"Mpango wa Chipukizi" ni shughuli iliyoanzishwa na Mfuko wa China unaowasaidia watoto na vijana mwaka 1989 kwa lengo la kuwasaidia watoto wa kike kutoka kwenye familia zenye matatizo ya kiuchumi walioacha shule warudi tena shuleni.
Naibu mwenyekiti wa shirikisho kuu la wanawake wa China, ambaye pia ni katibu wa sekretarieti ya shirikisho hilo Bibi Huang Qingyi hivi karibuni alitufahamisha kuwa, hadi kufikia mwaka huu mpango huo umechangisha Yuan zaidi ya bilioni 1 na kuwasaidia watoto wa kike milioni 1.7 kurudi tena shuleni.
Bibi Huang Qingyi alisema China ni nchi kubwa yenye watu zaidi ya bilioni 1.3 ambao kati yao watu wasio wazima ni milioni 370 na nusu kati yao ni watoto wa kike. Kamati za ngazi mbalimbali za chama cha kikomunisti cha China na serikali siku zote zinafuatilia sana elimu kwa watu wasio wazima. Lakini China bado ni nchi inayoendelea yenye idadi kubwa ya watu, kiwango cha maendeleo na nguvu ya uzalishaji bado kiko chini. Kwa hivyo, watoto kadhaa walioko sehemu zenye matatizo ya kiuchumi za magharibi mwa China, hasa watoto wa kike wanapata matatizo kadhaa ya kupata elimu.
Kutokana na matakwa ya kamati kuu ya chama cha kikomunisti cha China na baraza la serikali la China, shirikisho kuu la wanawake wa China lilifanya juhudi kuwasaidia watoto wa familia zenye matatizo ya kiuchumi hasa watoto wa kike walioacha shule warudi tena shuleni.
Katika miaka 10 iliyopita, mpango huo ulipata uungaji mkono na misaada kutoka pande mbalimbali, umechangisha Yuan milioni 600 na kuwasaidia watoto wa kike zaidi ya milioni 1.7 kurudi tena shuleni. Watu kutoka makundi mbalimbali walichangia fedha nyingi, kuwasaidia watoto wa familia zenye matatizo ya kiuchumi kurudi tena shuleni. Watu wenye wanaojitolea wa Hongkong na Macao walikwenda kukagua sehemu za magharibi mwa China zenye matatizo makubwa ya kiuchumi, na kuchangia fedha ili zitumike kwa ajili ya ujenzi wa "shule za chipukizi".
Idara husika pia zilichukua hatua mbalimbali kwa mujibu wa matakwa ya kamati kuu ya chama cha kikomumisti cha China na baraza la serikali. Wizara ya elimu ya China imetoa sera ya elimu ya lazima ya miaka tisa, ili kuwafanya watoto wa familia zenye matatizo ya kiuchumi wapate fursa ya kurudi tena shuleni.
Kutokana na hali mpya, "Mpango wa Chipukizi" unaendelea lakini lengo lake la mwanzo linabadilika na kuwa ni pamoja na kutatua masuala ya wavulana watakaojiunga na shule za sekondari.
Watoto wa kike waliopata msaada kutoka kwenye mpango huo walisema, kutokana na msaada wa "Mpango wa Chipukizi", wanaweza kujiunga na shule za sekondari kuendelea na masomo yao bila vikwazo, na sasa tumejiunga na vyuo vikuu, tutaendelea kusoma kwa bidii. Walisema baada ya kuhitimu kutoka vyuo vikuu watarudi nyumbani kuwafundisha watoto wengi zaidi wa familia zenye matatizo ya kiuchumi.
"Mpango wa Chipukizi" ni mradi wa kimsingi unaonufaisha vizazi hadi vizazi, pia ni hatua muhimu ya kutimiza elimu ya lazima ya miaka tisa na kuondoa hali ya vijana wasiojua kusoma wala kuandika.Ili kuimarisha elimu kwa watoto wa kike, kuwaandaa watoto wa kike wawe na uwezo wa kujiendeleza, mfuko huo pia ulianzisha "mfuko maalumu wa kutoa mafunzo ya ufundi wa kazi kwa watoto wa kike, na kutoa mafunzo ya aina mbalimbali ya ufundi wa kazi kwa wanawake na watoto wa kike zaidi ya laki 4.
"Mpango wa Chipukizi" umekuwa kitu kinachojulikana kwa kila mtu nchini China.
|