Wafanyakazi wa Idhaa ya Kiswahili ya CRI
China Radio International
China
Dunia
(GMT+08:00) 2007-12-04 09:44:02    
Chemsha bongo "Tukutane Beijing mwaka 2008 kwenye Michezo ya Olimpiki"4

cri

Kutokana na mahitaji ya mipango ya mashindano, siyo michezo yote ya Olimpiki ya mwaka 2008 itafanyika mjini Beijing. Michezo ya soka itafanyika mijini Tianjin, Qinhuangdao, Shanghai na Shenyang, michezo ya mashua zenye matanga itafanyika mjini Qingdao, na mchezo wa kuonesha ustadi wa farasi utafanyika huko Hongkong. Miji hiyo 6 inayoshirikiana na Beijing kuandaa Michezo ya Olimpiki ya mwaka 2008 pia itajulikana katika historia ya Michezo ya Olimpiki.

Michezo ya mashua zenye matanga na mchezo wa kuteleza kwenye mawimbi ya maji ni michezo ya Olimpiki itakayofanyika kwenye bahari. Hivyo michezo kama hiyo hakika itafanyika kwenye mji ulioko pwani. Kwa mfano, kwenye Michezo ya 20 ya majira ya joto iliyofanyika huko Munich, kusini mwa Ujerumani mwaka 1972, michezo ya mashua zenye matanga ilifanyika huko Kiel, mji ulioko pwani wa kaskazini mwa Ujerumani. Na mji wa Qingdao ulioko kwenye kando ya magharibi ya Bahari ya Pasifiki unakaribia na Bahari ya manjano, na kutazamana na peninsula ya Korea na Japan, kwani ziko kwenye pande mbili za bahari. Kwenye sehemu ya Qingdao kuna hali mwafaka ya nguvu ya upepo na mkondo wa maji, ambapo ni sehemu nzuri ya kufanyika kwa michezo ya mashua zenye matanga, hivyo mji wa Qingdao umechaguliwa kushirikiana na Beijing kuandaa Michezo ya Olimpiki ya mwaka 2008. Mji wa Qingdao ulioko katika mazingira yenye rangi ya kijani ya miti mingi iliyopandwa kote mjini, rangi ya buluu ya bahari na anga ya samawati unawavutia sana watu macho kwa mandhari yake nzuri. Baada ya kuchaguliwa kuwa mji unaoshirikiana na Beijing kuandaa Michezo ya Olimpiki ya mwaka 2008, mji huo umepewa fursa nyingi za kujiendeleza. Meya wa mji huo Bw. Xia Geng alisema: "Kutokana na kuhimizwa na maandalizi ya Michezo ya Olimpiki, katika miaka ya hivi karibuni mambo ya uchumi wa mji wa Qingdao yamepata maendeleo ya haraka. Kuandaa Michezo ya Olimpiki kumetuletea mabadiliko mengi katika maisha ya wakazi wa mji wetu, ambapo mapato ya wakazi yanaongezeka kwa miaka mfululizo. Katika miaka minne iliyopita, mapato ya wakazi wa mjini na vijijini kwetu yaliongezeka kwa asilimia 15.1 na asilimia 11.8, ambapo ni kipindi cha kupata ongezeko la kasi zaidi kwa mapato ya wakazi".

Lakini mabadiliko makubwa zaidi yametokea katika sura ya mji. Takwimu zilizokusanywa zimeonesha kuwa, katika miaka minne iliyopita, Mji wa Qingdao ulitenga Yuan karibu bilioni 20 kwa ajili ya kuandaa mashindano ya michezo ya mashua zenye matanga, ambapo ongezeko la mwaka la fedha zilizotengwa na mji huo katika mambo ya matibabu, utamaduni na mawasiliano zimefikia asilimia 40. Hivi sasa eneo jipya la hospitali ya mji huo itakayotoa huduma za matibabu kwa ajili ya michezo ya Olimpiki ya mashua zenye matanga limezinduliwa; ujenzi wa Jumba kubwa la michezo ya sanaa la Qingdao na Kituo cha usanii wa kisasa cha Qingdao unaendelea sasa; kazi za ukarabati wa Jumba la sanaa ya uchoraji la mji wa Qingdao, Maktaba ya Qingdao na Jumba la muziki pia zinaendelea. Ili kuhakikisha mawasiliano barabarani wakati wa Michezo ya Olimpiki, Qingdao imeimarisha ujenzi wa mawasiliano ya umma, na kuanzisha ujenzi wa handaki chini ya bahari na daraja kubwa la ghuba, ambapo mradi wa upanuzi wa kipindi cha pili wa Uwanja wa ndege wa kimataifa wa Qingdao utakamilika mwishoni mwa mwaka huu. Ujenzi wa miundo hiyo mbinu umeongeza nafasi laki moja za ajira, pia umeufanya mji huo wenye mandhari nzuri uonekane kuwa wenye hali ya kisasa na kiutamaduni zaidi.

