Wafanyakazi wa Idhaa ya Kiswahili ya CRI
China Radio International
China
Dunia
(GMT+08:00) 2007-11-20 15:31:38    
Chemsha bongo "Tukutane Beijing mwaka 2008 kwenye Michezo ya Olimpiki" 2

cri

Mwito wa kauli mbiu na wanasesere wa alama ya baraka kwenye Michezo ya Olimpiki ya Beijing

Michezo ya Olimpiki ya mwaka 2008 itafunguliwa kwa shangwe mjini Beijing tarehe 8 Agosti, ili kutangaza vizuri zaidi wazo la maandalizi ya michezo hiyo na kuionesha dunia utamaduni wa China unaong'ara, mwaka 2005 Kamati ya maandalizi ya Michezo ya Olimpiki ya Beijing ilitoa mwito wa kauli mbiu na Fuwa wa alama ya Baraka kwenye Michezo ya Olimpiki, basi mwito huo wa kauli mbiu na wanasesere wa alama ya Baraka ni nini? Na vina maana gani?

"Mwito wa kauli mbiu ya Michezo ya Olimpiki ya mwaka 2008 ni "Dunia moja na ndoto moja". Usiku wa tarehe 26 Juni, mwaka 2005, mjumbe wa ofisi ya siasa ya kamati kuu ya Chama cha Kikomunisti cha China Bwana Li Changchun alitangaza mwito wa kauli mbiu ya Michezo ya Olimpiki ya mwaka 2008 kwenye Jumba la michezo la wafanyakazi la Beijing.

Mwito wa kauli mbiu wa Michezo ya Olimpiki huonesha kwa maneno machache sahihi wazo la Michezo ya Olimpiki na utamaduni wa nchi mwenyeji wa michezo hiyo. Tokea Michezo ya Olimpiki ya mwaka 1988 ifanyike huko Seoul Korea Kusini, kila awamu nchi mwenyeji wa michezo hiyo hutoa mwito wa kauli mbiu. Kwa mfano, kwenye Michezo ya Olimpiki ya mwaka 2004 iliyofanyika huko Athens, wagiriki walitoa mwito usemao: "Karibuni nyumbani". Mwito huo si kama tu ulitoa mwaliko kwa furaha kubwa kabisa kwa nchi zote za ukoo mkubwa wa Olimpiki duniani, bali pia ulieleza vilivyo furaha na fahari iliyo nayo Ugiriki ya kukaribisha Michezo ya Olimpiki kufanyika tena katika nchi hiyo, ambayo ni chimbuko la michezo ya Olimpiki.

Basi, mwito wa kauli mbiu wa Michezo ya Olimpiki ya Beijing usemao "Dunia moja na ndoto moja" unaeleza nini? Kamati ya maandalizi ya Michezo ya Olimpiki ya Beijing ilisema, mwito huo wa "Dunia moja na ndoto moja" si kama tu umeeleza kuwa chini ya uhamasishaji wa moyo wa Michezo ya Olimpiki, dunia nzima ina matumaini ya pamoja ya kutafuta siku nzuri za mbele, bali pia umeeleza matumaini ya wakazi wa Beijing na wananchi wa China ambao wanapenda kuwa na maskani mazuri, kunufaika pamoja na matokeo ya ustaarabu, na kujenga siku nzuri za mbele. Aidha, utamaduni wa jadi wa China husisitiza uhusiano wenye masikilizano kati ya binadamu na mazingira ya asili, na kati ya watu na watu, mwito wa kauli mbiu wa Michezo ya Olimpiki ya Beijing unamaanisha kujiendeleza katika hali ya masikilizano, kuishi kwa amani, na kufanya ushirikiano wa kunufaishana ili kupata maendeleo ya pamoja, maana hizo zinaligana na utamaduni wa jadi wa China. Mtaalamu wa suala la Michezo ya Olimpiki wa Chuo kikuu cha Beijing Bwana Zhang Yiwu alisema:

"Mwito wa kauli mbiu wa Michezo ya Olimpiki ya Beijing una maana mbili muhimu, "Duni moja na ndoto moja" inamaanisha kuwa China inafuata moyo wa kuzifungulia mlango nchi za nje, China inataka kuwasiliana na nchi nyingine duniani, na China na nchi nyingine duniani zina matarajio ya pamoja juu ya Michezo ya Olimpiki, amani na vitu vingine vyote vyenye thamani wanavyopenda binadamu".

