Jua la alasiri lilikuwa likiangaza kwenye njia iliyotandikwa vipande vya mawe, tulipotembea kwenye njia hiyo ya kuelekea Shangri-la tulisikia muziki huo unaojulikana kwa "Shangri-la nzuri". Kwa kufuata mahali unapotoka sauti ya muziki, tuliingia kwenye baa moja. Mwenye baa hilo ni kijana Adu mwenye umri wa miaka zaidi ya 30. "Shangri-la nzuri" ni muziki anaopenda zaidi. Kila anapojiwa na wageni waliotoka mbali, Adu huwaburudisha kwa muziki huo wa saxophone. Wakati tulipozungumza, Adu alisema, hakutarajia kabisa kuwa alifanya uamuzi wa kubaki Shangri-la baada ya matembezi yake kwenye sehemu hiyo.
"Nilifika hama mwaka 2003. Mwanzoni nilifika hapa ni kufanya matembezi tu, lakini baada ya mimi kukaa kwenye sehemu hiyo kwa muda wa zaidi ya mwezi mmoja, nikaipenda sana. Nilikuwa na wazo la kupanda nyumba ili niweze kuja kupumzika kila mwaka. Baada ya kujiendeleza kwa muda fulani, nikaibadilisha nyumba hiyo kuwa baa."
Ndivyo hivyo, Adu alianza kuishi kabisa kwenye Shangri-la, tena alioa mke na kuzaa mtoto mmoja wa kike. Alilipatia baa hilo jina la "Karakana ya Ana", neno la "ana" katika lutha ya Kitibet ni pombe, hapo zamani nyumba hiyo ilikuwa ya kutengenezea pombe.
Dashan ni rafiki tuliyemzoea kwenye Shangri-la. Dashan ni mwanamke wa kabila la watibet aliyekulia kwenye Shangri-la, jina lake halisi ni Yang Jin.
"Kwa sababu tabia yangu ni nzuri sana, hivyo watu wananiita Dashan, maana yake ni mlima mkubwa. Jina hilo ni rahisi kukumbukwa, tena ni rahisi kwa kuita. Mimi ni mtu ambaye ninagombana na wewe sasa hivi, lakini baada ya dakika mbili tu nikasahau na kufanya urafiki na wewe tena."
Dashan aliwehi kujifunza na kusoma katika Beijing na Shanghai kwa nyakati mbalimbali, halafu alirejea Shangri-la na kuanzisha nyumba ya wageni inayojulikana kwa "Nyumba ya Wageni ya Zamani". Jengo hilo lilijengwa kabla ya miaka 300 iliyopita, baada ya kufanywa matengenezo kupanbwa kwa makini na Dashan, vyumba zaidi ya kumi vya jengo hilo vinaonekana safi na kupendeza.
"Nyumba hiyo ilijengwa zaidi ya miaka 300 iliyopita, nilifanya matengenezo katika nyumba hiyo kwa muda wa mwaka mmoja, nyumba hiyo imedumisha sura yake ya zamani. Zamani hapa ni njia ya kusafirisha cha kwa kutumia farasi, nyumba ya wageni iko mahali pazuri zaidi, vikundi vya wasafirishaji vikija kutoka sehemu ya juu au chini, vilikuwa hukusanyika hapa."
Nyumba hiyo ya wageni si mahali pa kuendesha shughuli za biashara kwa Dasan, bali pia ni mahali pa kujipatia marafiki, wakiwemo watalii wengi waliotoka nchi za nje. Thomas Blake na marafiki zake waliotoka Australia walikaa siku chache kwenye mji wa zamani wa Shangri-la, walikuwa na kumbukumbu nyingi kuhusu "Nyumba ya Wageni ya Zamani" pamoja na wakazi wa mji huo wa kale.
"Tulikaa siku mbili hapa. Tuliona sehemu nyingi ukiwemo mtelemko wa Bijiang tulionja aina mbalimbali za chakula cha hapa. Hapa ni mahali penye kivutio kikubwa, ni mahali penye maajabu mengi na pa kupendeza. "Nyumba ya Wageni ya Zamani" ni jengo zuri la kupendeza. Tuliwahi kukaa kwenye hoteli nyingine, lakini tunapenda zaidi nyumba ya wageni hiyo. Lile ni jengo la zamani, lakini vitu vilivyowekwa ndani ya vyumba pamoja na jinsi vyumba vilivyopambwa ni vya mtindo mpya na vya kipekee."
"Baa la "Karakana ya Ana" pamoja na 'Nyumba ya Wageni ya Zamani' ziko kwenye sehemu ya 'Dukezong', ambayo ni tarafa ya kele ya Shangri-la iliyokuwako toka miaka zaidi ya elfu moja iliyopita. Kuna njia nyingi zilizotandikwa vipande vya mawe, zinaendea sehemu mbalimbali kutoka mji huo wa kale. Nyumba nyingi zilizojengwa kwa mawe zenye mtindo wa kitibet ziko sehemu mbalimbali za mji huo. Nyumba hizo zenye kuta zilizopakwa rangi nyeupe zinag'ara sana chini ya mwangaza wa jua; usiku nyumba hizo zinatoa rangi ya kupendeza katika mbara-mwezi. Hivyo watu wanaita 'Dukezong' ni 'mji wa mawe meupe'."
Ukifika Sangri-la usisahau kuonja chakula cha huko, mgahawa unaojulikana kwa Aruokangba ni maarufu zaidi, mgahawa huo unapendeza sana kutokana na kuwekwa samani za kale, pamoja na vikombe vya chai na vitandiko vyake vilivyotengenezwa kwa kazi nzuri sana. Chakula chenye umaalumu zaidi katika mgahawa wa Aruokangba ni kuku waliopikwa pamoja na kiungo cha bizari, samli tamu iliyochanganywa na maji ya mboga ya spinach ya India, nyama ya ng'ombe iliyopikwa na bia pamoja na samaki iliyokaangwa na maji ya limau. Mgahawa huo una fanasi kwa watu 40 hadi 50 hivi. Wahudumu wote ni wachangamfu, ambao dada mmoja wa kabila la watibet anayeitwa Zhuoma aliiba nyimbo za kienyeji za huko.
Bhaskar Uday ni mpishi mkuu wa mgahawa huo aliyetoka Nepal, anajua sana mapishi ya kitibet, kinepal, kiindia na kichina. Wakati wa kupumzika mpishi huyo aliaungumza na sisi kwa lugha ya Kichina.
"Nimekaa hapa kwa mwaka mmoja unusu. Nilikuwa mpishi mkuu katika sehemu za mikoa ya Gansu, Qinghai na Sichuan. Marafiki zangu wengi walinishauri nifike hapa, ninapenda hapa Shangri-la, hapa si tofauti sana na kwetu Nepal."
Baada ya kutoka Aruokangba, "Dukezong" bado ilikuwa na shughuli nyingi wakati wa usiku. Kwenye uwanja wa mji huo wa kale, watu walikuwa wakiimba na kucheza ngoma, ambapo sisi tulijiunga nao na kuanza kucheza kwa kuwaiga.
Idhaa ya kiswahili 2007-09-24
|