Mahitaji
Ini la nguruwe gramu 200, uyoga gramu 20, tango moja, mvinyo wa kupikia vijiko viwili, siki kijiko kimoja, mchuzi wa sosi vijiko vitatu, sukari kijiko kimoja, chembechembe za kukoleza ladha, chumvi vijiko viwili, wanga vijiko viwili, kiasi kidogo vipande vya vitunguu maji, vitunguu saumu na tangawizi
Njia
1. kata ini la nguruwe liwe vipande vipande. Kata tango liwe vipande vipande. Osha uyoga.
2. koroga mvinyo wa kupikia, mchuzi wa sosi, siki, sukari, chembechembe za kukoleza ladha, chumvi na maji ya wanga.
3. washa moto tia mafuta kwenye sufuria, mpaka yawe nyuzi za joto la 80, tia vipande vya ini la nguruwe, korogakoroga, halafu vipakue.
4. washa moto tena, tia vipande vya vitunguu maji, vitunguu saumu na tangawizi korogakoroga, tia vipande vya ini la nguruwe, sosi iliyokorogwa, korogakoroga, tia uyoga, vipande vya tango, korogakoroga. Mimina mafuta ya ufuta, korogakoroga ipakue. Mpaka hapo kitoweo hiki kiko tayari kuliwa.
|