Mkoa unaojiendesha wa Tibet ulioko kwenye Uwanda wa Juu wa Qinghai-Tibet unajulikana kama paa la dunia na ncha ya tatu duniani. Kwenye mkoa huo, kuna wakazi wa makabila mbalimbail yakiwemo ya Watibet, Wahan, Wahui, Wamenba, Waluoba, Wanaxi, Wanu na Wadulong, na miongoni mwao watu wa kabila la Watibet ni wengi zaidi. Kutokana na hali mbaya ya kimaumbele, mkoa wa Tibet ulikuwa nyuma kimaendeleo ikilinganishwa na mikoa mingine nchini China, lakini sasa uchumi na jamii ya mkoa huo limeendelea kwa kasi. Wakati unapojiendeleza kiuchumi kwa nguvu, mkoa wa Tibet pia unazingatia uhifadhi wa mazingira.
Mkoa wa Tibet ni sehemu inayowavutia watu. Lakini Uwanda wa Juu wa Qinghai-Tibet ni uwanda wa juu zaidi duniani wenye miundo wa zaidi ya mita 4,000 kutoka usawa wa bahari, hivyo zamani ni vigumu sana kwa watu kuingia na kutoka kwenye mkoa huo, na kwa kawaida iliwachukua hata miezi kadhaa. lakini sasa hali imebadilika.
Wapendwa wasilikilizaji, mliousikia ni wimbo unaoitwa Njia ya Peponi unaosifu Reli ya Qinghai-Tibet. Mwimbaji huyu anaimba akisema, nilikaa juu ya kilima jioni, nikiangalia reli ikijengwa kwenye maskani yangu, reli hiyo inapanda na kuteremka milimani, imeleta heri kwa Uwanda wa Qinghai-Tibet, na hii ni njia ya ajabu ya peponi.
Reli ya Qinghai-Tibet ilijengwa na serikali ya China kwa kutumia yuan bilioni 33, na ilizinduliwa rasmi mwaka jana. Sasa watu wanaweza kufika Tibet kwa magari, garimoshi na ndege, tatizo kufika Tibet limeondolewa kabisa. Naibu mwenyekiti wa kamati ya mambo ya kawaida ya serikali ya mkoa unaojiendesha wa Tibet Bw. Hao Peng alisema,
"Reli ya Qinghai-Tibet imebadilisha kimsingi mawasiliano ya Tibet. Wakati huohuo shughuli za safari za ndege pia zimepata maendeleo mkoani Tibet, na hivi sasa viwanja vitatu vya ndege vimejengwa, na viwanja viwili vinaendelea kujengwa. Mbali na hayo urefu wa barabara kubwa mkoani humo umefikia kilomita elfu 45."
Baada ya kuondoa tatizo la mawasiliano, mkoa wa Tibet umepata watalii wengi kutokana na dini na utamaduni wake wenye umaalumu wa kabila la Watibet, na hivi sasa idadi ya watalii kwenye mkoa huo kwa mwaka imezidi milioni moja. Utalii umeleta manufaa makubwa kwa Tibet. Lakini serikali na wakazi wa Tibet wanajua kuwa, maziwa yenye maji safi na anga ya rangi ya buluu ya Tibet ni vitu muhimu vya kuwavutia watalii wa nje, mbali na hayo, mkoani Tibet pia kuna vyanzo vya mito mingi ya China na hata ya nchi nyingine za Asia. Hivyo serikali ya Tibet inazingatia sana shughuli za uhifadhi wa mazingira, wakati inapojitahidi kuendeleza uchumi, haiachi juhudi za kuhifadhi mazingira, na inazuia uchafuzi wa mazingira kutoka kwenye chanzo.
