Mahitaji: Samaki mmoja, nyama ya nguruwe gramu 100, karoti gramu 50, mvinyo wa kupikia vijiko vitatu, mchuzi wa sosi vijiko vitatu, sukari kijiko kimoja, siki kijiko kimoja, chumvi nusu kijiko, chembechembe za kukoleza ladha nusu kijiko, mafuta ya pilipili manga kijiko kimoja, sosi iliyotengenezwa na maharagwe, kiasi kidogo cha wanga, vitunguu maji na tangawizi.
Njia:
1. ondoa vitu vilivyo ndani ya tumbo la samaki, halafu osha samaki na umkate awe vipande, paka sosi iliyotengenezwa na maharagwe kwenye samaki. Washa moto mimina maji kwenye sufuria, weka vipande vya samaki kwenye sufuria vikaange, halafu vipakue.
2. washa moto tena, tia mafuta kwenye sufuria, tia vipande vya vitunguu maji na tangawizi, korogakoroga, tia vipande vya nyama ya nguruwe, vipande vya karoti korogakoroga, mimina mvinyo wa kupikia, siki, mchuzi wa sosi, sukari na chumvi baada ya kuchemka, tia vipande vya samaki, halafu punguza moto na funika kwa mfuniko pika kwa mvuke, baada ya sosi kukauka imekausha, ondoa vitunguu maji na tangawizi, tia chembechembe za kukoleza ladha, mimina maji ya wanga, korogakoroga, mimina mafuta ya pilipili manga. Pakua. Mpaka hapo kitoweo hiki kiko tayari kuliwa.
|