"Tukutane Qingdao mwaka 2008 kwenye mchezo wa mashua zenye matanga", huu ni mwaliko uliotolewa na Mji wa Qingdao kwa watalii wa dunia nzima.

Mchezo wa kuonesha ustadi wa farasi ni mchezo pekee unaofanywa na wachezaji pamoja na farasi kwenye michezo ya Olimpiki ya aina 28, hivyo mchezo huo unawavutia na kuwafurahisha zaidi watazamaji. Mwaka 2005, kwenye Mkutano wa 117 wa wajumbe wote wa Kamati ya Olimpiki ya kimataifa, Kamati ya Olimpiki ya kimataifa, Kamati ya maandalizi ya Michezo ya Olimpiki ya Beijing na Shirikisho la kimataifa la mchezo wa kuonesha ustadi wa farasi vilifikia makubaliano kuhusu Hongkong kuandaa Mchezo wa kuonesha ustadi wa farasi wa Michezo ya Olimpiki ya mwaka 2008. Wanamichezo wengi wa duniani wanaona kuwa, Hongkong yenye desturi za kufanya mbio za farasi kwa zaidi ya miaka 100, hakika ni sehemu mwafaka zaidi ya kuandaa mchezo huo.

Mchezo wa mbio za farasi ni mchezo unaopendwa sana na wakazi wa Hongkong. Kwenye sehemu ya Hongkong yenye idadi kubwa ya watu na pilikapilika nyingi zaidi, kwenda kwenye uwanja wa michezo kuangalia mbio za farasi kumekuwa njia ya maisha kwa wakazi wengi kujiburudisha. Mashindano ya mbio za farasi yanafanyika kila wikiendi huko Hongkong, na kila mara watazamaji ni wengi sana. Hivi sasa kati ya wakazi wa Hongkong wapatao zaidi ya milioni 6?mashabiki wa mbio za farasi wanachukua theluthi moja, yaani zaidi ya milioni 2.

Mwezi Julai mwaka 1997, Hongkong iliondokana na utawala wa kikoloni wa Uingereza na kurudi kwa taifa lake China. Mpaka sasa miaka zaidi ya 10 imepita tangu Hongkong irudi China, mwenyekiti wa Kamati ya Olimpiki ya Hongkong Bw. Ho Zhenting alisema, umuhimu wa kufanya Mchezo wa kuonesha ustadi wa farasi huko Hongkong kabisa hauoneshwi tu kwenye michezo. Alisema: "Kwa kupitia mashindano ya Mchezo wa kuonesha ustadi wa farasi yatakayofanyika huko Hongkong, wakazi wa Hongkong wataweza kuongeza zaidi uzalendo wao juu ya taifa lao la China. Kama wajuavyo watu wote, nchi ya Ugiriki ilifanikiwa kuandaa Michezo ya Olimpiki, kutokana na hayo nchi hiyo iliimarisha kiwango chake cha michezo na kuongeza nguvu ya nchi nzima, muhimu zaidi ni kuwa kuandaa Michezo ya Olimpiki kuliwawezesha vijana wa nchi hiyo waongeze upendo wao kwa taifa lao. Hali kadhalika kwa Hongkong, kama Hongkong itafanikiwa kuandaa Mchezo wa kuonesha ustadi wa farasi, mafanikio hayo hakika yatasaidia michezo ya Hongkong, muhimu zaidi ni kuwa yatawahamasisha vijana wafanye juhudi zaidi na kuongeza uzalendo juu ya taifa lao la China".

Tarehe 7 Julai mwaka 2007, ujenzi wa Uwanja wa kufanyia mchezo wa kuonesha ustadi wa farasi kwa ajili ya Michezo ya Olimpiki ya Beijing na uwanja wa kufanyia mazoezi umekamilika. Kwenye mashindano ya majaribio ya mchezo huo yaliyofanyika mwezi Agosti mwaka huu, zana na vifaa vya uwanja wa michezo zilisifiwa sana na wachezaji wa sehemu mbalimbali duniani walioshiriki kwenye mashindano hayo.

