Wafanyakazi wa Idhaa ya Kiswahili ya CRI
China Radio International
China
Dunia
(GMT+08:00) 2007-11-28 16:50:34    
China yaadhimisha siku ya kwanza ya ugonjwa wa Kisukari ya Umoja wa Mataifa

cri

Ugonjwa wa kisukari ni ugonjwa sugu unaosababishwa na upungufu wa insulin mwilini. Hivi sasa idadi ya wagonjwa wa kisukari duniani imezidi milioni 500. kutokana na madhara makubwa ya ugonjwa huo, mwaka jana mkutano wa baraza kuu la Umoja wa Mataifa ulipitisha azimio na kuamua kubadilisha siku ya ugonjwa wa Kisukari duniani ambayo ni tarehe 14 Novemba kila mwaka kuwa siku ya ugonjwa wa kisukari ya Umoja wa Mataifa. Hii imeonesha kuwa Umoja huo unatilia maanani kazi ya kinga na tiba ya ugonjwa huo, na pia imeonesha nia na imani ya serikali ya nchi mbalimbali ya kudhibiti ugonjwa huo.

Serikali ya China pia imeitikia mwito wa Umoja wa Mataifa, na kufanya shughuli nyingi za kueneza ufahamu kuhusu ugonjwa huo katika siku hiyo.

Tarehe 14 Novemba mwaka huu ni siku ya kwanza ya ugonjwa wa Kisukari ya Umoja wa Mataifa. Siku hyo shughuli nyingi za maadhimisho zimefanyika hapa Beijing. Mwenyekiti wa shirika la mfuko wa ugonjwa wa Kisukari duniani Bw. Anil Kapur alisema, hali ya kuwepo kwa wagonjwa wengi na idadi ya wagonjwa inaongezeka siku hadi siku imeufanya ugonjwa huo usio suala la kawaida la afya, masuala mbalimbali ya kiuchumi na kijamii yaliyosababishwa na ugonjwa huo pia yanapaswa kutiliwa maanani. Bw. Kapur alisema:

"Ugonjwa wa Kisukari si kama tu unaleta madhara makubwa kwa afya ya binadamu, bali pia unasababisha hasara za kiuchumi. Kwa mfano China inatumia dola za kimarekani bilioni 20 kila mwaka katika matibabu ya ugonjwa huo, ambapo hasara za kiuchumi zinazosababishwa na wagonjwa hao kuacha kazi pia zinafikia dola za kimarekani bilioni 20."

Kauli mbiu ya siku hiy ni "Ugonjwa wa Kisukari na watoto na vijana" naibu mkurugenzi wa idara ya kinga na udhibiti wa magonjwa katika wizara ya afya ya China Bi. Kong Lingzhi alisema, ingawa idadi wa watoto wenye ugonjwa wa kisukari inaongezeka kila mwaka, lakini watu wengi hawawezi kuhusisha ugonjwa huo na watoto na vijana, hivyo wagonjwa hao hawafuatiliwa ipaswavyo kama watu wazima wenye ugonjwa huo. Utafiti wa ksayansi umeonesha kuwa, uzito unaosababisihwa na tabia mbaya za maisha unahusiana kwa karibu na ugonjwa huo. China ni nchi yenye watoto zaidi ya milioni 300, lakini hivi sasa watoto wenye uzito wa kupita kiasi pia wanaongezeka, kwa upande huo, kauli mbiu ya siku hiyo ya mwaka huu ina umuhimu mkubwa kwa China. Bi. Kong Lingzhi alisema:

"mwelekeo wa hivi sasa unaleta wasiwasi mkubwa. Tunaweza kuona watoto wenye uzito mkubwa kupita kiasi kila mahali, hasa mijini idadi ya watoto wenye tatizo hilo imezidi asilimia 8. uzito mkubwa wa kupita kiasi unahusiana kwa karibu na ugonjwa wa Kisukari, na hivi sasa ugonjwa huo ambao ulitokea kwa watu wazima pia unatokea kwa watoto."

Idara za afya katika ngazi mbalimbali zinatumia fursa ya siku hiyo na kuandaa shughuli mbalimbali ili kueneza ufahamu kuhusu kinga na tiba ya ugonjwa huo, na kuinua mtizamo wa vijana, walimu na wazazi wa watoto kuhusu ugonjwa huo. idara za afya za sehemu kadhaa zinatuma wataalamu kufanya mihadhara shuleni, sehemu nyingine zinasambaa vipeperushi kuhusu ugonjwa huo shuleni, au kushrikisha wanafunzi kwenye mashindano ya ujuzi kuhusu ugonjwa huo.

Wanafunzi wengi wanapata ufahamu kuhusu ugonjwa huo katika shughuli hizo na kutaka kubadilisha tabia zao baya za kula na maisha, mwanafunzi mmoja wa shule ya msingi mjini Beijing alisema:

"napenda sana kula nyama, kwa kuwa nadhani sisi watoto bado hatuwezi kupatwa ugonjwa wa kisukari, basi hatuna wasiwasi. Leo baada ya kusikiliza mihadhara hiyo, nimeanza kuwa na wasiwasi, sithibuthu kula nyama nyingi katika siku za baadaye."

Walimu na wazazi wa wanafunzi pia wanaridhika na shughuli hiyo. Naibu mkuu wa shule moja mjini Beijing Bw. Guan Jie alisema:

"sisi watumishi wa elimu tunapaswa kufuatilia zaidi ukuaji na afya ya wanafunzi. Tunataka vijana na watoto wawe na tabia nzuri za maisha na kuondokana na ugonjwa wa Kisukari."

Naibu mkurugenzi wa idara ya kinga na udhibiti wa magonjwa katika wizara ya afya ya China Bi. Kong Lingzhi alisema, chakula cha kiafya na mazoezi ya viungo yana umuhimu mkubwa kwa kukinga na hata kutibu ugonjwa huo. Kwa hivyo kazi ya kinga na tiba ya ugonjwa huo kwa vijana inapaswa kuhusisha maisha na masomo yao. Bi. Kong Lingzhi alisema,

"tunapaswa kuunganisha kazi ya kinga na tiba ya ugonjwa wa kisukari na mazoezi ya viungo na masomo ya shuleni, wala si shughuli ya peke yake inayoongeza mizigo kwa wanafunzi na shule. Tunataka wanafunzi waweze kuona kuwa michezo sio kwa furaha tu, bali pia kwa ajili ya kulinda afya yao."