Wafanyakazi wa Idhaa ya Kiswahili ya CRI
China Radio International
China
Dunia
(GMT+08:00) 2007-12-21 14:53:50    
China na Afrika zahimiza ushirikiano wa kiuchumi na kibiashara kati yao

cri

Mwaka 2006 mkutano wa wakuu wa Baraza la ushirikiano kati ya China na Afrika ulifanyika hapa Beijing kwa mafanikio, mkutano huo ulihimiza maendeleo ya uhusiano wa kiuchumi na kibiashara kati ya China na Afrika. Kuimarishwa kwa ushirikiano wa kiuchumi na kibiashara kati ya China na Afrika si kama tu kulisukuma mbele uhusiano wa kiwenzi na kimkakati wa aina mpya kati ya pande hizo mbili, bali pia kumewanufaisha kihalisi wananchi wa pande hizo mbili.

Thamani ya biashara kati ya China na Afrika iliongezeka na kuzidi dola za kimarekani 10 kwa mara ya kwanza mwaka 2000, tangu hapo thamani hiyo iliongezeka kwa kasi kwa miaka sita mfululizo, hivi sasa China imekuwa mwenzi mkubwa wa tatu wa biashara wa Afrika. Takwimu zimeonesha kuwa tangu mwezi Januari hadi mwezi Septemba mwaka 2007, thamani ya biashara kati ya China na Afrika ilifikia dola za kimarekani bilioni 52.3, na mwaka huu thamani hiyo inatazamiwa kufikia dola za kimarekani bilioni 70. Naibu waziri wa biashara wa China Bwana Wei Jianguo hivi karibuni alisema, lengo lililowekwa na China kuhusu thamani ya biashara kati ya China na Afrika kufikia dola za kimarekani bilioni 100 hadi kufikia mwaka 2010 linatazamiwa kutimizwa kabla ya mpango uliowekwa.

Kwa upande wa uwekezaji, kampuni za China zinalichukulia bara la Afrika kuwa ni sehemu muhimu ya uwekezaji. Hadi kufikia mwishoni mwa mwaka 2006, thamani ya uwekezaji wa moja kwa moja kutoka China barani Afrika ilifikia dola za kimarekani bilioni 6.64. Katika nusu ya kwanza ya mwaka huu, thamani hiyo ilifikia dola za kimarekani milioni 480, na kuongezeka kwa kiasi kikubwa kuliko mwaka jana wakati kama huo. Miradi ya uwekezaji kutoka China inafanyika katika nchi 49 barani Afrika, ambayo inahusu sekta za biashara, uzalishaji na utengenezaji, uchimbaji wa maliasili, mawasiliano na uchukuzi, na kilimo.

Kubeba majukumu ya ujenzi ni sehemu moja muhimu ya ushirikiano wa kiuchumi na kibiashara kati ya China na Afrika. Pamoja na uhusiano mzuri wa kisiasa uliopo kati ya China na Afrika, kampuni za China zinapanua eneo la miradi hatua kwa hatua kwa bei chini na sifa nzuri. Mwaka 2006 thamani ya makubaliano yaliyosainiwa na kampuni za China barani Afrika kuhusu kazi ya ujenzi ilifikia dola za kimarekani bilioni 28.97. Katika nusu ya kwanza ya mwaka huu, thamani hiyo ilifikia dola za kimarekani bilioni 18.4, na kuongezeka kwa asilimia 18.2 kuliko mwaka jana wakati kama huo. Afrika imekuwa ni soko kubwa la pili la nje kwa kampuni za China katika kufanya kazi ya ujenzi wa miradi.

Uwekezaji kutoka China barani Afrika na ushirikiano wa kiuchumi na kibiashara kati ya China na Afrika unahimiza maendeleo ya uchumi wa nchi za Afrika, kuongeza nafasi ya ajira za huko, kuleta teknolojia zinazofaa kwa nchi za Afrika, na kuimarisha uwezo wa kujiendeleza wa nchi za Afrika, na pia umekuwa nguvu kubwa ya kuhimiza ongezeko la uchumi wa Afrika. Wataalamu walikadiria kuwa biashara kati ya China na Afrika ilihimiza ongezeko la uchumi wa Afrika kwa asilimia 20.

