Mwandishi wa habari wa gazeti la moja la Algeria Bw. Ali alisema, zamani alifahamu hali kuhusu China kwa kupita vyombo vya habari vya nchi za magharibi, lakini ziara aliyofanya nchini China ilimfanya aelewe hali halisi nchini China. Mwandishi huyo wa habari amefanya kazi ya utoaji wa habari za kimataifa kwa miaka mitano, alisema wakati wa ziara yao nchini China, alitembelea Beijing, mji mkuu wa China, pia alikwenda mkoani Hunan. Ili kufanya mawasiliano kwa uhuru na vijana wa China, aliwaalika vijana kadhaa wa China kula chakula pamoja nao. Aliona kuwa zamani alielewa mambo machache sana kuhusu China.
Mwandishi wa habari anayefanya kazi kwenye Radio Algeria kimataifa Bw. Mustafa alisema, ingawa zamani aliwahi kusikia mabadiliko kuhusu China, lakini baada ya yeye mwenyewe kufika China, aliona kihalisi mabadiliko hayo makubwa. Alisema ujenzi wa miradi unafanyika katika sehemu mbalimbali nchini China. Mwandishi huyo wa habari alieleza matumaini yake kuwa ataweza kufanya kazi kwa muda nchini China, anataka kuona mabadiliko nchini China, pia anataka kurudi Algeria na uzoefu wa China.
Mkurugenzi wa gazeti la Siku za mbele la Algeria Bw. Nabih alisikitika kuwa hajapata fursa ya kuja China. Maneno ya wenzake kuhusu hali ya China yaliongeza hamu yake ya kutaka kuitembelea China. Alisema ana imani kuwa atakuwa na fursa ya kuitembelea China. Balozi wa China nchini Algeria Bw. Zhang Shixian aliwaambia waandishi wa habari kuwa, China inawakaribisha marafiki wengi zaidi wa nchi za nje kuitembelea, ili waweze kuona mabadiliko ya China wao wenyewe, pia China inapenda kusikiliza mapendekezo yanayosaidia maendeleo ya China.
Bw. Zhang Shixian alisema, China na Algeria zote ni nchi zinazoendelea, zina historia inayofanana, pia hivi sasa zinakabiliwa na changamoto za pamoja. Kuzidisha mawasiliano kati yao kunaonesha urafiki kati yao, na kutazinufaisha pande hizo mbili ili kutimiza lengo la kupata maendeleo ya pamoja.
Mwezi Novemba mwaka jana, baraza la ushirikiano kati ya China na Afrika lilitunga mipango ya mfululizo kuhusu kuimarisha zaidi mawasiliano kati ya China na Afrika, ukiwemo mpango wa kuwaandaa watu wa nchi za Afrika. Waandishi wa habari zaidi 10 wa Algeria Kuitembelea China ni sehemu moja ya mpango huo.
**************
Waziri wa habari na mawasiliano wa Kenya Bw. Koigi Wamwere hivi karibuni alipokutana na naibu mkurugenzi wa shirika la habari la Xinhua, China Bw. He Ping alisema, Kenya itaendelea kuimarisha ushirikiano na China katika sekta ya habari, ili kuzidisha maelewano na urafiki kati ya wananchi wa nchi hizo mbili.
Bw. Wamwere alisema shirika la habari la Kenya linaloongozwa na wizara ya habari na mawasiliano lina uhusiano wa kirafiki na wa muda mrefu na shirika la habari la China Xinhua, mawasiliano kati yao yanasaidia kuhimiza ushirikiano kati yao. Bw. Wamwere pia akiwa kwa niaba ya serikali ya Kenya na alishukuru shirika la habari la China Xinhua kwa kutoa vitendea kazi kwa shirika la habari la Kenya.
Bw. He Ping alisema China na Kenya zote ni nchi zinazoendelea, na maendeleo ni jukumu la kwanza linalozikabili nchi hizo mbili. Alisema shirika la habari la Xinhua linazingatia siku zote mafanikio zilizopata nchi za Afrika ikiwemo Kenya katika sekta za uchumi na jamii, na linashikilia kuripoti habari za Afrika kwa msimamo wa haki kuhusu mambo ya sekta mbalimbali zilizo za halisi
****************
Watoto sita kutoka sehemu za magharibi nchini Kenya tarehe 11 mwezi Agosti walianza safari zao na kwenda shule ya sarakasi ya Wu Qiao mkoani Hebei, China kwa ajili ya mafunzo ya sarakasi ya mwaka mmoja. Serikali ya Kenya siku hiyo kwenye jumba la tamthiliya la taifa ilifanya sherehe ya kuwaaga watoto sita wenye umri kati ya miaka 11 hadi 15. ambapo wanafunzi kadhaa waliojifunza sarakasi nchini China mwaka jana walifanya maonesho ya michezo ya sarakasi ya kichina iliyoyavuta watu
Waziri wa mambo ya wanawake, michezo, utamaduni na huduma za jamii Bi. Maina Kamanda aliishukuru serikali ya China kwa kuwaandaa wachezaji wa sarakasi wa Kenya, vilevile aliwataka watoto hao watumie fursa za kujifunza sarakasi nchini China, kufanya juhudi na kurudi nchini Kenya mapema pamoja na ufundi hodari wa sarakasi. Bi. Kamanda alisema, China ni nchi kubwa yenye ufundi wa sarakasi, ameitaka China itume walimu kadhaa nchini Kenya, ili watoto wengi zaidi wa Kenya wapewe mazoezi maalumu ya michezo ya sarakasi.
Balozi wa China nchini Kenya Bw. Zhang Ming alisema, ikiwa sehemu moja ya mawasiliano ya utamaduni kati ya China na Kenya, tangu mwaka 2003 kila mwaka China inapokea watoto 6 wa Kenya, na kutoa mafunzo ya michezo ya sarakasi kwao. Licha ya hayo kila mwaka serikali ya China inapokea wanafunzi 80 wa Kenya kusoma nchini China.
**************
Ubalozi wa China nchini Kenya tarehe 22 ulitangaza kuwa, mwaka kesho serikali ya China itaongeza kwa mara moja idadi ya wanafunzi wa Kenya wanaopata udhamini wa masomo nchini China idadi ya wanafunzi hao itafikia 80, ili kuhimiza mawasiliano ya utamaduni kati ya nchi hizo mbili.
Balozi wa China nchini Kenya Bw. Zhang Ming siku hiyo aliwapatia wanafunzi 40 wa Kenya taarifu ya kuandikishwa kwao. Alisema China na Kenya zote ni nchi zinazoendelea, na zinakabiliwa na majukumu makubwa ya kuendeleza uchumi na kuinua kiwango cha maisha ya watu, hivyo zote zinahitaji wa vijana wengi wenye ujuzi.
Bw. Zhang Ming alisema katika miaka kadhaa iliyopita China na Kenya ziliimarisha ushirikiano katika sekta mbalimbali, hasa sekta ya elimu. Tangu miaka ya 90 ya karne iliyopita, kila mwaka wanafunzi 2000 wa Afrika walipata udhamini wa masomo nchini China. Kwenye mkutano wa wakuu wa Baraza la Ushirikiano kati ya China na Afrika uliofanyika mwaka jana hapa Beijing, serikali ya China iliahidi kuongeza idadi hiyo kuwa 4000 kila mwaka. Ili kutimiza ahadi hiyo, kuanzia mwaka kesho idadi ya wanafunzi wa Kenya watakaopata udhamini wa masomo nchini China itaongezeka kuwa 80 kutoka 40 kila mwaka.
Idhaa ya kiswahili 2007-08-31
|