Mwito huo una maneno machache, lakini ulitolewa kutokana na busara za watu wengi. Tarehe 1 Januari mwaka 2005, Idara ya kuandaa shughuli za utamaduni katika Kamati ya maandalizi ya Michezo ya Olimpiki ya Beijing, ilianza rasmi kuwahamasisha watu wa nchini na ng'ambo watoe mapendekezo kuhusu mwito wa kauli mbiu. Katika mwezi mmoja tu baada ya hapo, ofisi husika ilikusanya miito zaidi ya laki 2.1. Wananchi wa sehemu mbalimbali nchini China, pamoja na wakazi wa mikoa ya utawala maalum ya Hongkong na Makau, wakazi wa kisiwani Taiwan, wachina na marafiki wanaoishi nchini Marekani, Uingereza, Norway, na Brazil walishiriki kwenye shughuli za kutoa mapendekezo hayo.

Na miito zaidi ya laki 2.1 iliyokusanywa ilisaidia kutoa mwito wa kauli mbiu wa Michezo ya Olimpiki usemao "Dunia moja na ndoto moja", ambapo Kamati ya maandalizi ya Michezo ya Olimpiki ya Beijing ilichambua na kusikiliza maoni na mapendekezo ya watu wa idara mbalimbali, na kufanya utafiti na utungaji kwa kupitia kampuni maarufu duniani, mwishowe ikaamua mwito wa "Dunia moja na ndogo moja" kuwa mwito wa kauli mbiu wa Michezo ya Olimpiki ya Beijing. Tunaweza kusema kutolewa kwa mwito huo wa kauli mbiu kunatokana na juhudi na busara za wataalamu wa idara mbalimbali za nchi mbalimbali duniani, kumeonesha matumaini na ufuatiliaji mkubwa wa watu wa duniani juu ya Michezo ya Olimpiki ya Beijing, vilevile kumeonesha uelewa wa wananchi wa China kuhusu Michezo ya Olimpiki.

Tarehe 11 Novemba, mwaka 2005, Kamati ya Maandalizi ya Michezo ya Olimpiki ya Beijing ilitangaza wanasesere watano wa alama ya Baraka ya Michezo ya Olimpiki ya Beijing, yaani Fuwa watano, Fu, maana yake ya Kichina ni Baraka, Wa, maana yake ya Kichina ni mtoto, Fuwa hao watano walipewa majina ya Beibei, Jingjing, Huanhuan, Yingying na Nini. Kwa kuwa utamaduni wa China unahusu mambo mengi mbalimbali, kama kutoa alama moja tu si rahisi kueleza mambo mbalimbali ya utamaduni wa China, tangu vitu vya alama ya Baraka vionekane kwenye Michezo ya Olimpiki ya mwaka 1972 iliyofanyika huko Munich, Ujerumani, Fuwa watano wa alama ya Baraka ya Michezo ya Olimpiki ya Beijing wanaonekana ni vitu vingi zaidi vya alama ya Baraka kwenye michezo ya awamu moja.

Maumbo ya wanasesere hao watano yameonesha sura za samaki, panda, moto mtakatifu wa Olimpiki, swala wa kitibet na mbayuwayu. Sura za wanasesere hao watano zinamaanisha uhusiano kati ya bahari, misitu, moto, ardhi na mbingu, ambazo zinamithilisha binadamu kuishi katika hali ya mapatano na mazingira ya asili, maana hiyo inalingana na wazo la China la kuandaa Michezo ya Olimpiki katika mazingira yasiyo na uchafuzi. Aidha, maumbo ya Fuwa hao watano pia yamemithilisha maana kadha wa kadha kuhusu utamaduni wa China. Kwa mfano, Fuwa Beibei, umbo lake ni kama samaki, usanifu wa umbo hilo ulitokana na picha ya mwaka wa jadi wa China, na tukisoma kwa mfululizo majina matano ya Fu Wa hao watano, Beibei, Jingjing, Huanhuan, Yingying na Nini, maana ya Kichina ya majina hayo ni Beijing Huan Ying Ni, yaani Beijing inakukaribisha. Naibu mwenyekiti wa Kamati ya uratibu wa Michezo ya Olimpiki ya Beijing katika Kamati ya kimataifa ya Olimpiki Bw. Gospa alisifu sana Fuwa hao watano, akisema:

"Vitu vya alama ya Baraka kwenye Michezo ya Olimpiki ya Beijing vinaundwa na Fuwa watano wanaopendeza, ambao wanashikamana barabara kama vidole vitano, sura zao zinang'ara kama ilivyo nembo ya Olimpiki ya maduara matano, ambayo imeonesha binadamu kuishi katika hali ya mapatano na mazingira ya asili, kweli inawapatia watu taswira nyingi, hivyo Michezo ya Olimpiki inatakiwa kuishukuru Beijing".

Wasikilizaji wapendwa, sasa tunatoa maswali mawili:

1. Mwito wa kauli mbiu ya Michezo ya Olimpiki ya Beijing ni nini?

2. Wanasesere watano wa alama ya Baraka ya Michezo ya Olimpiki ya

Beijing yaani Fuwa watano, wamepewa majina gani?

Idhaa ya kiswahili 2007-11-20