Tarehe 10, mwezi Septemba ilikuwa ni siku ya walimu. Habari kutoka wizara ya elimu ya China zinasema, katika miaka ya hivi karibuni, China imekuwa inaimarisha kazi ya kuandaa walimu hasa wa vijijini, ili kuboresha hali ya nguvu za walimu vijijini na kuinua uwezo wao wa ufundishaji. Maofisa wa wizara ya elimu wa China wanasema katika siku za usoni serikali ya China itaendelea kuinua kwa nguvu uwezo wa ufundishaji wa walimu vijijini.
Kutokana na kutokuwepo kwa uwiano kwa maendeleo ya uchumi na jamii ya sehemu mbalimbali, mahitaji ya walimu vijijini ni makubwa, na walimu wanaofundisha lugha za kigeni, teknolojia na habari, muziki na uchoraji wanahitajika sana, kiwango cha sifa za ufundishaji kinatakiwa kuinuka, mapato ya walimu na kiwango cha maisha yao ni ya chini. Kwa hivyo katika miaka ya hivi karibuni serikali imekuwa inachukua hatua kadhaa kama vile kutenga fedha zaidi kwa ajili ya vijijini, kutuma walimu wengi wazuri kwenda kufundisha vijijini kwa muda, kuwaandaa walimu wa vijijini na kuimarisha utaratibu wa kupeleka walimu wa vijijini.
Mkuu wa idara ya elimu kwa walimu ya wizara ya elimu ya China Bw. Guan Peijun alitufahamisha akisema,
"kuinua zaidi hadhi na mapato ya walimu wa vijijini, kuboresha mazingira yao ya maisha na kazi, kuongeza nguvu za ushindani za ualimu, kuvutia watu wengi wenye ujuzi kwenda kufundisha vijijini, ni malengo ya idara hiyo kwa sasa."
Wakati huo huo, serikali pia iliweka nafasi maalumu kwa ajili ya walimu kwenda kwenye vijiji vya magharibi, kuhimiza wanafunzi waende kwenye vijiji vya magharibi kufundisha baada ya kuhitimu kwenye vyuo vikuu. Hivi sasa wanafunzi elfu 20 hivi waliohitimu kwenye vyuo vikuu wamekwenda kufanya kazi kwenye shule za msingi na shule za sekondari zaidi 2800 za sehemu magharibi mwa China, hatua hii imepunguza hali ya upungufu wa walimu kwenye vijiji vya magharibi mwa China.
Hivi sasa, vijiji vya China vina walimu wengi wazuri, nguvu za walimu zimeinuka sana. Idadi ya walimu kutoka vijijini waliopewa tuzo kabla ya siku ya walimu inaongezeka mwaka hadi mwaka.
Bw. Yang Xiaosheng ni mwalimu wa somo la fizikia kwenye shule ya sekondari ya kijiji kimoja mkoani Shanxi, ambaye alitunukiwa na serikali ya China mwaka huu. Katika miaka yake 20 ya kufundisha, alifanya utafiti wa mageuzi ya njia ya kufundisha somo la fizikia, na kuwaandaa wanafunzi kuwa na uwezo wa kufikiri wao wenyewe. Alisema kuwa,
"ujuzi wa fizikia unahitaji uwezo wa kufikiria, kama nikifundisha kwa kufuata vitabu, wanafunzi watasahau mara moja baada ya kutoka darasani, na wanafunzi hawawezi kupata ujuzi. Fizikia ni sayansi ya majaribio na sayansi ya maisha, hivyo nilitafuta masuala kutokana na maisha ya kawaida, na kuwafundisha wanafunzi kuchunguza na kupata ujuzi wa fizikia, na wanafunzi wangu wanapenda kujifunza.
Hivi karibuni, China imekuwa inaimarisha zaidi kazi ya kuwaandaa walimu wa vijijini. Rais Hu Jintao wa China hivi karibuni alisema China itatilia mkazo zaidi na kuimarisha halisi kazi ya kuwaandaa walimu, kuvutia na kuhimiza watu wenye ujuzi kufanya kazi ya ualimu, kuwatia moyo vijana kwenda vijijini na sehemu nyingine zinazowahitaji kutoa mchango kwa ajili ya maendeleo ya shughuli za elimu ya taifa.
Habari kutoka wizara ya elimu ya China zinasema, China itaongeza kutenga fedha kwa ajili ya kuwaandaa walimu, kutekeleza mradi mpya wa kuwaanda walimu wa vijijini, ili kuinua zaidi kiwango cha ufundishaji wa walimu vijijini.
Idhaa ya kiswahili 2007-10-11
|