Bibi Tuoya ni mmoja wa wanawake wa kabila la wamonglia wanaoishi kwenye mbuga ya Xilinguole, yeye ana umri wa miaka 30. Kila siku anafanya shughuli sawa sawa. Akisema:
"ninaamka saa 11 alfajiri, halafu ninaanza kuandaa kifungua kinywa kwa jamaa zangu. Mchana huwa ninakamua maziwa ya farasi kila baada ya saa mbili, mara 6 kwa siku."
Bibi Tuoya alikuwa amezoea kazi hizo za nyumbani kabla ya kuolewa. Sasa anapaswa kumtunza bin yake mwenye umri wa miaka 6, na kufanya kazi za nyumbani kila siku.
Kwa kawaida wanawake wa kabila la wamongolia hawakupendi kwenda nje ya nyumbani, lakini sasa hali imebadilika. Kutokana na maendeleo ya uchumi wa sehemu hiyo nakuinuka kwa kiwango cha elimu waliyopata watu wa sehemu hiyo, wanawake wengi zaidi wanashiriki katika shughuli za uzalishaji zinazohusu mifugo, na baadhi ya wanawake wamepata mafanikio katika shughuli nyingine. Katika sehemu ya Xilinguole, wanawake wawili wamekuwa maofisa wa kijiji cha Erdeng Baolige.
Mkuu wa kijiji hicho ni Bibi Erdeng Gerile. Na mkuu wa zamani wa kijiji hicho ni mume wa Bibi Erdeng Gerile. Katika uchaguzi wa kijiji hicho, wanakijiji walimchagua Bibi Erdeng Gerile kuwa mkuu mpya wa kijiji hicho badala ya mume wake.
Familia ya Bi. Erdeng Gerile ina watu watano, wakiwemo wakwe zake na mwanaye. Wamepewa eneo la malisho la zaidi ya hekta mia 6.
Katika sehemu hiyo majani na maji yanahusiana sana na mapato ya wafugaji. Ili kuhakikisha ng'ombe na kondoo wana malisho ya kutosha, familia ya Bi. Erdeng Gerile iliamua kugawanya malisho yao katika sehemu mbalimbali, na kuishi na kufuga mifugo katika sehemu tofauti kutokana na hali ya malisho na maji. Na familia yake pia imehamia katika sehemu hizo.
Kijiji cha Erdeng Baolige kilisaini mkataba na wanakijiji kuhusu kushughulikia malisho, wafugaji wa kijiji hicho wanatumia njia mwafaka ya usimamizi, ili kuinua kiwango cha maisha yao. Bi. Erdeng Gerile alitufahamisha kuwa,
"Mabadiliko ya kijiji chake yanaonekana dhahiri. Zamani, mapato yote yalikuwa ya ushirika, na sisi tulipata mishahara. Lakini sasa hivi hali imekuwa inabadilika, ukifanya kazi kwa bidii, utapata mapato mengi."
Familia ya Erdeng Gerile inafuga kondoo zaidi ya mia 4 na ng'ombe zaidi ya mia mbili. Mapato ya familia yake ya kila mwaka yanafikia renminbi laki moja kutokana na kuuza kondoo, ng'ombe na manyoya. Hii imekuwa ya kiwango cha katikati cha mapato ya sehemu hiyo.
Akiwa mkuu wa kijiji, Bi. Erdeng Gerile siyo tu anashughulikia kazi za kawaida, bali pia anazusaidia familia mbili za watu maskini kwenye kijiji chake. Alisema:
"Kwenye kijiji chetu, viongozi wanapaswa kusaidia familia moja au mbili za watu maskini. Tutawasaidia kuhusu usimamizi wa mambo ya kiuchumi, na wakati wa kuwasiliana nao tunajadiliana kuhusu mambo hayo."
Idhaa ya kiswahili 2007-10-18
|