Wafanyakazi wa Idhaa ya Kiswahili ya CRI
China Radio International
China
Dunia
(GMT+08:00) 2007-10-02 19:44:40    
Viwanda vya serikali vya China vyaharakisha kubana matumizi ya nishati na kupunguza utoaji wa majitaka na hewa chafu

cri

Katika miaka ya hivi karibuni, uchumi wa China umekuwa unaendelezwa kwa kasi, lakini migongano kati ya maendeleo ya uchumi na mazingira pia imekuwa inaonekana siku hadi siku. Ili kutatua migongano hiyo, China imeweka lengo la kipindi cha kati la kubana matumizi ya nishati na kupunguza utoaji wa majitaka na hewa chafu, ili kutimiza maendeleo endelevu ya uchumi na jamii. Vikiwa nguvu muhimu za kuhimiza uchumi wa China, viwanda vikubwa vya serikali vya China vinaitikia mwito wa serikali, na kuharakisha hatua za kubana matumizi ya nishati na kupunguza utoaji wa majitaka na hewa chafu.

Kwa mujibu wa lengo la serikali ya China, hadi mwaka 2010, matumizi ya nishati ikilinganishwa na pato la taifa la China yatapunguzwa kwa asilimia 20 kuliko mwaka 2005, na utoaji wa majitaka na hewa chafu utapunguzwa kwa asilimia 10. Ili kutimiza lengo hilo, China imeanza kufanya harakati za watu wote kubana matumizi ya nishati na kupunguza utoaji wa majitaka na hewa chafu. Mwaka jana, matumizi ya nishati ikilinganishwa na pato la taifa la China yalipunguzwa kwa mara ya kwanza baada ya mwaka 2003, na ongezeko la utoaji wa majitaka na hewa chafu lilipunguzwa. Katika nusu ya kwanza ya mwaka huu, matumizi ya nishati ikilinganishwa na pato la taifa la China yalipunguzwa kwa karibu asilimia 3, ambayo yamedumisha hali ya kupungua kwa miezi 12mfululizo, na kuimarisha hali nzuri ya kupunguza matumizi ya nishati.

Mwishoni mwa mwezi Agosti, naibu mkurugenzi wa kamati ya maendeleo na mageuzi ya China Bw. Xie Zhenhua aliposhiriki kwenye mkutano kuhusu kubana matumizi ya nishati na kupunguza utoaji wa majitaka na hewa chafu alisema, hivi sasa hatua mbalimbali za kubana matumizi na kupunguza utoaji wa majitaka na hewa chafu zinazochukuliwa na China zinafanya kazi, lakini hali ya kubana matumizi na kupunguza utoaji wa majitaka na hewa chafu ya China bado ni ngumu. Aliona kuwa ni lazima kufanya kazi ya kubana matumizi ya nishati na kupunguza utoaji wa majitaka na hewa chafu kuwa njia muhimu ya kurekebisha muundo wa uchumi na kubadilisha njia ya kupata ongezeko la uchumi, na kuimarisha kazi hiyo.

"Hivi karibuni tutahimiza kazi hizo: kwanza tutaimarisha utaratibu wa kukagua utekelezaji wa lengo na majukumu ya kazi ya kubana matumizi ya nishati na kupunguza utoaji wa majitaka na hewa chafu; pili ni tutazuia kithabiti viwanda vinavyotumia nishati kwa wingi na kutoa majitaka na hewa chafu kwa wingi visiongezeke kwa kasi; tatu ni kuimarisha nguvu za kuchuja uzalishaji uliopitwa na wakati; nne ni kuharakisha kutekeleza miradi ya kubana matumizi ya nishati na kupunguza utoaji wa majitaka na hewa chafu; tano ni kusimamia vizuri viwanda na makampuni makubwa kubana matumizi ya nishati na kupunguza utoaji wa majitaka na hewa chafu."

