Mjini Xuzhou, mkoani Jiangsu, mashariki mwa China, kuna kijana mmoja aitwaye Zheng Fusheng ambaye alipata ulemavu kutokana na ugonjwa. Katika miaka kadhaa iliyopita, alipambana na ugonjwa kwa nia imara na uvumilivu, na pia alitoa mchango kwa jamii bila kujali maslahi yake binafsi.
Bw. Zheng Fusheng ana umri wa miaka 38 mwaka huu. Alipokuwa na umri wa miaka 21, alipata ugonjwa kwenye uti wa mgongo wake kwa ghafla, na viungo vyake vililemaa, alikuwa anaweza kusimama na hakuweza kuinama wala kukaa, aliweza kutembea kwa kutumia magongo tu. Ugonjwa huo mgumu uliitwa kuwa ni ugonjwa wa saratani usioweza kusababisha kifo. Kabla ya kuwa mgonjwa, kijana huyo alikuwa na nguvu, lakini baada ya kuumwa alipoteza uwezo wake wa kufanya kazi, na hata ilikuwa ni vigumu sana kwake kufanya vitendo vya kawaida. Bw.Zheng Fusheng alisema alikuwa analala kila siku na kupoteza mawasiliano na nje, aliona upweke. Akisema: "wakati huo nilisikitika sana hata niliona huzuni kubwa kukumbwa na janga kwenye maisha."
Kabla ya kupata ugonjwa huo, Bw. Zheng Fusheng alikuwa anaishi kama vijana wengine wenye afya, na alikuwa na matarajio mazuri juu ya siku za baadaye. Alipohojiwa na mwandishi wa habari alikuwa anawaangalia watu waliokuwa wanafanya mazoezi ya kujenga mwili kwenye viwanja mbalimbali. Alisema "kama nisingepata ugonjwa huo, mimi pia ningeweza kufanya mazoezi ya kujenga mwili bila matatizo kama walinavyofanya. Wakati huo nilianza kupata ajira nilitaka kuchuma pesa na kupata mchumba wangu ili niweze kusafiri naye sehemu mbalimbali nchini. Nilikuwa nina matumaini mazuri juu ya siku za baadaye".
Bw. Zheng Fusheng ni mtoto pekee kwa wazazi wake. Alipopata ugonjwa huo, mama yake alikuwa hana kazi na baba yake alikuwa amestaafu siku chache zilizopita, na alikuwa anapata mapato ya Renminbi mia kadhaa tu kwa mwezi. Wazazi wake walimtaka mtoto wao aweze kuwasaidia kuboresha hali ya uchumi ya familia hiyo baada ya kuanza kazi, lakini hawakutarajia kama ugonjwa wa mtoto wao ungewafanya wabebe mzigo mkubwa. Mama yake Bibi Wu Xinhua alisema: "Mtoto wangu alipatwa ugonjwa usioweza kutibika. Sina la kusema hata sioni raha yoyote katika maisha yetu."
Kuanzia hapo wazazi wa Bw. Zheng Fusheng walipata shinikizo kubwa zaidi. Walipaswa kubeba mzigo wa kulipia gharama za maisha yao na pia walipaswa kukusanya fedha, ili kulipia matibabu ya mtoto wao. Bw. Zheng Fusheng hakufurahia kuona wazazi wake wanafanya kazi ngumu,. Siku moja Bw. Zheng Fusheng alikuwa akisikiliza radio ya huko, alijaribu kuandika barua ya kuomba msaada kwa radio hiyo, lakini hakutegemei kama barua hiyo ingevutia ufuatiliaji wa watu wengi, wafanyakazi 16 wa kampuni moja ya Xuzhou walijitolea kumsaidia Zheng Fusheng kwenda hospitali ili atibiwe, kila mara walikwenda nyumbani kwake kumchukua, baadaye kumsaidia kurudi nyumbani bila kujali hali yoyote itakayotokea.
