Wafanyakazi wa Idhaa ya Kiswahili ya CRI
China Radio International
China
Dunia
(GMT+08:00) 2007-10-26 16:35:44    
Ushirikiano kati ya China na Afrika wafikia kiwango kipya cha juu

cri

Watu wenye umri wa miaka zaidi ya 40 nchini China wanapozungumia miradi ya ushirikiano kati ya China na Afrika, wengi wao hutaja reli ya TAZARA na madaktari wa China kwenye sehemu mbalimbali barani Afrika. Katika muda mrefu uliopita, Bw. Zhou Zhicheng mwenye umri wa miaka 44 alikuwa anaona Afrika ni bara lenye ukame na matatizo ya kiuchumi tu. Lakini maoni yake yalibadilika baada ya kushiriki kwenye mradi mmoja wa ushirikiano kati ya China na Afrika. Kwenye mradi huo, Bw. Zhou Zhicheng akiwa mhandisi mkuu, alibeba jukumu la kupanga na kutengeneza satellite kwa ajili ya Nigeria.

Bw. Zhou Zhicheng alisema baada ya satellite hiyo kurushwa kwa mafanikio na kupita majaribio nchini China mwaka 2007, alipata fursa ya kwenda Abuja, mji mkuu wa Nigeria kuikabidhi satellite hiyo kwa Nigeria. Bw. Zhou alisema Abuja ni mji mzuri, na watu wa upande wa Nigeria aliokutana nao wanapenda kujifunza. Bw. Zhou alisema nguvu ya uhai na nia imara ya nchi hiyo na wananchi wake vilimwachia kumbukumbu nzuri.

Mtaalamu wa Idara ya utafiti wa Asia ya magharibi na Afrika katika Taasisi ya sayansi ya jamii ya China Bw. Liu Naiya alisema, baada ya kutekeleza sera ya mageuzi na kufungua mlango kwa miaka 20, China imekuwa na uwezo wa kutoa vitu vinavyohitajiwa na nchi za Afrika, kama vile teknolojia zinazofaa kutokana na hali halisi za nchi za Afrika, teknolojia maalumu za kupunguza umaskini, na uzoefu wa kuendeleza uchumi.

Bw. Liu Naiya alisema, ikilinganishwa na teknolojia za nchi za magharibi, teknolojia ya China si ya mbele sana. Lakini China inaweza kutoa huduma kwa pande zote zaidi baada ya kutoa teknolojia. Ni muhimu sana kuwa China inapenda kukabidhi teknolojia kwa nchi za Afrika kuliko nchi za magharibi, na nchi za Afrika zinapenda kupokea bidhaa zenye teknolojia za China.

Bw. Zhou Zhicheng alisema, kutokana na makubaliano kati ya China na Nigeria kuhusu satellite, si kama tu China inashugulikia kupanga, kutengeneza na kurusha satellite, bali pia inabeba jukumu la kuanzisha vituo viwili vya kufuatilia satellite hiyo ardhini, na vilevile itatoa mafunzo kwa watu zaidi ya 50 wa Nigeria.

Bw. Liu Naiya alisema wakati China inapata maendeleo, nchi nyingi barani Afrika pia zinafanya mageuzi ya soko huria, zamani China ilizipatia nchi za Afrika misaada bila malipo, hivi sasa uhusiano huo umebadilika kuwa ushirikiano wa kiuchumi na kiteknolojia wa kufuata hali halisi ulio wa kunufaishana. Takwimu zilizotolewa na wizara ya biashara ya China zinaonesha kuwa, mwaka 2006 thamani ya biashara kati ya China na Afrika iliongezeka kwa kasi na kufikia dola za kimarekani bilioni 55, na mwaka 1950 thamani hiyo ilikuwa ni dola za kimarekani milioni 12 tu. Hivi sasa China imekuwa ni mwenzi mkubwa wa tatu wa biashara kwa bara la Afrika.

