Kutokana na kuimarika kwa uhusiano kati ya China na Kenya, katika miaka ya hivi karibuni wachina wengi wamekuwa wakienda nchini Kenya kutalii, wengi wao wametimiza matumaini ya kutembelea mbuga za wanyama barani Afrika kwa kupitia shirika la utalii wa Kenya la China. Akiwa maneja mkuu wa shirika hilo, Bw. Zhang Yuanxiang anajiita mwenyewe kuwa ni mtu asiye na kazi rasmi. Alipohojiwa na mwandishi wetu wa habari, Bw. Zhang Yuanxiang alisema, "Mimi ni mfanyabiashara, kwa kweli ninafanya biashara, lakini sijiyumbukizi kwenye shughuli za biashara."
Bw. Zhang Yuanxiang alifika nchini Kenya mwaka 1999, na alianzisha shirika la utalii kati ya China na Kenya mjini Nairobi. Katika miaka kadhaa iliyopita, Bw. Zhang na wafanyakazi wa shirika hilo walifanya juhudi kubwa, na shirika hilo lilipata maendeleo makubwa. Wakati matawi ya shirika hilo yalipongezeka, Bw Zhang alikuwa anaonekana ofisini mara chache, kwa sababu Bw. Zhang alikuwa anasafiri mara kwa mara kati ya China na Kenya. Bw. Zhang alisema nia yake ya mwanzo ya kushughulikia mawasiliano ya utamaduni kati ya China na Afrika, ilikuwa ni kutaka kuhimiza maendeleo ya zaidi ya matawi ya shirika lake la utalii. Alisema, (sauti2)
"kwa sababu mawasiliano hayo ya utamaduni hakika yanaweza kuhimiza maendeleo ya shughuli za utalii. Kuwafanya wachina wengi zaidi waelewe Afrika, na kutembelea bara la Afrika wao wenyewe, kutahimiza maendeleo ya utalii. Hivyo kwa upande mwingine, kushughulikia mawasiliano ya utamaduni pia ni njia ya kuhudumia matawi ya shirika la utalii wa Kenya la China."
Lakini kutokana na maendeleo ya mawasiliano ya utamaduni kati ya China na Kenya aliyoshuhudia, Bw. Zhang Yuanxiang aliona kuwa anazidi kuvutiwa na mambo hayo. Hasa alipoona kuwa wananchi kati ya China na Kenya hawafahamiani vizuri, Bw. Zhang alitambua amepata nafasi kubwa ambapo anaweza kufanya mambo mengi zaidi. Alisema,
"walipozungumzia wachina, wakenya wengi walitaja filamu za Gongfu za China, lakini filamu hizo kabisa haziwezi kuonesha kikamilifu sura ya China, hasa sekta ya utamaduni ya China. Ingawa wakenya wana urafiki na wachina, lakini urafiki tu hautoshi, inapaswa kuzidisha mawasiliano ya utamaduni kati yao, ili kuwafanya wakenya wawasiliane na wachina, na kuelewa utamaduni wa China, hivyo uhusiano kati ya wachina na wakenya utakuwa wa kiwenzi halisi. "
Ili kufanikisha nia hiyo, katika miaka kadhaa za karibuni, Bw. Zhang Yuanxiang kwenye shirika la mpango wa mazingira duniani aliandaa maonesho ya picha zilizopigwa na mpiga picha wa China Bw. Luo Hong, ambayo mada yake ni mazingira. Baadaye aliwashirikisha watu wenye ujasiri kutembelea kwenye ncha tisa duniani kwa ajili ya kutangaza michezo ya Olimpiki ya mwaka 2008 mjini Beijing. Bw. Zhang pia alianzisha mfululizo shughuli za utamaduni zenye kauli mbiu ya "nalipenda bara la Afrika", ambayo inawafahamisha wachina ubora wa mbuga za Afrika kwa njia ya vitabu, picha, na Internet. Bw. Zhang alileta sampuli za ndege za makumbusho ya Afrika nchini China, na kuwafanya wachina wasio na nafasi ya kuwasili Afrika waweze kuona uzuri wa Afrika. Tangu mwaka 2004, Bw. Zhang Yuanxiang aliongoza wakimbiaji wa Kenya kuja mjini Beijing, Shanghai, Xiamen na Yangzhou, ili kushiriki kwenye mashindano ya kimataifa ya marathon. Mwishoni mwa mwezi huu, Bw. Zhang ataongoza wakimbiaji wa Kenya kwenda mjini Xiamen kushiriki kwenye mashindano ya kimataifa ya mbio ya marathon. Alisema, "Nitaongoza wakimbiaji watano kwenda mjini Xiamen, miongoni mwao kuna wakimbiaji wawili maarufu. Nafikiri mara hii kuna uwezekano wa kuvunja rekodi, nina matumaini kuwa watavunja rekodi ya mashindano ya kimataifa ya mbio ya marathon mjini Xiamen."
Bw. Zhang Yuanxiang si kama anawaleta wachezaji wa Kenya nchini China tu, bali pia anafanya juhudi kuwapeleka wachezaji wa China nchini Kenya ili wakafanye mazoezi. Wakati huo huo anafanya juhudi ili kuandaa kituo cha maingiliano ya utamaduni kati ya China na Afrika, Bw. Zhang anataka kupanua eneo la mawasiliano ya utamaduni kati ya China na Kenya hadi sehemu ya Afrika ya mashariki. Kama alivyosema alipohojiwa na mwandishi wetu wa habari, alisema bora awe balozi wa kushughulikia maingiliano ya utamaduni kati ya China na Afrika kuliko kufanya kazi za biashara.
|