Kwa mfano, Reli ya Qinghai-Tibet ilipojengwa, mtizamo wa uhifadhi wa mazingira ulitiliwa mkazo kutoka mwanzo wa ujenzi hadi mwisho. Ziwa Cuona lililoko kilomita zaidi ya 400 kutoka Lhasa, mji mkuu wa Tibet, lenye eneo la kilomita zaidi ya 300 za mraba ni maskani ya wanyama wengi. Sasa ziwa hilo liko jirani na Reli ya Qinghai-Tibet, na sehemu zake zilizo karibu zaidi zikoumbali wa mita kumi kadhaa tu. Bw. Yan Peizun alikuwa mkuu wa ujenzi wa sehemu hiyo ya Reli ya Qinghai-Tibet, alisema,
"Ili kutochafua maji ya ziwa la Cuona, wakati tulipokuwa tukijenga reli kwenye sehemu ya ziwa hilo, tulijenga tuta kwa mifuko ya mchanga ili kuhakikisha maji."
Sasa Reli ya Qinghai-Tibet imekuwepo kwa zaidi ya mwaka mmoja, maji ya ziwa la Cuona bado ni safi, na wanyama wanaendelea kulichukulia ziwa hilo kama maskani yao.
Kuhifadhi mazingira ni maoni ya pamoja ya Wachina, sasa si kazi ya idara za serikali tu, bali pia kumechukuliwa na mashirika mengi ya umma nchini China kuwa ni jukumu lao. Shirika la kuhimiza kuhifadhi mazingira ya mito hivi karibuni liliandikisha watu wanaojitolea kwenye garimoshi linalopita kwenye Reli ya Qinghai-Tibet, ili kuwaeleza wasafiri namna ya kuhifadhi mazingira watakapofanya utalii mkoani Tibet. Mkuu wa shirika hilo Bw. Yang Xin alisema baada ya kuzinduliwa kwa Reli ya Qinghai-Tibet, watu zaidi ya laki tisa watafanya utalii mkoani Tibet kwa garimoshi, endapo hawafahamu umuhimu wa kuhifadhi mazingira kwenye mkoa wa Tibet, wataleta athari kwa mazingira mkoani humo. Bw. Ya Xin alisema,
"Baada ya kuzinduliwa kwa Reli ya Qinghai-Tibet, wingi wa watalii na usambazaji vitu umeleta shinikizo kubwa kwa mazingira kwenye mkoa wa Tibet. Hivyo tunapanga kutangaza mtazamo wa uhifadhi wa mazingira kwenye garimoshi kwa abiria kwenye garimoshi watakaofanya utalii mkoani Tibet."
Ili kuhifadhi mazingira, serikali ya Tibet inakataa kuinidhisha miradi inayoweza kuleta uchafuzi wa mazingira, na kuzingatia kuhifadhi mazingira katika ujenzi mkubwa. Aidha serikali ya Tibet pia inatumia hali bora ya sehemu na kuendeleza matumizi ya nishati safi, kwa mfano nishati ya jua. Bw. He Peng alisema,
"Mkoa wa Tibet ni mkoa unaopata mwangaza mwingi zaidi wa jua nchini China, na unapata mwangza wa jua kwa zaidi ya saa 3,000 kwa mwaka. Aidha kutokana na kuwa kwenye uwanda wa juu zaidi, Tibet iko karibu zaidi na jua, hivyo ina hali nzuri ya kutumia nishati ya jua."
Imefahamika kuwa uwezo wa vituo vya kuzalisha umeme kwa nishati ya jua mkoani Tibet umefikia kilowati elfu kumi, mbali na hayo vifaa vya kutumia nishati hiyo pia vimewekwa kwenye makazi ya wakulima wa mkoa huo, hata baadhi ya simu, radio na televisheni pia zinatumia nishati ya jua.
Aidha hifadhi saba za kimaumbile za ngazi ya taifa zimeanzishwa mkoani Tibet, maeneo ya hifadhi hizo yanachukua theluthi moja ya ardhi yote ya Tibet.
Kutokana na juhudi hizo, misitu, mito, maziwa, mbuga, milima yenye theluji, wanyama na mimea mkoani Tibet vinahifadhiwa vizuri, na maji na hewa vinaendelea kuwa na sifa nzuri.
|