Wakati huo huo, kijana anayeitwa Ding Qiang alibadilisha maisha ya Bw. Zheng Fusheng. Bw. Ding Qiang ni mwanafunzi wa shule ya sekondari ya ufundi wa kazi, alipomfahamu Bw. Zheng Fusheng alibeba jukumu la kumsaidia Bw. Zheng Fusheng pamoja na wazazi wake. Pia Bw. Ding Qing alitumia muda wa mapumziko ya siku za baridi na siku za joto kwa kuambatana na Bw. Zheng Fusheng kwenda mji mwingine kutibiwa. Ambapo alimsaidia Bw. Zheng Fusheng katika maisha yake. Bw. Ding Qiang alisema watu wengine waliona kama wao ni ndugu. Akisema: "niliweza kuelewa huzuni yake, baada ya kumjua nakwenda nyumbani kwake kupiga soga naye na kumsaidia, nafanya juhudi kwa niwezavyo, kwa sababu sisi wote ni vijana."
Chini ya msaada ulioletwa na watu mbalimbali wa jamii, hivi sasa Bw. Zheng Fusheng amepata nafuu, na anaweza kutembea pole pole, lakini wakati huo alizidiwa na wasiwasi. Aliandika katika makala moja: kutoka kutafuta misaada hadi kuishi miongoni mwa watu wengi wanaotoa upendo kwangu, nilikuwa kama zimepita majira ya baridi na mara nikapokea majira ya spring, nina bahati kubwa na ninawashukuru sana watu wanaonisaidia, lakini pia nina wasiwasi. Alisema: (sauti 4)
"wakati wengine wanakuonesha upendo wao, na wewe pia unapaswa kuonesha shukurani ili kujibu upendo wao. Kufanya hivyo kunaweza kuinua upendo huo kwenye kiwango cha juu zaidi."
Tarehe 20 mwezi Aprili mwaka 1997 Bw. Zheng Fusheng alitimiza umri wa miaka 30. Ni katika siku hiyo, kituo cha huduma cha watu wanaojitolea cha Xin Yuanzhi mjini Xuzhou kilianzishwa kutokana na pendekezo la Bw. Zheng Fusheng. Kuanzia siku hiyo Bw. Zheng Fusheng alianza kuwa na shughuli nyingi.
Katika miaka 10 iliyopita Bw. Zheng Fusheng na watu wanaojitolea wa kituo hicho walichangisha fedha za Renminbi zaidi ya Yuan milioni 4, na wakawasaidia watu wengi waliopatwa na magonjwa au waliokuwa na ulemavu. Miongoni mwa watu waliopata misaada kutoka kwenye kituo hicho, Bi. Juan Zi ni mtu mwenye bahati kubwa. Alipata saratani ya damu alipokuwa na umri wa miaka 12. Baada ya kutibiwa kwa miaka kadhaa, familia yake ilikuwa haina fedha za kumwokoa. Baada ya kufahamishwa kuhusu hali ya ugonjwa wa Bi. Juan Zi, Bw. Zheng Fusheng na watu wengine wanaojitolea walichanga fedha za renminbi karibu Yuan laki moja ili kumsaidia afanyiwe operesheni ya kuhamisha mfupa. Katika siku zaidi ya 20 ambapo Bi. Juan Zi alipokuwa anasubiri kufanyiwa operesheni, Bw. Zheng Fusheng na watu wengine walikuwa wanamuhudumia kwa zamu. Bi. Juan zi alisema: "wakati huo kulikuwa hakuna umbali kati ya mioyo yetu, mimi nilikuwa napaswa kukaza nia ili nifaulu kufanyikwa operesheni."
Hivi sasa Bi. Juan Zi amepona ambaye afya yake imekuwa ya kawaida, na amekuwa mwalimu wa Yoga kwenye klabu ya kujenga mwili, na pia amejiunga na kituo cha watu wanaojitolea cha Xin Yuanzhi. Kituo hicho kilianzishwa zaidi ya miaka 10 iliyopita, na maisha ya Bw. Zheng Fusheng yanahusiana moja kwa moja na shughuli za hisani. Kutokana na athari yake, watu karibu na milioni moja wamejiunga na shughuli hizo na kufanya harakati za kusaidia watu maskini wenye matatizo ya kiuchumi. Bw. Zheng Fusheng alisema ingawa alikuwa mlemavu, lakini anafanya juhudi zote ili kuinua thamani ya maisha yake katika kutoa mchango wa upendo, na kutakasa moyo wake.
Idhaa ya kiswahili 2007-12-06
|