Mashindano ya mchezo wa soka huwa ni mashindano yanayofanyika kwa muda mrefu zaidi. Ili kutoa urahisi kwa mpango wa mashindano ya michezo yote, katika Michezo ya Olimpiki ya awamu zilizopita mashindano ya mchezo wa soka hufanyika kwenye uwanja wa sehemu nyingine. Kwa mfano, kwenye Michezo ya Olimpiki ya mwaka 1988 iliyofanyika huko Seoul, Korea ya kusini, michuano kadhaa ilifanyika huko Pusan na miji mingine nchini Korea ya kusini. Hivyo michuano kadhaa ya soka kwenye Michezo ya Olimpiki ya mwaka 2008 ya Beijing pia itafanyika katika miji mingine minne ya Shanghai, Shenyang, Qinhuangdao na Tianjin, ambapo michuano 10 hivi itafanyika katika kila mji kwenye miji hiyo minne. Kupanga michuano ya soka kufanyika katika miji hiyo, kwa upande mmoja ni kutokana na mahitaji ya mpango wa Michezo ya Olimpiki, lakini kwa upande mwingine pia kutawawezesha watazamaji wengi wa China wafurahie Michezo ya Olimpiki.

Ndio maana, miji hiyo yote imeonesha uchangamfu na juhudi zao kubwa katika kuandaa mchezo wa soka wa Olimpiki. Shanghai ni mmoja kati ya miji yenye ustawi mkubwa zaidi na nguvu kubwa zaidi ya uhai ya kiuchumi nchini China. Kadiri mji wa Shanghai unavyoonesha umuhimu wake mkubwa siku hadi siku katika mambo ya uchumi duniani, ndivyo dunia inavyofuatilia zaidi mji huo siku hadi siku. Hivi leo mji wa Shanghai unafanya juhudi kubwa katika sekta ya michezo, ambapo michezo mbalimbali kama vile Fainali ya mwishoni mwa mwaka ya mchezo wa mpira wa wavu, Mchezo wa mbio za magari za Formula One wa tuzo kubwa ya ubingwa duniani, Mchezo wa soka wa wachezaji wa kike wa kombe la dunia wa mwaka 2007, Mashindano ya mchezo wa kuogelea wa ubingwa wa dunia wa mwaka 2011, na Michezo ya watu wenye mtindio wa ubongo wa majira ya joto ya mwaka 2007 yote yalifanyika au yatafanyika mjini Shanghai. Na hivi sasa mji wa Shanghai umechaguliwa kuwa mji unaoshirikiana na Beijing kuandaa Michezo ya Olimpiki ya mwaka 2008, ambapo michuano ya mchezo wa soka ya Olimpiki wa majira ya joto ya mwaka 2008 itafanyika pia mjini humo. Wakazi wa Shanghai wana imani kuwa, lazima kuandaa michezo mbalimbali ya kiwango cha juu mjini humo, kwani kazi hiyo inaweza kuonesha sura ya Shanghai hata ya China inayobadilika kuwa mpya siku hadi siku. Meya wa Mji wa Shanghai Bw. Han Zheng alisema: "Naona mji wa Shanghai ukiwa mji unaozifungulia mlango nchi za nje, unatakiwa kuandaa michezo mbalimbali ya kimataifa, ili kuonesha sura mpya ya China inayofuata sera ya mageuzi na ufunguaji mlango, na kuonesha sura mpya ya mji wa Shanghai".

Hali kadhalika mjini Tianjin, hivi sasa mji huo una pilika pilika za kushirikiana na Beijing kuandaa Michezo ya Olimpiki ya mwaka 2008, ambapo michuano 10 ya mchezo wa soka itafanyika huko. Wakazi wa mji huo wakiwa na uchangamfu mkubwa wanashiriki katika maandalizi yote ya mchezo. Na miji hiyo yote inayoshirikiana na Beijing kuandaa Michezo ya Olimpiki ya mwaka 2008 ina matumani kuwa itaweza kuandaa michezo ya kiwango cha juu na kuwawezesha marafiki wa nchi mbalimbali duniani waelewe utamaduni unaong'ara wa China.

Wasikilizaji wapendwa, sasa tunatoa maswali mawili :

1. Taja miji 6 itakayoshirikiana na Beijing kuandaa Michezo ya Olimpiki ya mwaka 2008.

2. Mchezo gani wa Michezo ya Olimpiki ya mwaka 2008 utafanyika huko Hongkong?

Idhaa ya kiswahili 2007-12-04