Kwenye mkutano wa kwanza wa baraza la "kushirikiana na nchi za Afrika ili kupata maendeleo ya pamoja" uliofanyika tarehe 30 Juni hadi tarehe 1 Julai huko Nanjing, mwandishi wa habari wetu alifanya mahojiano na Bw. Joseph Wolukau, mwanafunzi anayefanya utafiti na kujitahidi kupata shahada ya juu kwenye kituo cha utafiti wa kilimo ya Afrika cha chuo kikuu cha kilimo cha Nanjing mkoani Jiangsu, China, ambaye alikuwa mwalimu wa chuo kikuu cha Egerton cha Kenya.
Bw. Joseph alikuja Nanjing mwaka 2004, wakati alipotaja picha yake kuhusu Nanjing na ametembeela sehemu gani mjini Nanjing alisema kuwa, anaona mjini Nanjing kuna vivutio mbalimbali kama vile kaburi la Bwana Sun Yat San, Ziwa Xuanwu, Lango Zhonghua na vinginevyo. Kila akipata nafasi hutembelea sehemu mbalimbali mjini Nanjing, anafurahi matembezi kama hayo.
Bwana Joseph alisema, amezoea maisha yake mjini Nanjing, ila tu hali ya hewa ya huko ni joto zaidi kuliko ile ya Kenya, lakini anazoea siku hadi siku.
Bwana Joseph alisema, kabla ya kuja China yeye alipata ujuzi kuhusu China kutoka kwenye magazeti, mwanzoni alisoma vitabu kadhaa kuhusu China nchini Kenya. Na baada ya kuja China amepata fursa nyingi za kuielewa zaidi China, siku hizi hata kwa kupitia mtandao wa internet, anaweza kupata habari nyingi zaidi kuhusu China.
Bwana Joseph alisema, alipokuwa na nafasi alikwenda miji mingine nje ya Nanjing kufanya matembezi, kama mji wa Hangzhou, ambapo aliona vivutio vingi, hekula kubwa la Budha, watu wengi walioabudia Budha, aliona Ziwa Xihu ambalo ni ziwa maarufu nchini. Anaona mji wa Hangzhou ni wenye mandhari nzuri.
Bw. Joseph alimwambia mwandishi wetu kuwa, katika chuo kikuu cha kilimo cha Nanjing anafanya utafiti kuhusu mazao ya kilimo, magonjwa ya kilimo na mambo mbalimbali yanayohusika na uzalishaji wa kilimo. Atarudi nyumbani mwanzoni mwa Mwezi Julai, na baada ya kurudi nyumbani atatoa mapendekezo mbalimbali kwa wakulima wa Kenya ili wapate teknolojia za kisasa kuhusu uzalishaji wa kilimo, atawaletea wakulima wa Kenya uzoefu na teknolojia ya kisasa ya China na kuwasaidia kujiendeleza. Kilimo ni sekta muhimu katika nchi nyingi za Afrika, mapendekezo ya Bw. Joseph bila shaka yatanufaisha wakulima wa Afrika.
Habari zinasema, chuo kikuu cha Egerton kinashirikiana na chuo kikuu cha kilimo cha Nanjing kuanzisha kituo cha ushirikiano wa kilimo kati ya China na Kenya. Atarudi chuo kikuu cha Egerton na kufanya kazi katika chuo hicho.
|