Wafanyakazi wa Idhaa ya Kiswahili ya CRI
China Radio International
China
Dunia
(GMT+08:00) 2007-07-09 16:12:32    
Matembezi kwenye mlima wa kibudha wa Jiuhua

cri

Mlima Jiuhua ulioko mkoani Anhui, China ni moja kati ya milima minne maarufu ya dini ya kibudha nchini China. Kuna mahekalu mengi ya dini ya kibudha kwenye mlima huo, ambao unajulikana pia kama "nchi ya kibudha ya ua la yungiyungi" kutokana na kuwa kilele cha mlima huo kinafanana na ua la yungiyungi.

Mlima Jiuhua una eneo la kilomita za mraba 120. Mlima huo mzuri sana una vilele vingi. Mkurugenzi wa shirika la maendeleo ya utalii ya mlima wa Jiuhua Bw. Gui Lin alisema, tokea zama za kale mlima wa Jiuhua ni mlima maarufu wa dini ya kibudha nchini China, na pia ni sehemu maarufu yenye mandhari nzuri nchini China.

"Mlima wa Jiuhua ni moja ya milima maarufu minne ya kibudha nchini China, mlima huo umekuwa maarufu, kwanza kutokana na sehemu hiyo kuwa na mandhari nzuri ya kimaumbile, mlima huo una vilele 99 kwa jumla, mahekalu mengi yalijengwa katika zama za kale, ambapo sauti za kengele kubwa ya mahekalu hayo zinasikika kila wakati, na toka zamani zinawavutia watalii wengi."

Bw. Gui Lin alisema, sababu ya kujulikana sana kwa mlima wa Jiuhua, licha ya kuwa mazingira mazuri ya kipekee ya kimaumbile, pia ni utamaduni wa kibudha ulioanza miaka mingi sana iliyopita. Inasemekana kuwa Buddha Kshitigarbha alifafanua msahafu wa dini ya kibudha kwenye mlima wa Jiuhua. Buddha Kshitigarbha ni mmoja kati ya mabudha wanne wanaoabudiwa sana katika dini ya kibudha nchini China, dini ya kibudha inasema kuwa, Buddha huyo ni kama ardhi yenye mbingu nyingi zisizohesabika za wema. Basi kwa nini mlima wa Jiuhua ulikuwa mahali pa kufafanua msahafu wa kibudha kwa Budha Kshitigarbha? Profesa wa heshima wa chuo cha dini ya kibudha cha mlima wa Jiuhua Bw. Fei Yechao alisema, kuna hadithi moja inayohusu jambo hilo.

Inasemekana kuwa mwaka 719, mtawa mmoja alifika kwenye mlima Jiuhua, yeye alikuwa mwana wa mfalme wa nchi ya Xinluo iliyoko kwenye peninsula ya Korea, aliitwa Jin Qiaojue. Jin Qiaojue alijifunza elimu ya kibudha tangu utotoni mwake. Hapo baadaye alivuka bahari na kufika China kufanya matembezi kwenye milima na mito maarufu ya China, hatimaye alichagua mlima Jiuhua kuwa mahali pa kujifunza dini na kufanya shughuli za kibudha. Alijifunza elimu ya dini kwa miaka 75, na alifariki dunia alipotimiza umri wa miaka 99.

"Baada ya yeye kufariki dunia, watu waliona kuwa mwili wake hauozi, na kubadilika kuwa 'mwili usiodhurika wa King Kong', jambo hilo liliwastaajabisha sana watu. Hapo baadaye wanafunzi wake walifanya utafiti kuhusu mbinu na njia ya kujifunza elimu ya dini na kujiendeleza pamoja na maandishi yake, waligundua kuwa hayo ni sawa kabisa na maelezo yaliyoandikwa katika msahafu wa kibudha kuhusu Budha Kshitigarbha. Msahafu wa kibudha unasema, Budha Kshitigarbha yuko katika dunia yetu hii, dhamira ya Jin Qiaojue ni sawa kabisa na ile ya Buddha Kshitigarbha, hivyo watu wanasema yeye ndiye Buddha Kshitigarbha aliyegeuka binadamu na kufika huko, hivyo mlima wa Jiuhua ukachukuliwa kuwa ni mahali pa kufanyia shughuli za dini ya kibudha kwa Buddha Kshitigarbha."

Kuna mabaki mengi kwenye mlima Jiuhua yanayomhusu Jin Qiaojue, kati ya mahali pa kujifunza dini ya kibudha kwa miaka ile, kuna sehemu moja maarufu, ambayo ni hekalu la Dongya lililojengwa kwenye genge la mlima mkubwa. Habari zinasema, mlima Jiuhua uliumbwa kwa mawe ya granite?hivyo mahekalu mengi yaliyojengwa kwenye mlima Jiuhua yako kwenye miteremko ya mlima, baadhi ya majengo yalijengwa kwenye mawe makubwa, ambayo yanaungana pamoja na mlima, miti na mawingu na kuwa mandhari nzuri wa kipekee. Mwongoza watalii wa mlima Jiuhua Bw. Li Lu alisema, hekalu la Dongya liko kwenye kilele chenye urefu wa mita 871 juu ya usawa wa bahari, siyo tu liko karibu na genge la mlima, bali pia kuna ndege aina ya mbayuwayu wengi wanaoruka angani.

Mwandishi wa habari aliuliza, "Tukitazama chini kutoka hapa, tunaona genge refu sana, tena tunaweza kusikia sauti ya mtiririko wa maji. Sasa tunaona mbayuwayu wengi wakirukaruka, je! Huo ni umaalumu wa mlima wa Jiuhua?"

Mwongoza watalii alisema, "Huu ndiyo umaalumu wa mlima wa Jiuhua. Kwa kuwa mazingira ya asili ya mlima wa Jiuhua yanahifadhiwa vizuri, hivyo hapa kuna ndege wengi."

Mlima Jiuhua unajulikana sana kwa majengo ya kibudha, tena una mandhari nzuri ya milima na mto. Katika njia ya mlimani kuna sehemu moja inayoota maua mengi, ambapo maua ya azalea yanayoota na kuwa madogo, lakini huko yanakuwa makubwa kama mti. Mtu akitembea kwenye njia iliyotandikwa vipande vikubwa vya mawe, anaweza kuona maua na miti mingi, na kusikia milio ya ndege wa aina nyingi, hali ambayo inaongeza uzuri na ukimya wa bonde la mlimani.

Toka zama za kale, wasomi wengi walivutiwa na uzuri wa mlima Jiuhua. Bw. Li Yong ni mchoraji maarufu, ambaye ni mara ya kwanza kwenda kuchora michoro kwenye mlima wa Jiuhua, anaona mlima Jiuhua ni mzuri sana hususan mandhari yake ya miti ya misonobari, mawe yenye maumbo ya ajabu pamoja na mawingu angani. Alisema,

"Mlima wa Jiuhua una mandhari maalumu, hususan ukungu wa mlimani unafanya watu wajisikie kama wamefika peponi wanakoishi malaika."

Idhaa ya kiswahili 2007-07-09