Mjumbe maalumu wa serikali ya China anayeshughulikia mambo ya Afrika Bw. Liu Guijin hivi karibuni alipohojiwa na mwaandishi wa habari wa Shirika la habari la China Xinhua alisema, China inashughulikia mambo kwa njia inayoweza kuelewa na kukubaliwa na marafiki wa Afrika, hivyo inaweza kuonesha umuhimu maalumu katika utatuzi wa suala la Darfur.
Katika miezi mitatu iliyopita tangu ateuliwe kuwa mjumbe maalumu wa serikali ya China anayeshughulikia mambo ya Afrika mwezi Mei, mwaka huu, Bw. Liu Guijin alifanya ziara barani Afrika mara tatu. Katika ziara hizo tatu, alikwenda mara mbili kwenye sehemu ya Darfur yenye hali ya wasiwasi. Baada ya Sudan kukubali kuwekwa jeshi la mseto la kulinda amani la Umoja wa Afrika na Umoja wa Mataifa kwenye sehemu ya Darfur, wakimbizi zaidi ya milioni moja kwenye sehemu hiyo wanakaribia kurudi nyumbani.
Bw. Liu Guijin alisema siku zote China inafuata msimamo ulio wazi katika utatuzi wa suala la Darfur. Viongozi wa China na maofisa wa kidiplomasia wa China wakitumia fursa mbalimbali walibadilishana maoni mara kwa mara na viongozi na maofisa wa kidiplomasia wa nchi za magharibi.
Serikali ya Sudan na Umoja wa Afrika zilifanya ushirikiano wa muda mrefu kuhusu utatuzi wa mgogoro wa kikabila kwenye sehemu ya Darfur. Nchi kadhaa za magharibi zinailaani serikali ya Sudan kufanya mauaji ya kikabila kwenye sehemu ya Darfur, lakini lawama hizo zinapingwa kutokana na uchunguzi uliofanywa na Umoja wa Mataifa kwenye sehemu hiyo.
Kutokana na kuwa na wasiwasi juu ya lengo halisi la nchi za magharibi, serikali ya Sudan ilikataa jeshi lolote kuingia kwenye sehemu ya Darfur isipokuwa jeshi la Umoja wa Afrika. Nchi za magharibi zilitishia kuiwekea serikali ya Sudan vikwazo vya kiuchumi, na hali ya sehemu hiyo ilizidi kuwa ya utatanishi zaidi.
Serikali ya China inashikilia kutatua suala la Darfur kwa njia ya kisiasa, yaani mamlaka ya nchi na ukamilifu wa ardhi ya Sudan vinapaswa kuheshimiwa, na inaona kuwa vikwazo dhidi ya Sudan havisaidii kutatua suala hilo. Ili kufanya hali ya wasiwasi isizidi kuwa mbaya, China ilifanya juhudi mfululizo za kidiplomasia. Rais Hu Jintao wa China alifanya mazungumzo mara mbili na rais Omar al-Bashir wa Sudan mwezi Novemba mwaka jana na mwezi Februari mwaka huu, ambapo walijadili kuhusu mchakato wa kisiasa wa utatuzi wa suala la Darfur.
Alipofanya ziara nchini Sudan mwezi Mei mwaka huu, Bw. Liu Guijin alikutana na rais Bashir na mawaziri kadhaa wa serikali ya Sudan, ambapo aliishauri Sudan irekebishe msimamo wake kuhusu mpango uliotolewa na Bw. Kofi Annan kuhusu kuweka jeshi la mseto la kulinda amani kwenye sehemu ya Darfur. Bw. Liu Guijin alieleza kuwa kupokea mpango uliotolewa na Bw. Kofi Annan kunaendana na maslahi ya Sudan kwa hivi sasa na muda mrefu wa siku za mbele, kwa sababu mpango uliokubaliwa na pande mbalimbali unaweza kusaidia utatuzi wa suala la Darfur.
