Wafanyakazi wa Idhaa ya Kiswahili ya CRI
China Radio International
China
Dunia
(GMT+08:00) 2008-01-18 18:29:29    
Bidhaa za China zinakaribishwa nchini Kenya

cri

Katika miaka ya hivi karibuni, biashara kati ya China na Kenya iliendelezwa kwa kasi. Takwimu zilizotolewa na idara ya forodha ya China zinaonesha kuwa, mwaka 2006 thamani ya jumla ya biashara kati ya China na Kenya ilifikia dola za kimarekani milioni 646, na kuongezeka kwa asilimia 36.1 kuliko mwaka 2005, ambayo ilifikia kiwango cha juu kabisa katika historia. Thamani hiyo kwa mwaka 2007 inatazamiwa kuongezeka zaidi. Hivi sasa bidhaa zilizouzwa na China kwa Kenya ni pamoja na mashine?vyombo vya umeme, nguo, bidhaa zenye teknolojia mpya ya hali ya juu, magari, na pikipiki. Hivi sasa nchini Kenya, bidhaa za China zinauzwa katika maduka makubwa, supamaketi, na vibanda mitaani.

Meneja mkuu wa kituo cha maduka cha Paradise mjini Nairobi hivi karibuni alipohojiwa na mwandishi wa habari wa shirika la habari la China, Xinhua alisema, bidhaa za China zinauzwa kwa haraka, kwa sababu zina sifa nzuri na bei nafuu. Kwa wafanyabiashara, bidhaa zinazoleta faida haraka ni bidhaa nzuri.

Kituo hicho cha maduka kinashughulikia uuzaji wa bidhaa za China, zikiwemo radio, televisheni, na nguo mbalimbali. Meneja mkuu huyo alimwambia mwandishi wa habari kuwa, hivi sasa utoaji wa bidhaa za aina mbalimbali katika kituo hicho ni wa kutosha, hali hiyo inanufaishwa na bidhaa nyingi zilizotengenezwa na China. Mkazi mmoja mwanamke alimwambia mwandishi wa habari kuwa, maduka yote yaliyoko karibu na nyumbani kwake yanauza bidhaa za China, ambazo bei zake ni za chini kuliko bei ya bidhaa zilizotengenezwa na nchi nyingine.

Mfanyabiashara wa Kenya anayeshughulikia uuzaji wa bidhaa za China mjini Nairobi alisema, wachina hujiendeleza kwa njia tofauti na njia ya magharibi. Alisema wachina wanatengeneza bidhaa kwa watu maskini, wanatumia teknolojia kuwahudumia watu maskini, wanatengeneza vyombo vinavyotumia umeme, nguo na mashine wanazoweza kununua watu maskini, na wachina wanatumia utamaduni, busara na jadi yao kujenga dunia iliyo tofauti na magharibi.

Licha ya kuwa na bei za chini, bidhaa za China pia zinakaribishwa hatua kwa hatua na maduka na wateja wa huko kwa sifa nzuri. Mkurugenzi wa duka kubwa mjini Nairobi alisema, usanifu, sifa na bei ya bidhaa za China zote ni nzuri kuliko bidhaa za Kenya, hivyo zinakaribishwa na wateja.

Kampuni ya mawasiliano ya habari "Cellcare" ya mjini Nairobi inashughulikia uuzaji wa vifaa vinavyotumia umeme vya China, zikiwemo zana za kompyuta na simu za mkononi. Kampuni hiyo pia ni mfanyabiashara mkubwa wa bidhaa za kampuni ya Huawei ya China inayouza zana za simu za nyumbani. Meneja mkuu wa kampuni hiyo alimwambia mwandishi wa habari kuwa, ingawa bidhaa za China bado zinatakiwa kuboreshwa zaidi, lakini anaridhika na sifa ya bidhaa hizo.

Wakazi wachache wa huko hawaridhiki na baadhi ya bidhaa bandia na zenye sifa mbaya kutoka China. Waziri wa biashara na viwanda wa Kenya alisema, bidhaa nyingi zaidi za China zina sifa ya ngazi ya kimataifa. Kuhusu kupambana na bidhaa chache za bandia na zenye sifa mbaya, Kenya inashirikiana na China na kupambana na bidhaa hizo.

Waziri wa fedha wa Kenya alisema, "kampuni za China zina nguvu kubwa ya ushindani. Sote tunapaswa kujiuliza, kwa nini kampuni za China zina nguvu kubwa ya ushindani? Tunapaswa kutumia fursa ya maendeleo ya uchumi wa China, na kujifunza kwa makini uzoefu wa maendeleo ya China."

......................................................................

Kama ukiingia kwenye duka lolote au kibanda chochote huko Cairo, mji mkuu wa Misri, utaona bidhaa nyingi ni za kutoka China. Kutokana na maendeleo ya biashara kati ya China na Misri, bidhaa ndogo zenye sifa nzuri na bei nafuu zilizotengenezwa na China, zimeingia kwenye maisha ya watu wa Misri, na kuwa sehemu moja isiyokosekana kwenye maisha ya watu wa kawaida nchini Misri.

Kwenye supamaketi moja mjini Cairo, mwandishi wetu wa habari alikutana na mteja wa huko, ambaye alinunua seti moja ya vyombo kuhifadhia mishumaa vilivyotengenezwa na China, alisema usanifu na sifa ya vyombo alivyonunua ni nzuri. Vilevile alisema kama bidhaa za nchi nyingine yoyote, bidhaa za China pia zina sifa nzuri au sifa mbaya, wateja wanahitaji kufanya chaguo kwa makini.

Muuzaji wa supamaketi hiyo alijulisha kuwa, vitu vingi vya kuchezea watoto vinavyouzwa kwenye supamaketi hiyo vilitengenezwa na China na vinapendwa sana na wateja.

Bw. Sayid ni kijana wenye umri wa miaka zaidi ya 20, ana duka la zana za muziki za magari mjini Cairo. Alijulisha kuwa licha ya zana za muziki za magari anazouza kutoka Thailand, zana nyingine zote ni kutoka China. Bw. Sayid alisema, zana nyingi zaidi za muziki za China zina sifa nzuri, ikilinganishwa na bidhaa za Ulaya, Marekani na Japan, bei ya bidhaa za China zinafaa zaidi kwa soko la Misri. Alipozungumza na mwandishi wa habari, simu yake iliita Bw. Sayid akamwonesha mwandishi wa habari simu yake ya mkononi, alisema simu hiyo pia imetengenezwa China.

Mfanyakazi mmoja wa kampuni moja ya Misri alisema hivi sasa watu wa kawaida wa Misri wanatumia zaidi bidhaa za China, hasa bidhaa ndogo zinazotumika kwenye maisha ya kawaida. Alisema anapenda kununua bidhaa ndogo za elektroniki zilizotengenezwa China kwa mfano wa sufuria ya umeme ya kupikia wali na mashine ya kukaushia nywele. Alisema bidhaa hizo ndogo zina bei ya chini, na pia ni rahisi kuzitumia.

Mfanyakazi huyo alisema kutokana na kuinuka hatua kwa hatua kwa kiwango cha maisha ya watu wa Misri, matakwa yao kwa sifa ya bidhaa yanazidi kuongezeka, na watu wa kawaida wa Misri wana matumaini kuwa bidhaa nyingi zaidi zenye sifa nzuri kutoka China zitaweza kusafirishwa kwenda Misri.

Idhaa ya kiswahili 2008-01-18