Wafanyakazi wa Idhaa ya Kiswahili ya CRI
China Radio International
China
Dunia
(GMT+08:00) 2007-09-20 15:27:28    
Kamati ya maandalizi ya michezo ya Olimpiki ya Beijing imetoa taarifa rasmi ya kukusanya picha za nyuso za watoto wanaocheka duniani

cri

Kamati ya maandalizi ya Michezo ya Olimpiki ya Beijing tarehe 5 Septemba ilitoa taarifa rasmi ya kukusanya picha za kitarakimu za watoto wanaocheka wa nchi mbalimbali duniani, na picha zitakazochaguliwa kati ya hizo zitatumika kwenye maonesho ya michezo ya sanaa ya ufunguzi na ufungaji wa Michezo ya Olimpiki ya Beijing.

Inafahamika kuwa ili kuwafanya wakazi waweze kushiriki kwenye maandalizi ya ufunguzi na ufungaji wa Michezo ya Olimpiki ya Beijing, kamati ya maandalizi ya michezo hiyo imeamua kukusanya picha za watoto wanaocheka wa nchi mbalimbali duniani. Muda wa shughuli hizo ni kuanzia tarehe 5 mwezi Septemba mwaka huu hadi tarehe 30 mwezi Aprili mwaka 2008.

Habari zinasema picha zitakazokusanywa ni za nyuso za wa watoto wanaocheka ambazo hazijatumika kibiashara, bila kujali watoto hao ni wa jinsia gani, lakini umri wa watoto hao unatakiwa kuwa chini ya miaka 10. Kila mtu anayetoa ombi anaweza kutoa picha za watoto kadhaa, lakini picha za kila mtoto zisizidi tano. Picha hizo zinatakiwa kuwa za rangi, na ziwe zimepigwa kwa kamera ya kitarakimu yenye Megapixel 5.

Ofisa anayeshughulikia mambo ya ufunguzi na ufungaji wa Michezo ya Olimpiki ya Beijing amesema Kamati ya maandalizi ya Michezo ya Olimpiki ya Beijing itafanya marekebisho kadhaa katika picha hizo kutokana na mahitaji ya maonesho ya michezo ya sanaa wakati wa ufunguzi na ufungaji wa michezo, na kuamua namna ya kutumia picha hizo.

Ili kuhakikisha mtindo mpya wa uvumbuzi na kuuwezesha uoneshwe vizuri kwenye ufunguzi na ufungaji wa Michezo ya Olimpiki, hivi sasa Kamati ya maandalizi ya Michezo ya Olimpiki ya Beijing haiwezi kutangaza njia ya kutumia picha hizo, na kwa kufuata kazi ya kuandaa michezo hiyo itatangaza katika wakati wa kufaa.

Kuanzia tarehe 5 mwezi Septemba wa mwaka huu, watu wanaweza kutembelea tovuti ya Michezo ya Olimpiki ya Beijing, anuani yake ni www.beijing2008.cn kuangalia "waraka wa kukusanya picha za nyuso za watoto wanaocheka wa Michezo ya Olimpiki ya Beijing", kupata fumu husika za kujiandikisha. Watu wakijaza fomu kwa kufuata kanuni, wanaweza kupeleka CD yenye picha zao kwa njia ya haraka kwenye ofisi ya kukusanya picha za nyuso za watoto wanaocheka ya kituo cha uendeshaji wa sherehe za ufunguzi na ufungaji wa Michezo ya Olimpiki ya Beijing, anuani ni Beijing, China, Namba ya posta ni 100085.

Habari zinasema jumba la makumbusho ya wanawake na watoto la China ambalo ni jumba la kwanza la makumbusho kuhusu wanawake na watoto nchini China litafunguliwa mwishoni mwa mwezi Julai mwaka 2008.

Katibu wa sekretarieti ya shirikisho kuu la wanawake wa China Bi. Zhang Shiping tarehe 5 mwezi Septemba alifahamisha hali ya ujenzi wa jumba hilo. Alisema jumba hilo liko upande wa kaskazini wa barabara ya Chang'an, mjini Beijing. Jumba hilo lina eneo la mita za mraba elfu 35 na linaundwa na jumba la wanawake na jumba la watoto. Baada ya ujenzi wa jumba hilo kukamilika, maonesho ya hali ya maisha ya wanawake na watoto, mabadiliko ya hadhi yao, desturi na utamaduni na mchango wao kwa jamii yatafanyika kwenye jumba hilo.

Kazi za kukusanya mabaki ya utamaduni zimepata maendeleo. Hadi sasa limepata mabaki ya utamaduni zaidi ya 8600 vikiwemo vyombo vya udongo, vyombo vya mawe, vyombo vya shaba nyeusi, nguo za kikabila, vyombo na vifaa vilivyotumika kwenye uzalishaji na maisha, na data husika za filamu na vitabu.

Kabla ya hapo, shirikisho kuu la wanawake wa China lilianzisha mfuko maalumu wa Jumba la makumbusho Ya wanawake na watoto la China katika mfuko wa watoto na vijana wa China, na kupokea michango iliyotolewa na watu wa hali mbalimbali kutoka kwenye jamii.

Idhaa ya kiswahili 2007-09-20