Wafanyakazi wa Idhaa ya Kiswahili ya CRI
China Radio International
China
Dunia
(GMT+08:00) 2007-06-25 14:52:34    
Mwigizaji wa filamu Yu Entai

cri

Mchezo wenye sehemu 80 wa vichekesho kwenye televisheni "Hadithi za Wanagonfu Hodari wa Zama za Kale Nchini China" ulianza kuoneshwa katika vituo vingi vya televisheni nchini China. Mchezo huo unawafurahisha sana watazamaji, na hasa vijana. Waigizaji katika mchezo huo wamejulikana kutokana na mchezo huo, mmoja kati ya waigizaji ni Bw. Yu Entai.

Mchezo huo unaeleza msichana mmoja aitwaye Guo Furong, alizuiliwa katika hosteli moja kwa kudaiwa. Katika hosteli hiyo alifahamiana na mwenye hosteli Bw. Dong, mwizi hodari wa zamani Bai Zhantang, msomi Lu, mpishi Li na wengine ambao wana tabia tofauti, na katika maingiliano nao yalitokea mambo mengi ya kuchekesha. Mchezo huo unawafundisha watazamaji kuwa matatizo na matata yanapotokea yasitatuliwe kwa ubabe, njia nzuri ya utatuzi ni uaminifu na upendo kati ya binadamu. Kwa hiyo ingawa mchezo huo ni wa kuchekesha na unachezwa kwa mapigano ya kigongfu lakini mada yake ni kupinga kutumia nguvu.

Katika mchezo huo Bw. Yu Entai alimuiga msomi aitwaye Lu ambaye ni mtu mpole na mara nyingi alichekesha kwa kuwakoga wengine kwa elimu yake kubwa na kusema kwa Kichina cha kale na Kiingereza, maneno yaliyokuwa mdomoni mwake huwa ni "To be or not to be", na "Confucius anasema, ubabe hauwezi kutatua tatizo lolote". Watazamaji wanampenda sana msomi huyo aliyeigizwa na Yu Entai, na kundi la wapenzi wa mwigizaji Yu Entai limejipatia jina la "mapezi", Bw. Yu Entai anafurahia jina la kundi hilo. Alisema,

"Sikutarajia kupata umaarufu kama hivi kupitia mchezo mmoja tu nilioigiza. Kundi la mahabiki wangu na kujipatia jina hilo vinanitia moyo, nafurahia jina hilo la 'mapezi'."

Bw. Yu Entai ana umri wa miaka 30, ni mtu mwenye kiwango cha juu zaidi cha masomo miongoni mwa waigizaji vijana nchini China. Mwaka 1999 alihitimu masomo yake katika Chuo Kikuu cha Uigizaji cha Shanghai, mwaka 2002 alisoma elimu ya uigizaji katika Chuo Kikuu cha Oxford, mwaka 2005 alipata shahada ya pili katika Chuo Kikuu cha Uigizaji cha Shanghai na mwaka 2006 alisomea elimu ya uongozaji wa michezo ya kuigiza katika Chuo Kikuu cha Uigizaji cha Beijing.

Hivi karibuni, katika mchezo wa kuigiza wa "Mapenzi na Maisha katika Sehemu Iliyotengwa na Dunia". Mchezo huo uliwahi kuchezwa kisiwani Taiwan kwa muda wa zaidi ya miaka 20 na uliwavutia watazamaji hata tikiti zilikuwa shida kupatikana. Mmoja wa watazamaji alisema uigizaji wa Bw. Yu Entai uligusa sana hisia zake.

Bw. Yu Entai anajivunia kwa kufanikiwa kuigiza mhusika mmoja katika mchezo huo. Kila baada ya kuuigiza alikuwa hujadiliana na waigizaji wengine namna ya kuigiza vizuri zaidi. Kutokana na umakini wake wa uigizaji, mchezo huo ulipooneshwa katika China bara uliwavutia zaidi watazamaji. Alisema,

"Nilikuwa na hamu ya kuigiza mchezo huo, lakini sikupata nafasi kwani uigizaji wa mchezo huo unatakiwa kwa kiwango cha juu sana, hata nilipokuwa katika chuo kikuu na kufanya mazoezi ya uigizaji, wale wanafunzi wenye matokeo mazuri tu ya masomo ndio waliochaguliwa kuigiza sehemu fulani ya mchezo huo. Sikutegenea kwamba baada ya miaka zaidi ya kumi kweli nimepata nafasi ya kuigiza mchezo huo."

Mchezo wa kuigiza wa "Mapenzi na Maisha katika Sehemu Iliyotengwa na Dunia" ni muunganisho wa michezo miwili ya kuigiza. Mchezo wa "Mapenzi" unaeleza jinsi wachumba wawili walivyofahamiana, walivyopendana na walivyoachana. Na mchezo wa "Maisha katika Sehemu Iliyotengwa na Dunia" unaonesha kuwa baada ya kugundua mke wake kuwa na mapenzi nje ya ndoa aliondoka nyumbani na kuishi katika sehemu iliyotengwa na dunia, mambo yaliyotokea katika maisha yake yalichekesha.

Mchezo wa "Mapenzi na Maisha katika Sehemu Iliyotengwa na Dunia" unahuzunisha na kuchekesha. Bw. Yu Entai alisema,

"Naona kwamba waigizaji wa kuchekesha hakika wana mambo ya huzuni yasiyojulikana kwa wengine, kwa mfano, mwigizaji maarufu wa kuchekesha wa Uingereza Bw. Charles Spencer Chaplin, maisha yake yalijaa mambo ya kusikitisha. Watu huona kwamba maisha ya waigizaji wa kuchekesha hakika ni ya furaha, lakini ukweli ni kwamba wanapowachekesha watazamaji wanahuzunika mioyoni mwao."

Licha ya kuigiza michezo, Bw. Yu Entai anashughulika na mambo mengine ya utamaduni. Aliwahi kutafsiri michezo mingi ya kuigiza kutoka lugha ya Kiingereza, na siku chache zilizopita alikuwa mtangazaji wa kipindi cha "matukio katika kalenda yetu", kipindi hicho alikiendesha kwa aina mpya kabisa na kinavutia zaidi.

Idhaa ya kiswahili 2007-06-25