Bw. Xie Zhenhua aliona kuwa viwanda na makampuni ya China ni lazima yawe nguvu muhimu ya kubana matumizi ya nishati na kupunguza utoaji wa majitaka na hewa chafu. Alidokeza kuwa mkutano wa kubana matumizi ya nishati na kupunguza utoaji wa majitaka na hewa chafu wa viwanda 1,000 vikubwa nchini China utafanyika mwezi Septemba, ili kuhimiza viwanda hivyo vibane matumizi ya nishati na kupunguza utoaji wa majitaka na hewa chafu. Aliona kuwa, kama viwanda hivyo vitamaliza majukumu yao, basi nusu ya majukumu yote ya viwanda kubana matumizi ya nishati na kupunguza utoaji wa majitaka na hewa chafu yatakamilishwa.

Kwa kweli viwanda vingi vya taifa la China vinatia maanani sana kazi ya kubana matumizi ya nishati na kupunguza utoaji wa majitaka na hewa chafu. Kampuni ya aluminium ya China ni kampuni kubwa kabisa ya China ya madini yasiyo ya chuma, naibu meneja mkuu wa kampuni hiyo Bw. Lu Youqing alifahamisha kuwa, ili kampuni hiyo idhibiti matumizi makubwa ya maji kiwandani na kudumisha kiwango cha chini cha matumizi ya maji kwa mfululizo, kampuni yao inatumia teknolojia ya kisasa, na kutimiza kutotoa majitaka ya viwanda. Alisema,

"Mwaka 2006, kiwango cha kutumia kwa mfululizo maji viwandani kilifikia asilimia 88, mwaka huu matumizi ya maji katika uzalishaji bidhaa wenye thamani ya Yuan za RMB elfu 10 yatapungua kwa asilimia 35 kuliko mwaka 2005, na viwanda vingi vinatimiza matakwa ya kutotoa majitaka ya viwanda."

Pia alisema ikinganishwa na uzalishaji vifaa vya aluminum kwa kutumia mawe ya madini, matumizi ya nishati kwa kutumia takataka za aluminum yanaweza kupungua kwa asilimia 95, na kutumia takataka za aluminum pia kunaweza kupunguza kwa kiasi kikubwa utoaji wa hewa ya carbon dioxide inayosababisha kuongezeka kwa hali joto. Hivyo kampuni hiyo inaendeleza uzalishaji wa vifaa vya aluminium kwa kutumia takataka za aluminum, hivi sasa ujenzi wa mradi huo unaendelea.

Wataalam wanasema, viwanda vikubwa vya serikali vya China kubana matumizi ya nishati na kupunguza utoaji wa majitaka na hewa chafu, sio tu kunatoa mchango katika kuboresha mazingira ya raslimali, bali pia ni njia muhimu ya kuinua ufanisi wao, kupunguza gharama na kuimarisha nguvu ya ushindani katika kimataifa. Naibu meneja mkuu wa kampuni ya aluminum ya China Bw. Lu Youqing alisema, kazi ya kubana matumizi ya nishati na kupunguza utoaji wa majitaka na hewa chafu inayanufaisha sana makampuni. Alisema

"Kufanya kwa kina kazi za kubana matumizi ya nishati na kupunguza utoaji wa majitaka na hewa chafu na matumizi ya raslimali, sio tu kunaifanya kampuni ipige hatua mpya katika kazi ya kubana matumizi ya nishati na hifadhi ya mazingira, bali pia kunaifanya kampuni iinue kiwango cha usimamizi na sifa ya maendeleo katika mchakato wa kujikagua, kugundua makosa na kuboreshwa kwa mfululizo, na kutimiza kuboreshwa kwa mfululizo kwa vigezo vya teknolojia na sifa ya bidhaa kuinuka kwa hatua madhubuti."

Bw. Lu Youqing alisema, kampuni ya aluminium ya China itashirikiana na viwanda vingine vikubwa vya serikali, ili kuhimiza maendeleo ya viwanda, na kutoa mchango kwa jamii.