Wafanyakazi wa Idhaa ya Kiswahili ya CRI
China Radio International
China
Dunia
(GMT+08:00) 2007-08-30 15:51:20    
Mabadiliko ya "shule za msingi zilizojengwa kwenye migongo ya farasi"

cri

Miaka 30 iliyopita, kwenye mbuga kubwa ya Xilinguole ya mkoa unaojiendesha wa Mongolia ya Ndani, matakwa makubwa kabisa ya Siqinbilige aliyekuwa na umri wa miaka 12 yalikuwa kukutana na mwalimu wake aliyefika mara moja kwa wiki kwa kupanda farasi kuwafundisha yeye na wenzake kusoma na kuandika na kuwasimulia hadithi. Hivi sasa yeye amekuwa mkurugenzi wa shule ya msingi ya kikabila ya wilaya ya Xilinguole, na matakwa yake kwa sasa ni kupanua shule yake ili kuwaandikisha watoto wengi zaidi wa wafugaji wa huko.

Katika miaka ya 70 ya karne iliyopita, kwenye mbuga kubwa ya Mongolia ya ndani yenye eneo kubwa na watu wachache, wilaya moja ilikuwa na familia 4 au 5 tu, hivyo hakukuwa na shule maalumu. Ili kuwawezesha watoto wa wafugaji hao wapate elimu, walimu walikuwa wanapanda farasi kwenda katika mahema ya wakazi wa kabila la wamongolia kuwafundisha watoto, hivyo shule za huko ziliitwa "shule za msingi zilizojengwa kwenye migongo wa farasi". Bi. Siqinbilige alisema:

"Walimu walitufundisha Kichina, na kutusimulia hadithi. Tulifahamu mambo ya nje kutoka kwa walimu waliokuja kutufundisha kwa kupanda farasi."

Lakini mwanafunzi wa shule ya msingi mwenye umri wa miaka 13 kwa sasa aliyezaliwa katika familia ya mfugaji Zhu La, anaishi maisha mazuri zaidi kuliko ilivyokuwa kwa Bi.Siqinbilige. Hivi sasa anakaa kwenye darasa zuri na kusoma kama wanavyosoma wanafunzi wa mijini, anaweza kuongeza Kichina kizuri, hata lugha ya Kiingereza.

Miaka mitatu iliyopita, mkoa unaojiendesha wa Mongolia ya ndani ulianza kutekeleza mradi wa kurekebisha mfumo wa elimu katika sehemu wanazoishi wafugaji. Mwenyekiti wa mkoa huo Bwana Yang Jing alisema:

"Tangu China ianze kufanya mageuzi na kufungua mlango, mkoa wetu ulikuwa umefuata utaratibu wa kuwakusanya wanafunzi na kujenga shule za bweni. Lakini kutokana na hali duni ya shule na kiwango cha chini cha walimu, baadhi ya watoto wa wafugaji baada ya kuhitimu masomo waliamua kurudi nyumbani kujishughulisha na ufugaji, hivyo ufanisi wa kuendesha shule hauwezi kuonekana vizuri."

Mwaka 2004 mkoa unaojiendesha wa Mongolia ya ndani ulianza kutekeleza mpango wa kuanzisha shule za msingi na sekondari katika miji ya wilaya, wanafunzi wa kabila la wamongolia na makabila mengine madogo madogo si kama tu wameondolewa karo za shule, bali pia wanapewa chakula kila mwezi. Katika miaka mitatu iliyopita, wilaya ya Xilinguole ilikuwa imewekeza Yuan milioni 5.9 kuwajumuisha watoto 6,200 wa wafugaji wasome katika shule za mjini. Zaidi ya hayo, wilaya hiyo pia imetenga fedha maalumu kwa ajili ya kuwapa ruzuku ya kiserikali watoto wa wafugaji wanaosoma katika shule ya sekondari ya juu.

Takwimu zilizotolewa na idara ya elimu ya mkoa unaojiendesha wa Mongolia na ndani zimeonesha kuwa, ilipofika mwezi Juni mwaka huu, watoto wote wenye umri wa kusoma shule wamepewa elimu ya lazima ya miaka tisa, na idadi ya wanafunzi wa vyuo vikuu ilifikia elfu 70 hivi, ambayo imeongezeka kwa mara tatu ikilinganishwa na ile ya mwaka 2000.

Bi. Siqinbilige alisema, ili kuwaelimisha watoto utamaduni wao wa jadi, shule za msingi na sekondari pia zimeanzisha vikundi mbalimbali vya mashabiki kama vile sataranji (chess) ya kimongolia, Madouqin ambayo ni ala maalumu ya kimongolia, na michezo ya jadi."

Idhaa ya kiswahili 2007-08-30