Wafanyakazi wa Idhaa ya Kiswahili ya CRI
China Radio International
China
Dunia
(GMT+08:00) 2007-10-11 17:00:02    
Somo la hifadhi ya mazingira ya asili kwenye uwanda wa juu

cri

Mkoa wa Qinghai ulioko kwenye sehemu ya magharibi ya China, unajulikana duniani kwa "water tower" (mnara wa maji) wa bara la Asia, ziwa la Qinghai pamoja na vyanzo vya mito mitatu mikubwa ya Changjiang, Manjano, Lancang vina athari ya moja kwa moja maisha ya karibu nusu ya idadi ya watu wa dunia. Katika miaka ya hivi karibuni serikali katika ngazi mbalimbali pamoja na watu wa China walitenga nguvukazi na vitu vingi kwa ajili ya marekebisho na hifadhi ya mazingira ya sehemu hiyo, hivi sasa mazingira ya viumbe ya mkoa wa Qinghai yameboreshwa kwa udhahiri. Hivi karibuni mwandishi wetu wa habari alifanya matembezi kwenye mkoa wa Qinghai na kutengeneza mfululizo wa vipindi vya "Masikilizano kati ya binadamu na mazingira ya kimaumbile mkoani Qinghai". Leo tunawaletea kipindi cha nne cha "somo la hifadhi ya mazingira ya asili kwenye uwanda wa juu".

"Lo, nilidhani wewe ni mkubwa mno, itakuwa haidhuru hata kama inakatwa miti mingi, kumbe unatokwa na machozi; Dunia, maskani yetu wa kipekee, tunakupenda milele; Dunia, mama yetu, tubarikiwe na wewe."

Wasikilizaji wapendwa, sauti mliyokuwa mkisikiliza ni shairi lililosomwa na wanafunzi wa shule ya msingi ya Bendera Nyekundu katika tarafa ya Jiegu, wilaya inayojiendesha ya kabila la watibet ya Yushu, mkoani Qinghai, magharibi mwa China, wakati waandishi wetu wa habari walipoitembelea shule hiyo, kichwa cha shairi hilo ni "Dunia mama yetu".

Wilaya inayojiendesha ya kabila la watibet ya Yushu iko kwenye vyanzo vya mto Changjiang, mto Manjano na mto Lancang, mazingira ya viumbe ya huko ni dhaifu kutokana na kuathiriwa na hali ya kijiografia ya uwanja wa juu, hivyo kuhifadhi mazingira ya asili kumekuwa sehemu muhimu ya maisha ya wakazi wa huko. Kujishughulisha kutoka utotoni ni moja ya hatua muhimu inayochukuliwa na serikali ya wilaya ya Yushu ya kuinua mwamko wa umma wa kuhifadhi mazingira ya asili.

"Katika shule ya msingi ya Bendera Nyekundu, wanafunzi wa vidato mbalimbali huwa wanafundishwa masomo ya hifadhi ya mazingira. Msichana wa kabila la watibet anayeitwa Suonanbaji anayesoma kidato cha tano, anasifiwa kama ni "mlinzi mdogo wa hifadhi ya mazingira", msichana huyo mdogo anajivunia sana sifa hiyo, alimwambia mwandishi wetu wa habari, akisema,

"Tumeanzisha shughuli za 'kutunza raslimali ya maji, na kuupenda mto mama'. Tunategemea sana mazingira yetu, endapo mazingira ya asili yanaharibiwa, basi maskani yetu yatateketea kabisa. Ninajivunia sana kutokana na kuweza kutoa mchango wangu kwa vyanzo vya mito mitatu. Sisi tuko kwenye vyanzo vya mito mitatu, na tuko kwenye mtiririko wa mwanzo. Endapo sehemu hiyo ya mtiririko wa mwanzo inachafuliwa, sehemu ya mtiririko wa chini pia itachafuka."

Msichana Chen Jingying alipowaona waandishi wetu wa habari wakifanya mahojiano huko, alikwenda na kuwaeleza waandishi wetu wa habari shughuli zake za kuhifadhi mazingira. Alisema,

"Niliwaambia baba na mama, wasitupe ovyo mifuko ya plastiki, mifuko ya plastiki pia ni vitu vya kuchafua mazingira ya asili, inajulikana kama vitu vyeupe vya kuchafua mazingira, kwani vitu hivyo ni vigumu sana kuoza."

Hii ndiyo moja ya malengo ya waenezaji wa ufahamu wa kuhifadhi mazingira ya asili, watoto si wa kupewa ufahamu kuhusu hifadhi ya mazingira, bali pia ni waenezaji wa ufahamu wa kuhifadhi mazingira, wakati wanapojifunza ufahamu wa hifadhi ya mazingira na kutenda vitendo, pia wanaeneza ufahamu wa hifadhi ya mazingira kwa wazazi, marafiki na watu walioko karibu nao.

Mtu aliyekabidhiwa jukumu la kutoa masomo ya hifadhi ya mazingira kwa wanafunzi wa shule hiyo ya msingi, ni ofisa katika mradi wa uelimishaji wa mazingira wa jumuiya ya hifadhi ya mazingira ya viumbe ya vyanzo vya mito mitatu Bi. Zhuomaqingshui, aliwaeleza waandishi wetu wa habari kuwa jukumu kubwa katika mradi huo wa "malezi ya kijani" ni kufungua masomo rasmi ya ufahamu wa hifadhi ya mazingira katika shule tano za msingi za tarafa ya Jiegu, baadaye mradi huo utapanuliwa hadi kwenye shule zote za tarafa ya Jiegu, vilevile utapanuliwa hadi kwenye wilaya nyingine, na hatimaye hadi kwenye sehemu zote za vyanzo vya mito mitatu.

Dada Zhuomaqingshui alitoka Hong Kong, China, na alifanya kazi za kujitolea kwa miezi 9 katika jumuiya ya kuhifadhi mazingira ya viumbe ya vyanzo vya mito mitatu. Kabla ya hapo alifundisha masomo yanayohusu mazingira ya kimaumbile kwa zaidi ya miaka kumi huko Hong Kong. Aliwaambia waandishi wetu wa habari,

"Mazingira ya viumbe ya hapa ni dhaifu sana, na pia ni muhimu sana. Watu wengi wanamiminikia hapa kufanya utalii kama watu wanaokwenda kuhiji, lakini vitu wanavyoviona ni vya upande mzuri. Ninafanya kazi ya kufundisha somo la mazingira ya maumbile, kwa hiyo nina uchungu mwingi na maumbile. Nilifika hapa ni kufuatilia uzuri wa maumbile wa hapa, lakini mazingira ya hapa yanachafuliwa kwa kasi kila siku ipitayo, mimi ninataka kubadilisha hali hiyo.

Idhaa ya kiswahili 2007-10-11