Wafanyakazi wa Idhaa ya Kiswahili ya CRI
China Radio International
China
Dunia
(GMT+08:00) 2007-07-25 14:53:13    
Bi. Pan Du na nyumba yake ya watoto

cri

Katika kijiji kimoja cha mji wa Dalian, mkoani Liaoning, kaskazini magharibi mwa China kuna nyumba maalum ya watoto inayowapokea watoto wa wahalifu wanaotumikia vifungo gerezani.

Nyumba hiyo ilianzishwa mwaka 2003 na Bi. Pan Du. Miaka minne iliyopita Bi. Pan Du mwenye umri wa miaka 38 alipotazama filamu kuhusu jinsi watu wanaojitolea kutoka Hong Kong walivyowasaidia watoto na vijana waliofanya makosa, alipata wazo la kuwasaidia watoto wa aina hiyo. Alitembelea magereza kadhaa ya mkoa wa Liaoning akagundua kuwa, baada ya wazazi kuhukumiwa vifungo gerezani, watoto wao wengi walikuwa wamepoteza malezi na kuishi maisha ya kurandaranda mitaani. Ili kuwawezesha watoto hao wafurahie utoto wao kama walivyo watoto wengine, Bi. Pan Du aliamua kuanzisha nyumba hiyo kwa ajili ya watoto.

Kutokana na watoto hao kukosa upendo, na kutokana na wengi wao ambao waliwahi kuishi maisha ya kurandaranda mitaani, wakilinganishwa na watoto wa familia za kawaida, watoto hao wanaonekana kuwa na mienendo yenye dosari. Mama wa upendo wa nyumba ya watoto Bi. Yang Mei alisema, mwanzoni ilikuwa ni vigumu sana kwake kuwashughulikia watoto hao. Alisema:

"Walipofika hapa walikuwa na wasiwasi sana, walikuwa hawamwamini mtu yeyote, na ilikuwa ni rahisi kwao kukasirika, hawakutaka vitu vyao viguswe na mtu yoyote, na walionekana kuwa ni watoto wenye ubinafsi."

Bi. Yang Mei mwenye umri wa miaka 28 kwa sasa bado hajaolewa, lakini katika zaidi ya miaka mitatu iliyopita alitoa upendo wake kwa watoto hao wanaohitaji sana upendo wa mama. Kati ya watoto hao, aliyempa picha nzuri zaidi ni mtoto wa kiume aitwaye Haiwa. Haiwa alipokuwa na umri wa miaka minane, baba yake alimwua mama yake bila kusudia katika mkwaruzano, baba yake alihukumiwa kifungo gerezani. Jambo hilo lilikuwa ni pigo kubwa kwa Haiwa, mara akabadilika sana na kupenda kukaa katika hali ya upweke, na alikuwa mwepesi kukasirika.

"Nilikuwa namchukia sana baba yangu kwa kuharibu familia yetu iliyokuwa na upendo. Nawaonea wivu sana watoto wengine wanaoishi kwa furaha pamoja na wazazi wao. "

Kwa ajili ya kuwasaidia watoto hao kuondokana na hali ya upweke na mienendo mibaya, mama wa upendo wa nyumba hiyo wanajitahidi kwa wawezavyo kuwapa upendo kama vile kuwasaidia kunawa uso, kunawa miguu, kuwasimulia hadithi na kulala pamoja nao. Mtoto mmoja akiugua walezi wote wanamtunza kwa makini.

Hivi sasa watoto wa nyumba hiyo wanaishi kwa furaha na kwa afya wakiwa wanatunzwa na mama wa upendo. Familia hiyo maalum imewafahamisha watoto hao namna ya kuwashughulikia watu wengine kwa upendo. Kutokana na kupewa maelekezo na mama wa upendo, watoto hao wameelewa upya maisha yao ya zamani, na kufahamu namna ya kukabiliana na wazazi wao, na badala ya kuwachukia wazazi wao waliofanya makosa, sasa wameanza kuwapenda.

Jambo lingine linalowafurahisha mama wa upendo ni kuwa, watoto hao wameanza kufuatiliwa na jamii, serikali katika ngazi tofauti, mashirika ya ufadhili, na watu binafsi wamechanga fedha na vitu kwa wingi kwa ajili ya nyumba hiyo. Bi. Pan Du alisema:

"Kuangalia dunia hii tunayoishi nayo na kuwafuatilia watu wanaohitaji matunzo. Naona kuwa kupenda ni kuzuri zaidi kuliko kuchukia, wanaotoa msaada watapewa furaha."

Idhaa ya kiswahili 2007-07-25