Ili kustawisha uchumi wao, hivi sasa nchi nyingi barani Afrika zimetoa kipa umbele katika ujenzi wa miundo mbinu, katika miaka kumi ijayo ujenzi wa miundo mbinu barani Afrika inatazamiwa kuhitaji dola za kimarekani bilioni 250. Serikali ya China inafanya juhudi kuzihimiza na kuzihamasisha kampuni za China zenye nguvu na sifa nzuri zifanye ushirikiano wa miradi na nchi za Afrika kwa teknolojia zao na uzoefu wa usimamizi. Kampuni za China kushiriki kwenye ujenzi wa miundo mbinu ya huko, si kama tu kumeinua sifa ya miradi, bali pia kumepunguza gharama za ujenzi, na kuhimiza maendeleo ya uchumi na jamii za huko.

Wakati huo huo ongezeko la biashara kati ya China na Afrika lililopatikana kwa njia nzuri lilionesha umuhimu mkubwa katika kuinua kiwango cha maisha ya wananchi wa pande hizo mbili.

Bw. James Kipusan ambaye ni mfanyakazi wa kampuni moja mjini Nairobi, alimwambia mwandishi wetu wa habari kuwa, alinunua baiskeli iliyotengenezwa na China miaka mitano iliyopita, lakini hivi sasa baiskeli hiyo bado ni nzuri, kama baiskeli mpya. Bw. Kipusan alisema aliinunua baiskeli hiyo kwa shilingi elfu 5 miaka mitano iliyopita, lakini wakati ule baiskeli iliyotengenezwa Uingereza ilikuwa inauzwa kwa zaidi ya shilingi elfu 15. Alisema, kwa watu wasio na mapato makubwa kama yeye, bila shaka wanapenda kununua baiskeli iliyotengenezwa na China.

Bw. Kipusan alisema ana watoto watatu nyumbani, na wanapenda kuvaa nguo zenye sifa nzuri zilizotengenezwa na China. Alisema sifa nzuri na bei chini za bidhaa za China zinawavutia watu barani Afrika. Maoni ya mkenya huyo kuhusu bidhaa za China yanaonesha maoni ya watumiaji wengi wa Afrika. Katika miaka ya karibuni, bidhaa nyingi zilizotengenezwa nchini China zikiwemo baiskeli, pikipiki, televisheni na nguo zinapendwa na waafrika. Wakati huo huo, bidhaa za nchi mbalimbali barani Afrika zimeanza kuingia kwenye soko la China, na kupendwa na wachina wengi.

Hivi sasa China na Afrika ziko kwenye mwanzo mpya wa njia ya kuendeleza uchumi na kustawisha taifa, ushirikiano kati yao wenye msingi wa kunufaishana, umekuwa nguvu ya kusukuma mbele ongezeko la uchumi, na maendeleo ya jamii barani Afrika.

----------------------------------

Habari nyingine zinasema shirikisho la wasenegal waliosoma nchini China lilianzishwa tarehe 16 kwenye ubalozi wa China nchini Senegal. Balozi wa China nchini Senegal Bw. Lu Shaye na wafanyakazi wa ubalozi huo, wasenegal waliosoma nchini China, wajumbe wa shirikisho la wachina wanaoishi nchini Senegal, na wajumbe wa kampuni zilizowekezwa na wafanyabiashara wa China walishiriki kwenye sherehe ya kuanzishwa kwa shirikisho hilo.

Mkurugenzi wa shirika la wasenegal waliosoma nchini China Bw. Layman Diani kwenye sherehe hiyo alisisitiza kuwa, nia ya shirikisho hilo ni kuimarisha mawasiliano na ushirikiano kati ya wasenegal waliosoma nchini China, na kuuhimiza uhusiano na ushirikiano kati ya China na Senegal uendelezwe bila kusita.

Idhaa ya kiswahili 2007-12-21