Wafanyakazi wa Idhaa ya Kiswahili ya CRI
China Radio International
China
Dunia
(GMT+08:00) 2008-02-13 20:16:13    
Matibabu ya jadi ya kichina

cri

Katika miaka ya hivi karibuni, watalii wengi zaidi kutoka Russia wanapenda kutembelea mji wa Sanya mkoani Hainan wakati wa siku za baridi nchini Russia, kwa kuwa Sanya iko kwenye sehemu ya kitropiki, mbali na mwangaza wa jua, bahari na ufukwe, na chemchem, shughuli maalumu za aina mbalimbali za matibabu ya jadi ya kichina si kama tu zinawaburudisha bali pia zimewasaidia kujenga afya.

Katika hospitali ya matibabu ya jadi ya kichina mjini humo, Bi. Alyssa alikuwa analala na kupewa matibabu ya akupancha. Mwandishi wetu wa habari alizungumza naye.

"Mwandishi: unatoka wapi?

Bi. Alyssa: natoka Chita.

Mwandishi: umekuja kwa ajili ya kupewa matibabu?

Bi. Alyssa: ndiyo, nitapewa matibabu hapa kwa siku 10.

Mwandishi: wapi umepata kujua kwamba hapa kuna matibabu ya jadi ya kichina?

Bi. Alyssa: marafiki wengi waliniambia na mwongoza watalii pia aliniambia.

Mwandishi: unaonaje matibabu ya jadi ya kichina?

Bi. Alyssa: bila shaka ni mazuri sana, matibabu mazuri kabisa ni matibabu ya jadi ya kichina!"

Matibabu ya jadi ya kichina yanatumia mbinu za kifizikia pamoja na dawa za mitishamba ya kimaumbile. Kuanzia mwaka 2002, hospitali ya matibabu ya jadi ya kichina ya Sanya imeimarisha ushirikiano kati yake na sekta ya matibabu ya jadi ya nchi za nje na kuunganisha matibabu ya jadi ya kichina pamoja na shughuli za utalii. Watalii wengi kutoka Russia waliochagua kutembelea Sanya asubuhi watafanya matembezi mjini humo, alasiri watapewa matibabu ya jadi kwenye hospitali na kujiburudishia kwa udaktari wa jadi wa kichina.

Mkuu wa hospitali hiyo Bw. Liu Dexi alipozungumzia sababu kuwa kivutio hicho maaluma kinakaribishwa na watalii wa Russia alisema, watalii wengi kutoka Russia wanasumbuliwa na magonjwa sugu yakiwemo magonjwa ya viungo, rheumatism, shinikizo kubwa la damu na tatizo la uzito kupita kiasi. Matibabu ya jadi ya kichina yanatumia tu dawa za kimaumbile zenye athari ndogo mbaya kwa afya, pamoja na hali ya kitropiki mjini Sanya, hali hizo zote zimeufanya mji humo kuwa sehemu nzuri ya kujiburudisha kwa maisha ya kiafya.

Baada ya kupewa matibabu hayo, watalii wengi wao walijisikia vizuri na magonjwa yao yalipona kiasi. Hivi sasa watalii wengi zaidi kutoka Russia wamekubali na kupokea matibabu ya jadi kwa njia ya akupancha, usingaji na kuoga kwenye maji yaliyotiwa dawa.

Bw. Ivan mwenye umri wa miaka 58 alitembelea mjini Sanya mara mbili. Kila safari alichukua muda kupewa matibabu ya jadi kwenye hospitali. Bw. Ivan alisema, kutokana na matibabu hayo, maumivu kwenye shingoni na nyuma yake yamepungua sana. Bw. Ivan alisema:

"katika majira ya siku za joto, sina nafasi kwa sababu ya kazi; katika siku za baridi, nitakuja kupewa matibabu kuhusu ugonjwa wa shingo. Naona matibabu hayo ni ya jabu sana."

Kuanzia mwanzoni mwa mwaka 2002, baadhi ya watu waliojeruhiwa kwenye ajali ya uvujaji wa nyuklia katika kituo cha kuzalisha umeme kwa nishati ya nyuklia cha Chernobyl nchini Russia waliwahi kupewa matibabu hayo kwa muda mjini Sanya. Mwezi Machi mwaka huo, kampuni ya mafuta na gesi ya kimaumbile ya taifa ya Russia ilisaini mkataba wa utalii wa miaka mitano na hospitali ya matibabu ya jadi ya Sanya, kila mwaka maelfu ya wafanyakazi wa kampuni hiyo watapelekwa mjini humo kupewa matibabu. Aidha, katika mwaka 2006 na 2007, watoto walioathiriwa kwenye tukio la utekaji nyara lililotokea huko Beslan nchini Russia pia waliwahi kupelekwa mjini humo ili kupewa matibabu ya kurejesha afya. Mbinu za kuunganisha matibabu ya kisasa na ya jadi ya kichina pamoja na shughuli nyingi za michezo na maburudisho zimesaidia watoto hao waondokane na majeraha yao katika miwili na roho.

Ili kukidhi mahitaji ya nchini na kutoka nchi za nje, kuanzia mwaka huu mji wa Sanya umeanza kuharakisha maendeleo ya shughuli za utalii pamoja na maburudisho ya kimatibabu. Kituo cha kurejesha afya cha matibabu ya jadi ya kichina cha kimataifa cha Sanya kimepangwa kujengwa, kituo hicho ni pamoja na kituo cha kurejesha afya, kituo cha kutoa mafunzo na kituo cha maburudisho ya kimatibabu. Serikali ya mji huo pia imethibitisha shughuli za kuuendeleze mji huo uwe "mji wa afya" kuwa lengo la kazi katika siku za baadaye, na itafanya juhudi kuujenga mji huo uwe kituo maarufu cha kurejesha afya kwa matibabu maalumu ya jadi ya kichina duniani. Naibu katibu mkuu wa shirikisho la utalii la mji huo Bw. Li Qingxian alisema:

"utalii pamoja na maburudisho ya kimatibabu unapendwa na watu wa Russia, mji wa Sanya utaendelea kuunga mkono maendeleo ya shughuli hizo, ili ziweze kutoa huduma kwa watalii wengi zadii wa nchi za nje na kutoa bidhaa nyingi zaidi zinazowafahamisha watalii hao kuhusu utamaduni wa China."