Tarehe 12 mwezi Juni Sudan ilitangaza kupokea kikamilifu mpango uliotolewa na Bw. Kofi Annan kuhusu kuweka jeshi la mseto la kulinda amani kwenye sehemu ya Darfur. Tarehe 31 mwezi Julai Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa lilipitisha azimio la No.1769, na kuamua kutuma jeshi la kulinda amani linaloundwa na Umoja wa Afrika na Umoja wa Mataifa kwenye sehemu ya Darfur.
Mjumbe wa kudumu wa Sudan kwenye Umoja wa Mataifa Bw. Abdal Haleem alisema, azimio hilo lilizingatia ufuatiliaji mwingi wa serikali ya Sudan, kwa mfano, azimio limeweka kanuni kuwa jeshi la mseto la kulinda amani linapotekeleza majukumu haliruhusiwi kudhuru umuhimu wa serikali ya Sudan.
Bw. Liu Guijin alisema "Darfur ni Darfur ya Sudan, ni Darfur ya Afrika". China siku zote inatilia maanani uhusiano kati ya China na Afrika kwa msingi wa usawa, vilevile inashikilia sera ya kutoingilia kati ya mambo ya ndani ya nchi nyingine. Bw. Liu Guijin alisema sera ya China kuhusu Afrika inatokana na mfumo wa thamani ya utamaduni na historia ya muda mrefu ya China yenyewe.
Bw. Liu Guijin alisema China na Afrika zote zilipita kipindi cha utawala wa kikoloni wa nchi za magharibi, na China haitadhuru maslahi ya waafrika daima kwa ajili ya kutafuta maslahi yake binafsi. Urafiki kati ya China na Afrika ni msingi muhimu wa sera ya amani ya kidiplomasia ya China. Kuhusu ushirikiano kati ya China na Afrika, Bw. Liu Guijin alisisitiza kuwa ushirikiano huo ulianzishwa kwa msingi wa usawa, kunufaishana, hali ya uwazi na kutotenga upande mwingine.
Bw. Liu Guijin alisema kuwa kihalisi China inaagiza mafuta kutoka kwa Sudan, lakini kampuni za mafuta za nchi za magharibi zimechukua nafasi kubwa kabisa kwenye soko la raslimali barani Afrika. Kampuni za China zilipata makubaliano ya mafuta kwa kupitia zabuni ya kimataifa, hata nchini Sudan miradi ya China iliwekezwa na kampuni za China na pande nyingi zikiwemo Uingereza, Canada, India, Malaysia na Sudan. China inachukua nafasi ndogo kabisa katika kiasi cha jumla cha uzalishaji wa mafuta barani Afrika. Takwimu zilizotolewa na Umoja wa Afrika zimeonesha kuwa mwaka 2006 asilimia 33 ya mafuta barani Afrika yaliuzwa kwa Marekani, asilimia 36 yalisafirishwa kwa Ulaya, na China iliagiza asilimia 8.7 tu ya mafuta yaliyozalishwa barani Afrika.
Kampuni za China barani Afrika zimeleta mitaji na teknolojia kwa maendeleo ya Afrika. Mtaalamu maarufu wa elimu ya uchumi wa Afrika Bw. Adedeji alisema ushirikiano kati ya China na Afrika ni wa usawa, na kunufaishana, na wananchi wamepata manufaa mengi kutokana na ushirikiano huo.
Kampuni ya makundi ya mafuta na gesi ya China ambayo ni kampuni kubwa kabisa iliyowekezwa na nchi za nje nchini Sudan imetoa dola za kimarekani milioni 35 kujenga barabara, madaraja, hospitali na shule, na kuwanufaisha wakazi milioni 1.5 wa huko.
Wakati rais Hu Jintao wa China alipofanya ziara nchini Sudan mwezi Februari mwaka huu, alieleza kuwa China imeamua kutoa msaada mwigine wa vifaa wenye thamani ya Yuan milioni 40 kwa sehemu ya Darfur kwenye msingi wa msaada wa Yuan milioni 80 iliotoa hapo kabla.
|