Wafanyakazi wa Idhaa ya Kiswahili ya CRI
China Radio International
China
Dunia
(GMT+08:00) 2007-07-04 15:05:12    
Tamasha la filamu za Hong Kong lafanyika kwenye kasri la mataifa la Umoja wa Mataifa

cri

Tarehe mosi Julai ilikuwa ni siku ya kuadhimisha mwaka wa kumi tokea Hong Kong irudishwe nchini China. Tarehe 3 jioni tamasha la filamu za Hong Kong lilizinduliwa katika kasri la mataifa la Umoja wa Mataifa, katika tamasha hilo la siku tatu filamu tatu mpya za Hong Kong zitaoneshwa na pia yatafanywa maonesho ya picha zinazoonesha maisha wa wakazi wa Hong Kong kutoka pande mbalimbali. Watu wanaweza kufahamu hali ilivyo ya ustawi wa uchumi na utulivu wa jamii ya Hong Kong katika muda wa miaka kumi iliyopita chini ya sera ya "nchi moja, mifumo miwili".

Tamasha hilo limeandaliwa na ujumbe wa China na ofisi ya uchumi na biashara ya Hong Kong mjini Geneva. Filamu tatu zinazooneshwa katika tamasha hilo ni "Upendo", "Furaha ya Siku ya Kuzaliwa" na "Baba na Mwana". Kwenye uzinduzi mfupi uliofanyika jioni ya tarehe 3 kwenye kasri la mataifa naibu katibu mkuu wa Umoja wa Mataifa ambaye pia ni mkurugenzi wa ofisi ya Geneva ya Umoja wa Mataifa Bw. Ordzhonikidze alisema Wachina kote duniani wanaisherehekea siku ya kuadhimisha mwaka wa kumi tokea Hong Kong kurudishwa nchini China, tamasha hilo likiwa kama ni sehemu ya shughuli hizo Umoja wa Mataifa unafurahia tamasha hilo. Alisema,

"Kitu muhimu ni kwamba filamu hizo zinaweza kuimarisha maingiliano na maelewano na zinaweza kuzifanya tamaduni tofauti ziheshimiane na kuifanya dunia iwe na amani na utulivu. Filamu zina athari kubwa zaidi kuliko sheria, na ni muhimu sana katika kupatanisha tamaduni tofauti."

Bw. Ordzhonikidze aliongeza kuwa ingawa watazamaji kwenye kasri la Umoja wa Mataifa wana shida ya kuelewa lugha lakini furaha na huzuni za binadamu ni za namna moja kwa binadamu wote.

Balozi mpya wa China mjini Geneva Bw. Li Baodong alilielezea tamasha hilo kwa mtazamo mwingine. Alisema tamasha hilo sio shughuli za utamaduni tu, bali ni pamoja na hali ya ustawi ikiwa ni pamoja na sekta ya filamu na utamaduni na uchumi katika muda wa miaka kumi iliyopita imethibitisha kuwa sera ya "nchi moja, mifumo miwili" imepata mafanikio makubwa. Alisema,

"Sera ya 'nchi moja, mifumo miwili' sio ya kubahatisha tu, bali ni mfano wa sera za amani za China katika mambo ya nje. China ni nchi inayowajibika, inatekeleza kwa makini ahadi zake, utekelezaji wa sera ya 'nchi moja, mifumo miwili' huko Hong Kong ni matokeo ya lazima ya ahadi pamoja na vitendo."

Mkurugenzi wa Ofisi ya Hong Kong mjini Geneva Bw. Martin Glass kwenye ufunguzi alieleza hali ya maendeleo katika sekta ya filamu ya Hong Kong ilivyo. Alisema, hivi sasa Hong Kong imekuwa moja ya kituo cha filamu duniani, mwaka jana ilitengeneza filamu 51 na thamani ya filamu zilizouzwa katika nchi za nje imefikia dola za Kimarekani milioni 60, na filamu za Hong Kong mara nyingi zinapata tuzo katika matamasha ya filamu duniani. Ustawi wa filamu wa Hong Kong unatokana na waongoza filamu hodari, waigizaji hodari, wahariri hodari pamoja na teknolojia ya hali ya juu, na vile vile unatokana na nafasi ya Hong Kong isiyo kawaida duniani. Alisema,

"Hong Kong imekuwa daraja kati ya utamaduni wa nchi za magharibi na China bara, ni kama dirisha kwa watazamaji wa China kuifahamu dunia ya magharibi, na kwa sababu hiyo filamu za Hong Kong pia zinakubalika kwa watazamaji wa nchi za magharibi."

Idhaa ya kiswahili 2007-07-04