuitumia. Alieleza imani yake kuwa miradi mingi zaidi ya ushirikiano kati ya China na Zimbabwe itaanzishwa nchini Zimbabwe, na kuwanufaisha wananchi wa Zimbabwe.

Bw. Yuan Nansheng vilevile alisema, serikali ya China iliahidi kutoa misaada kwa Zimbabwe kadri iwezekanayo, ikiwemo misaada ya tekenolojia. Alisema China na Zimbabwe zina mustakabali mzuri wa ushirikiano katika sekta ya sayansi na tekenolojia.

Chuo kikuu cha Tshwane cha Afrika ya Kusini na ofisi ya mafunzo ya lugha ya Kichina ya China tarehe 14 zilisaini makubaliano ya kuanzisha pamoja chuo cha Confucius, chuo hicho kinatazamiwa kuanzishwa rasmi mwezi Septemba mwaka huu, na kitakuwa chuo cha pili cha Confucius nchini Afrika ya Kusini.

Ujumbe wa wizara ya elimu ya China ulioongozwa na naibu waziri wa elimu wa China Bw. Yuan Guiren na wakurugenzi wa chuo kikuu cha Tshwane cha Afrika ya Kusini walihudhuria sherehe ya kusaini makubaliano. Bw. Yuan Guiren alisema, chuo kikuu cha Tshwane cha Afrika ya kusini ni chuo kikuu cha kwanza kilichofanya mawasiliano ya taaluma na China. Alieleza matumaini kuwa vyuo vya Confucius vya nchi hiyo vinaweza kuwa mfano wa kuigwa miongoni mwa vyuo zaidi ya 100 vya Confucius duniani.

Ofisa wa ofisi ya elimu ya ubalozi wa China nchini Afrika ya kusini alisema, China itatoa dola za kimarekani laki moja na vitabu vya mafunzo, pia kuwatuma walimu wawili au watatu wa China kwenye chuo hicho. Hivi sasa wanafunzi zaidi ya 50 wameandikisha na kutaka kujifunza lugha ya Kichina.  

Mashindano ya nne ya "daraja la lugha ya Kichina" yalifanyika tarehe 14 kwenye chuo cha uhusiano wa kimataifa katika chuo kikuu cha pili cha Yaounde nchini Cameroon.

Wapenzi tisa wa lugha ya Kichina walishiriki kwenye mashindano hayo. Wale waliopata fursa ya kuja China walieleza upendo wao kwa China, na wale wanaotarajia kuja China walieleza matumaini yao ya kujifunza utamaduni wa China.

Hotuba walizotoa kwa Kichina zilisifiwa na wajumbe wa uchaguzi, na maonesho yao ya michezo ya sanaa ya kuimba nyimbo na kucheza ngoma za China, na mchezo wa Wushu ya China pia yalikaribishwa na watu.

Idhaa ya kiswahili 2007-06-22