Wafanyakazi wa Idhaa ya Kiswahili ya CRI
China Radio International
China
Dunia
(GMT+08:00) 2007-10-09 16:33:28    
Barua 1009

cri

Tamasha la 7 la maonesho ya sanaa duniani lilifanyika huko Suzhou, mashariki ya China kuanzia tarehe 25 Septemba hadi tarehe 1 Oktoba. Tamasha hilo liliandaliwa na Shirikisho la wasanii na wafasihi wa China na Serikali ya umma ya Mkoa wa Jiangsu na kuendeshwa na serikali ya umma ya Suzhou mkoani Jiangsu, Shirikisho la wasanii wa China na idara nyingine.

Bendi ya Sisi Tambala ya Tanzania ilikuja China kushiriki kwenye tamasha hilo. Mimi nikiwa mwandishi wa habari nilikwenda Suzhou kuwahoji wasanii hao kutoka Tanzania. Walipokutana na mimi mchina anayejua kuongea kwa Kiswahili walifurahi sana wakaimba wimbo kueleza furaha yao.

Kiongozi wa Bendi hiyo ya Sisi Tambala ya Tanzania Bwana Kibiriti Kijuja aliniambia kuwa, hii ni mara yao ya kwanza kuja China, na walifurahi kupata fursa ya kushiriki kwenye tamasha hilo, alisema:

Kwanza tumepata kutoka upande wa China, wao wachina tumeona wanathamini sana utamaduni wao. Tumeona hivyo kwa lugha, tumeona kwa vyakula, tumeona hata kwa michezo, na ngoma na muziki, sisi watanzania tumejifunza utamaduni wenu kumbe tumeona kuheshimu utamaduni wa taifa na muziki wa taifa ndiyo fahari?na ndiyo heshima.

Mwandishi wetu wa habari alimwuuliza kuwa bendi yao ni ya kisasa au ni ya kijadi, kiongozi wa bendi hiyo Bwana Kijuja alisema:

Bendi hiyo ya Sisi Tambala inapiga muziki wa kisasa ambao umebuniwa vilevile kwa vionjo vya kijadi vya Tanzania, ikipiga muziki wa kisasa kwa ajili ya kuwavutia watu wengi wa sasa kwa sababu ni watu wanaoweza kuendeleza na kupokea utamaduni. Wazee wetu pia hatukuwaacha, maana tumeenzi vionjo vyetu kwenye muziki wetu, hatutaki kupoteza utamaduni wetu. Lakini kwa ajili ya kutafuta soko letu ili kazi zetu ziweze kukubaliwa na wengine duniani, hatutaki kupiga muziki sisi wenyewe kwa wenyewe tu, tunataka muziki wetu uwe vitu vya kuvutia na kuwawezesha watu wa duniani waijue Tanzania. Na zile asili hatuondoi, watu watakaosikia ndani zaidi ni vionjo vya asili vya Tanzania, yaani ngoma zetu za asili tunalinda sana na tunatunza sana utamaduni wetu wa asili, tunapiga muziki wa kisasa, lakini undani wake ni muziki wa kijadi.

Mwandishi wetu wa habari alimwuliza kuwa, safari yao hii nchini China inaweza kuwasaidia wananchi wa China wajue zaidi mambo ya Tanzania au la? Bwana Kijuja alisema:

Kweli tamasha hili ni jukwaa la mawasiliano, tunashukuru waandaji wa tamasha hilo kupitia Kamati ya mfuko wa utamaduni wa Tanzania, kumpitia Mama Sayore kupokea kazi yetu, walisema wanapenda kazi yetu na kutuambia tuje, nafasi hii ni kubwa sana na pan asana kwa kutangaza utamaduni wa Tanzania, ni nafasi kubwa sana kwa wachina kupata habari za Tanzania kuhusu utamaduni wa Tanzania, kwa kuona tamsha hili, kwa watu wanaoshiriki tamasha hili au wengine wanaotazama kwenye televisheni kuhusu hali ya utamaduni wa Tanzania, bendi hiyo Sisi Tambala, hili la asili kuenzi fani hii ya muziki, ngoma, muziki walibuni mabu zetu lakini vilevile Tambala ni lugha ya kabila la kiyao la kusini mwa Tanzania, wanaoishi Luvuma, Tunduru, tambala ni shujaa, jogoo, kama sisi hatujaweza kutangaza utamaduni wetu, mimi ni msanii wa muziki lazima tutangazet utamaduni wetu kwa muziki ni mtu mwingine kutangaza utamaduni wetu kwa kupitia fani yake, mimi naweza kupiga muziki tu, kwa sababu hauna utambulisho halisi wa kitanzania tuna ngoma zetu nyingi, sisi tambala tunatangaza utamaduni wetu katope.

Idhaa ya kiswahili 2007-10-09