Mwezi June mwaka huu China ilianzisha mfuko wa maendeleo ya China na Afrika. Fedha za kwanza za mfuko huo zilifikia dola za kimarekani bilioni moja, na mwishowe zitafikia dola za kimarekani bilioni 5. Mfuko huo unachukuliwa kuwa ni mfuko mkubwa kabisa unaoshughulikia maendeleo ya Afrika, ambao ulianzishwa na benki ya maendeleo ya China.

Naibu mkurugenzi wa benki ya maendeleo ya China Bw. Gao Jian alisema, mfuko huo unashughulikia mambo ya uwekezaji wa kampuni zinazowekeza barani Afrika na kampuni zinazofanya biashara barani Afrika, kuzisaidia kampuni hizo kutatua suala la kutokuwa na fedha za kutosha, na kutoa huduma za habari kwa kampuni zinazowekeza barani Afrika.

Wakati rais Hu Jintao alipofanya ziara kwenye nchi nane za Afrika mwanzoni mwa mwaka huu, alisisitiza mara nyingi kuwa ushirikiano kati ya China na Afrika lazima ni wa kunufaishana. Rais Hu Jintao vilevile alizitaka kampuni za China barani Afrika zijitolee kubeba majukumu ya kijamii kwa msingi wa maendeleo ya muda mrefu.

Ili kuboresha miundo ya biashara kati ya China na Afrika, na kuhimiza maendeleo yenye usawa ya biashara kati ya pande hizo mbili, rais Hu Jintao alieleza kithabiti kuwa, serikali ya China haizihimizi kampuni za China zichukue nafasi za nchi nyingine kwenye soko kwa ongezeko la idadi ya bidhaa zinazouzwa kwa nje, China itaongeza idadi ya bidhaa zinazoagizwa kutoka barani Afrika, bali itapunguza kwa kiasi kikubwa ushuru wa bidhaa za Afrika zinazosafarishwa kuja China.

Serikali ya China pia imedhibiti uuzaji wa bidhaa za nguo kwa Afrika, na kuwaandaa watu wenye ujuzi na msaada wa kiteknolojia kwa viwanda vya nguo vya Afrika. Kwenye mkutano wa wakuu wa baraza la ushirikiano kati ya China na Afrika uliofanyika hapa Beijing mwezi Novemba mwaka jana, ili kuhimiza maendeleo ya uhusiano wa kiwenzi na kimkakati wa aina mpya kati ya China na Afrika, rais Hu Jintao alitangaza hatua nane, kama vile kufungua zaidi soko kwa Afrika, kuongeza bidhaa za Afrika zinazoruhusiwa kuuzwa kwenye soko la China bila ushuru kufikia aina za 440 kutoka 190, katika miaka mitatu ijayo kuanzisha sehemu 3 hadi 5 za ushirikiano wa kibiashara kwenye nchi za Afrika, kuzipatia nchi za Afrika mikopo nafuu ya dola za kimarekani bilioni 3, na kuzisaidia nchi za Afrika kuwaandaa watu wenye ujuzi.

Mkurugenzi wa ofisi ya utafiti wa mambo ya Afrika ya taasisi ya uhusiano wa kimataifa wa hivi sasa ya China Bw. Xu Weizhong alisema, China inakaribishwa barani Afrika na inaaminiwa na nchi za Afrika, sababu muhimu ni urafiki na udhati usiobadilika wa China kwa Afrika katika miongo kadhaa iliyopita.

Katika miaka ya 60 ya karne iliyopita, China ilikuwa inakabiliwa na matatizo makubwa ya kiuchumi, lakini wahandisi wa China bado walikuwa wanafanya juhudi kujenga barabara, madaraja, hospitali, majumba na viwanja vya michezo. Katika miaka ya 80 ya karne iliyopita, wakati Afrika ilipopuuzwa na nchi za magharibi, China bado ilitilia maanani kuendeleza uhusiano na Afrika.

Bw. Xu Wei Zhong alisema, maendeleo ya uhusiano kati ya China na Afrika yanathibitisha kuwa, kwa bara la Afrika, China ni rafiki muhimu anayeweza kukabiliana na matatizo pamoja na Afrika.

Idhaa ya kiswahili 2007-10-26