Mwaka 1992, Bibi Shizuko alikwenda tena mjini Chengdu. Marafiki zake walimkaribisha sana na kumtendea vizuri. Baada ya hapo, alikwenda Chengdu mara nyingi kutalii. Mwaka 1997 alipata fursa ya kufanya kazi mjini Chengdu. Kutokana na mwaliko wa rafiki yake aliyefanya kazi huko kwenye shirika la utalii, alikuwa mshauri wa shirika hilo, kusaidia shirika hilo kutafsiri data husika. Yeye aliishi mjini Chengdu kwa mwaka mmoja..
Wakati alipozungumzia maisha yake mjini Chengdu, alisema kuwa lugha ya kichina ilikuwa ni vigumu kwake, lakini watu wa Chengdu walimsaidia kutatua tatizo hilo. alisema:
"Tatizo kubwa ni kwenda Benki. Wafanyakazi wa benki walinieleza fomu mbalimbali. Lakini wao waliongea lafudhi ya kisichuan, sikuweza kuelewa hata kidogo. Na nilipokwenda benki hiyo baadaye, wafanyakazi hao walinisaidia kujaza fomu zote nilizohitaji."
Bibi Shizuko alipenda sana kuishi mjini Chengdu. Kama ingewezekana angependa kuishi huko kwa muda mrefu. Lakini kutokana na sababu fulani, alilazimika kurudi nyumbani. Baada ya kurudi nchini Japan, alikumbuka sana maisha yake mjini Chengdu, hata alisimulia wakati alipotazama vipindi kuhusu Chengdu kwenye televisheni. Yeye alijifunza lugha ya kichina, kupata hati ya kufundisha lugha ya kijapan, na kuwafundisha wanafunzi wa China lugha ya kijapan bila malipo nchini Japan kwenye kituo cha vijana cha Japan. Mwaka 2003, Bibi Li Huiqun alimpigia simu na kumwambia kuwa amenunua nyumba mpya, kama Bibi Shizoko atakwenda Chengdu basi anaweza kukaa kwenye nyumba yake. Maneno hayo yaliongeza matumaini ya Bibi Shizoko kuishi mjini Chengdu.
Mwaka 2004, Bibi Shizuko alikwenda Chengdu tena na kufanya kazi kwenye shule ya lugha ya kijapan iliyoko kwenye Jumba la urafiki kati ya China na Japan la Chengdu. Lakini yeye alikuwa hapati mapato yoyote, alimudu maisha mjini Chengdu kwa akiba yake. Kutokana na hali hiyo, Bibi Shizuko alitoa ombi la kukaa kwenye nyumba ya Bibi Li Huiqun. Li Huiqun na mume wake walikubali kwa furaha. Bibi Li Huiqun alisema:
"ninafurahia yeye kuishi kwenye nyumba yangu. Ninafurahi sana. Yeye ananiamini, na mimi ninamwamini. Ninapenda kumtendea kama dada yangu, na yeye ananitendea kama jamaa yake. Tunaishi kwa pamoja vizuri. Yeye alikuja Chengdu kufanya kazi, sisi wakazi wa Chengdu tunapaswa kumtendea vizuri."
Na wakati huo, yeye alikaa mjini Chengdu kwa miaka mitatu zaidi. Alipozungumzia mabadiliko ya Chengdu aliyoshuhudia, alisema,
"Majengo marefu yanasimama, magari yanaongezeka, madaraja ya barabara ya mwendo kasi pia yanajengwa. Nikilinganisha na mji wa Hiroshima, hakuna mabadiliko hata kidogo katika miaka ya hivi karibuni. Lakini mji wa Chengdu unabadilika sana. Zamani nilipokuja hapa, niliona mji huo ni kama wilaya, lakini sasa ni mji mkubwa. Sababu kubwa ya mabadiliko hayo ni maendeleo ya kasi ya uchumi wa China."
Wakati alipoishi nyumbani kwa Bibi Li Huiqun, alisaidiawa sana Bibi Li Huiqun na mume wake katika maisha yake, hivyo anaweza kufuatilia tu kazi yake ya kufundisha.
|