Wafanyakazi wa Idhaa ya Kiswahili ya CRI
China Radio International
China
Dunia
(GMT+08:00) 2007-09-27 15:18:43    
Ndoto ya mtu anayejitolea kwenye michezo ya Olimpiki Bi. Meng Xiaoyan

cri

Bi. Meng Xiaoyan mwenye umri wa zaidi ya miaka 30, ni mfanyakazi wa sheria, lakini anashikilia kufanya kazi ya kutoa huduma kwa kujitolea.

Bi. Meng Xiaoyan anatoka mkoa wa Guangxi. Baada ya kuhitimu kutoka Chuo kikuu cha Beijing mwaka 2004, alifanya kazi katika shirika moja la kutoa misaada ya kisheria. Yeye pia alijiandikisha kuwa mmoja kati ya watu wanaojitolea kwenye michezo ya Olimpiki.

Bi. Meng aliamua kuwa mtu anayejitolea kutokana na moyo wake mzuri wa kupenda kutoa mchango kwa jamii. Mwaka 1996 wakati alipokuwa mwanafunzi wa mwaka wa pili katika kitivo cha sheria cha Chuo kikuu cha Beijing, alitoa fedha za udhamini wa masomo alizopewa chuoni kwa watoto wa maskani yake. Watu wengi hawakuwezi kumwelewa, hali ya kiuchumi ya familia yake siyo nzuri, lakini kwa nini aliweza kufikiria kwanza kuwasaidia wengine wakati alipopata fedha za udhamini wa masomo?Bi. Meng alisema:

"nilipopata fedha za udhamini huo wa masomo, nilitaka kutumia fedha hizo kuwasaidia watoto wa maskani kwangu. Kwa sababu wakati nilipokuwa mtoto, hali ya kiuchumi ya familia yangu haikuwa nzuri, kwa hivyo ninataka kutoa msaada kwa watoto ambao hali yao inafanana na hali yangu utotoni. Siku zote nina matumaini ya kufanya shughuli kadhaa ili kuwasaidia watoto hao."

Baada ya mwaka 1999 Bi. Meng Xiaoyan alipohitimu kutoka Chuo kikuu cha Beijing, alifanya kazi katika shule ya sekondari ya wilaya ya Xin mkoani Henan kwa mwaka mmoja. Huu ulikuwa ni mwanzo kwake kutoa wa huduma za kujitolea.

Katika muda wake wa mwaka mmoja kwenye Wilaya hiyo, alitumia njia mbalimbali ili kuwasaidia watoto wa huko kuongeza kujiamini na kuinua uwezo wao. Baada ya miaka kadhaa, wanafunzi 10 wa Bi. Meng waliandikishwa kwenye vyuo vikuu vya mjini Beijing . Alipozungumzia kuhusu wanafunzi hao alisema:

"Ni jambo linalofurahisha kuwa tunaweza kuwasaidia watoto wa sehemu zilizoko nyuma kimaendeleo, na kuwasaidia kuongeza nia."

Baada ya kurudi Beijing, Bi. Meng alianzisha kazi yake ya kutoa misaada ya kisheria. Alisema wakati alipofanya kazi mkoani Henan, aliona umuhimu na thamani ya kazi za kujitolea, hii pia ni sababu kubwa iliyomfanya yeye ajiandikishe kuwa mtu anayejitolea kwenye Michezo ya Olimpiki ya Beijing.

Mwaka kesho Michezo ya Olimpiki ya Beijing itafunguliwa. Kazi za kutafuta watu wanaojitolea kwa ajili ya Michezo ya Olimpiki ya Beijing na Michezo ya Walemavu ya Olimpiki ya Beijing zinaendelea kufanyika. Michezo hiyo miwili inahitaji watu laki 1 wanaojitolea kwa ajili ya michezo na kuhitaji watu laki 4 wanaojitolea kwa ajili ya kutoa huduma mijini. Watu wanaojitolea kwa ajili ya michezo watatoa huduma katika viwanja vya michezo na watu wanaojitolea wa mijini watatoa huduma katika sehemu nyingine za mijini. Wote ni muhimu sana. Kila mtu anayejitolea anapaswa kuwa na moyo wa usawa na kujitolea wakati watakapotoa huduma katika Michezo ya Olimpiki ya Beijing. Bi. Meng alisema:

"kushiriki kwenye michezo hiyo, kunatubidi kufanye shughuli zote kwa makini hata kama ni shughuli ndogo. Michezo ya Olimpiki ya mwaka 2008 sio tu inaleta fursa mbalimbali za biashara kwa Beijing, bali pia inaweza kuinua sifa na elimu ya wakazi wa Beijing kwa kupitia kuandaa michezo hiyo, na watu wanaojitolea wa mijini wanaweza kutoa mchango mkubwa katika kuwasaidia wakazi kuongeza nia ya kuhudumia jamii."

Idhaa ya kiswahili 2007-09-27