Wiki chache zilizopita wafanyakazi wa vyombo vya habari kutoka nchi mbali mbali za Afrika,walikuja hapa Beijing, kwenye mafunzo ya muda mfupi.
Mmoja kati ya hao ni Bw.Edmond Msambazi kutoka taasisi ya Utangazaji nchini Tanzania, ambaye tulipata nafasi ya kuzungumza naye.Kwanza Bw. Edmond anazungumzia jinsi anavyoiona China.
Edmond:
China jinsi inavyoonekana na nilivyokuwa nasikia,kwa ujumla kwanza unajua kitu ulichokuwa unasikia unaweza kuwa unakiweka kwenye mawazo,akilini lakini unashindwa kuki define yaani kukiweka katika hali ambayo unajua kwamba ukweli uko hapa,sasa utakapokiona ndiyo unasema aah hivi kumbe yale mawazo niliyokuwa nayo kumbe tofauti.
Lakini kwa ujumla kwa kweli China ninavyoiona siyo ya kawaida,siyo ya kawaida kwa sababu nasema siyo ya kawaida unalinganisha na kule ambako umetoka au na sehemu ambazo umefika eeh hasa ndiyo hali halisi nayoona kwa kweli wenzetu wako mbali,wako mbali.
Fadhili:
Ni maeneo gani ambayo labda yamekufanya utambue kama wako mbali ambayo umeyaona kwa haraka haraka?
Edmond:
Kwa haraka haraka kwanza tu baada ya kufika, miundo mbinu tukisema miundo mbinu,unaangalia kwanza barabara jinsi zilivyo,halafu unaangalia mawasiliano mengine,halafu unaangalia hata baadhi ya vitu ambavyo unaweza ukawa unaviona mahali ambako utakuwa unapita.
Fadhili:
Nafahamu kwamba umekuja kwenye mafunzo ya.. mafunzo mafupi.Sijui ni mambo gani hasa ambayo mnajifunza na unaona mambo hayo yanakusaidia vipi wewe ukirudi nyumbani Tanzania?
Edmond:
Aah mambo ambayo tunajifunza hapa kwa mfano najifunza kuhusu mambo ya Radio na Televisheni broadcasting wanaita Technics.Sasa ukweli ni kwamba kuna mambo ambayo kwangu ni mapya,lakini mengine yapo.
Ila naona ni mpya kwa sababu wenzetu vifaa vyao ni vya kisasa zaidi, kuliko ukilinganisha na sisi, kwahiyo lakini mfumo wa matangazo ni ule ule mmh.
Fadhili:
Kwahiyo unaona kabisa kuna mapya ambayo ukirudi nyumbani yatakusaidia labda kwenye kazi zako?
Edmond:
Eeh ni kweli,kama jinsi nilivyokwambia toka mwanzo ukiangalia wenzetu walipo na sisi, wenzetu wako mbali eeh kwahiyo ina maana hivi ninavyovipata hapa nafikiri vitanisaidia zaidi nitakapokuja kurudi nyumbani.
Fadhili:
Na vile vile matangazo ya Radio China Kimataifa kwa upande wa Tanzania yamekuwa hayasikiki vizuri na tume..kumekuwa na juhudi ambazo zinafanyika kati ya watu,kwa mfano Taasisi ya Utangazaji ya Tanzania unakotoka na hapa Radio China Kimataifa,sijui labda wewe unaonaje kuna uwezekano wa kufanya ushirikiano ili kuboresha matangazo wasikilizaji wengi zaidi watanzania wasikilize?
Edmond:
Aah hicho unachozungumza ni kweli kwa sababu kuna kipindi china ilikuwa inasikika vizuri sana, Tanzania lakini, sasa hivi kidogo kuna matatizo kidogo,lakini hasa kwa ushirikiano ambao nauona sasa hivi kwa mfano mimi ni kundi la pili la watu kutoka Tanzania ambao wamekuja hapa.
Sasa kwa ujumla tunajifunza mambo haya haya ya broadcasting,ukilinganisha na mwanzo sidhani kama kulikuwa na kitu kama hichi sasa unakuta kwamba kile ambacho wenzentu wanakifanya sasa ukikipata na wewe ukaenda kukifanyia kazi yale mapungufu ambayo ulikuwa nayo yanaweza yakasaidia usikivu zaidi. Eeh labda kwa mfano tu hivi karibuni wakati naondoka, mfano kwa sisi tulikuwa tunafunga mitambo ambayo itakuwa inapita kwenye satelaiti ambayo nimeacha wenzangu wanaendelea nafikiri nayo hiyo na sisi inaweza kutusaidia kusikika ulimwengu nzima, sasa labda tu kwa wenzetu wa hapa china nao labda huenda sijaelewa jitihada zao za kuweza kufanya na sisi tukaweza kusikia vizuri zaidi tofauti na kama ilivyokuwa mwanzo mmh.
Fadhili:
Lakini unaonaje tukiwa na ushirikiano wasikilizaji wetu wa kule Tanzania wanaweza kusikiliza vizuri zaidi matangazo?
Edmond:
Watasikiliza vizuri matangazo ya china kwa sababu toka mwanzo kwa sababu hii idhaa ya Kiswahili ilikuwepo,watu walikuwa wanasikiliza na mimi nimeijua kwa sababu nilikuwa nasikiliza.
Sasa ni kwamba usikivu ukiimarishwa zaidi, ina maana wasikilizaji nao watakuwa wengi zaidi, kwa hiyo hata maoni mtayapata mengi zaidi.
Fadhili:
Kitu kingine ,watu wengi ambao wanakuja hapa china huwa wanashangazwa jinsi wachina walivyo kwa sababu siyo wengi ambao huwa wanawafahamu wachina,unajua wachina barani Afrika siyo wengi,labda nianze kwa kukuuliza toka ulipofika mpaka sasa mapokezi unayaonaje na jinsi unavyotendewa na wachina hapa china unaonaje?
Edmond:
Hali halisi ni kwamba bahati mbaya mimi kwa mara ya kwanza,tuseme ndiyo mara yangu ya kwanza kufika china.
Sasa nilipofika hapa china nilifika usiku, saa sita usiku na mahali nilipofikia sasa hivi ambapo naishi Zi Yu hotel ni mwendo wa saa moja kutoka uwanja wa ndege.Sasa nilipofika pale nilichofanya niliwauliza tu hoteli iko wapi, nikawapa namba yangu ya simu.
Kwahiyo nilikuja vizuri moja kwa moja mpaka pale hotelini nikampigia simu mhusika wangu akaja kunipokea nikawa nimeifadhiwa.
Ni kwamba ukweli wana ile hali ya ubinadamu tofauti na jinsi labda nilivyokuwa nafikiria labda huenda unaweza ukaenda ,unajua kuna baadhi ya nchi ukienda kuna ule ujanja ujanja fulani hivi kwa mfano ukiwa mgeni wanaweza wakakupitisha mahali siyo penyewe ili tu angalau waongeze pesa, lakini walinileta straight mpaka kwenye ile hoteli niliyotakiwa kufikia na kufika pale wakaniambia bwana wewe mahali ambapo ulitakiwa kufikia ni hapa,sasa mambo mengine unaweza kuendelea nao.
Nashukuru walinifikisha salama,kwahiyo nilichokifanya pale nilimpigia simu mhusika wangu mkuu akaja pale akaniona,kwahiyo nikiwa nimepokelewa vizuri na naendelea na mambo yangu vizuri,kwa kweli huduma zao na hata shughuli iliyonileta hapa kwa kweli haina matatizo na kwenda nayo vizuri kwahiyo kwa kweli ni watu wakarimu na jinsi nilivyokuwa nafikiri na nafikiri nimejifunza mengi sana kuhusu hawa watu kwa sababu ukarimu walionao ni kwamba hata Afrika tunao kuna baadhi ya nchi kweli hiki kitu kinakuwepo kuna baadhi sehemu ambazo unaweza ukatembelea unaweza kukuta kwamba kuna tofauti kidogo lakini hawa wenzetu ukarimu wanao,ukarimu wanao na nashukuru kwa kitu walichonitendea mpaka sasa hivi kwa kweli sijapata kikwazo chochote cha kunifanya mimi nishindwe kukipata kile ambacho nimekifuata hapa.
Fadhili:
Na vile vile kumekuwa na picha tofauti, watu wengi wa bara la Afrika wanaifahamu china labda hasa kwa kupitia vyomba vya habari vya magharibi, labda Televisheni au labda Radio za mgharibi,kwa sababu nyingi labda kwa mfano zinatumia lugha za kiingereza na watanzania na labda wakenya na watu wengine wanaopata habari kupitia katika vyombo hivi vya kiingereza wanakuwa na picha tofauti ya hali halisi iliyopo hapa china sasa sijui wewe picha uliyokuwa nayo pale wa mwanzo kuhusu china labda kama uliipata kupitia katika vyombo vya magharibi na hii unayoiona sasa hivi unaona kuna tofauti au kuna kufanana?
Edmond:
Ni kwamba kama jinsi nilivyokuwa nimesema kwa kweli unajua picha unayokuwa unaihisia kichwani tofauti na vile utakavyoona.Sasa kwa kweli nilivyokuwa na nafikiria na nilivyoona ni vitu viwili tofuati.
Ni kwamba halisi niliyoiona ni tofauti na nilivyokuwa nafikiri,sasa siwezi nikachukulia yale mawazo niliyokuwa nafikiria nikayaeleza hapa ni kwamba ninachotaka kusema tu ni kwamba china wenzetu kwa ukarimu wanao halafu hata kwa upande wa teknolojia wenzetu wako,wako mbali ukweli ni kwamba hatuwezi tukajilinganisha na sisi,hatuwezi tukajilinganisha na sisi.
Aah kwa mfano nilipofika mimi hapa sasa wengi baada ya kufika, hata baadhi ya watu niliokuja nao kutoka nchi nyingine za Afrika baada ya kusema mimi natoka Tanzania,mimi mpaka sasa hivi pale wananiita mwalimu,mwalimu kwa sababu wanamfahamu sana mwalimu Nyerere unaona eeh kwahiyo mimi wananifahamu mwalimu,Tanzania ndivyo wanavyoniita kwahiyo wakiniona tu mwalimu ,mwalimu kwa sababu mwalimu ndiyo wanayemfahamu zaidi,kwahiyo unakuta kwamba hata hawa wachina ninapoongea nao nikishaongea nao Tanzania wanaifahamu zaidi kwa ukarimu.
Idhaa ya kiswahili 2007-10-18
|